Posts

Showing posts from October, 2020

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

DUNIA INA UMRI GANI KIBIBLIA?

  Kulingana na hesabu ya vizazi na miaka yao waliyoishi katika biblia, inakadiriwa tangu Edeni mpaka wakati wa Gharika, ni miaka elfu 2, na tangu wakati wa gharika mpaka kuzaliwa kwa Bwana Yesu ilipita miaka elfu 2 hivi, na tangu kipindi cha Bwana wetu Yesu hata leo nacho pia ni kipindi cha miaka elfu 2 kimepita. Kwahiyo jumla yake tangu Edeni mpaka sasa ni miaka kama elfu 6 hivi, au imezidi kidogo au imepungua kidogo..Sasa kumbuka huo ulikuwa ni mwanzo wa Edeni, lakini haukuwa mwanzo wa Dunia..dunia ilikuwepo kabla ya Edeni..Tunasoma.   Mwanzo 1:1 “hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”   …hapa hajasema huo mwanzo ulikuwa ni wa miaka mingapi iliyopita inaweza ikawa ni miaka elfu kumi,milioni kumi au vinginevyo…   lakini mstari wa pili unasema nayo nchi ilikuwa ukiwa na utupu inamaanisha kuwa kuna jambo lilitokea likaifanya hiyo nchi kuwa ukiwa baada ya Mungu kuziumba mbingu na nchi na hapa si mwingine zaidi ya shetani ndiye aliyeiharibu na kuifanya ukiwa (kama anavyoendelea kuiha