Posts

Showing posts from January, 2019

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

UKRISTO BARANI AFRIKA

Image
Ukristo barani Afrika una historia ndefu inayokaribia miaka elfu mbili. Wakati mwingine tunaweza kusikia kuwa Ukristo uliingizwa Afrika juzijuzi tu, na asili yake ni Ulaya. Hili si kweli. Ukristo ni imani ya kale sana katika Afrika. Tangu mwanzo wa Kanisa walikuwepo Wakristo Waafrika. Ukristo uko Afrika katika wingi wa madhehebu yaliyopatikana katika historia ya Kanisa, baadhi katika bara hilo, baadhi katika mabara mengine. Kwa sasa ndiyo dini kubwa zaidi barani, hasa Kusini kwa Sahara, pamoja na Uislamu ambao unaongoza Kaskazini kwa jangwa hilo. Leo karibu nusu ya Waafrika wote ni Wakristo. Lakini asilimia ya Wakristo inaweza kuwa ndogo katika nchi kadhaa na kubwa katika nchi nyingine. Katika Afrika Kaskazini Wakristo ni wachache. Kumbe ni wengi kwa theluthi mbili za bara kusini kwa Sahara. Kwa jumla Wakristo wanaishi kati ya wafuasi wa dini nyingine, hasa Uislamu na dini za jadi. Idadi yao inaongezeka haraka sana. Kila baada ya nukta nne Mwafrika mmoja anaingia Ukristo. Wengine huz…

JINSI YA KUMPENDA NA KUMTHAMINI MKEO KWA KUTUMIA BIBLIA

Image
Je, unajua mambo yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke?

Waefeso 5:25, 28-29 
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa”

Mume kumpenda mke ni agizo. Agizo hili halibadiliki mke akiwa mkorofi, sio mtii au vyovyote vile. Biblia inamuagiza mume ampende mke kama Kristo alivyolipenda Kanisa. Huu ni upendo mkubwa sana, japokuwa kanisa lilikengeuka mbali naye bado upendo wa Kristo haukubadilika. Kumpenda mwanamke kama mwili wako mwenyewe, kumjali na kumtunza.

Akiwaandikia waume Wakristo kuhusu jinsi wanavyopaswa kuwatendea wake zao, Petro, mwandikaji aliyeongozwa na roho, aliwahimiza waige mtazamo wa Mungu na Yesu Kristo. ‘Enyi waume, endeleeni kuwapa heshima,’ akaandika. (1 Petro 3:7) Kumpa mtu heshima hutoa wazo la kwam…

HIVI UNAJUA MJI WA NINAWI UPO IRAKI?

Image
Ninawi (kwa Kiakadi: Ninwe; kwa Kiashuru: ܢܸܢܘܵܐ; kwa Kiebrania נינוה , Nīnewē; kwa Kigiriki Νινευη, Nineuē; kwa Kiarabu: نينوى, Naīnuwa) ulikuwa mji mkuu wa Waashuru upande wa mashariki wa mto Tigri. Magofu yake yako ng'ambo wa mto huo ukitokea Mosul (Iraki). Katika Biblia ni maarufu hasa kutokana na habari zinazopatikana katika kitabu cha Yona na zilizotumiwa na Yesu kuhimiza toba. Mji huu ulikuwa mkubwa kuliko yote duniani kwa miaka hamsini hadi mwaka 612 KK uliposhindwa na Wababuloni. Kitabu katika Agano la Kale ambacho kinaelezea juu ya tukio moja katika maisha ya Yona. Yona yawezekana hakuandika kitabu hiki yeye mwenyewe. Wazo kuu la kitabu cha Yona ni kwamba Yehova anatawala kila mahali na upande wake hauzuiliwi katika taifa moja au watu fulani tu. Katika mlango wa 1, Bwana anamwita Yona kwenda kuhubiri Ninawi. Badala ya kufanya kama Bwana alivyomwamuru, Yona alitoroka kwa mashua na akamezwa na samaki mkubwa. Katika Mlango wa 2, Yona alisali kwa Bwana, na yule samaki akamta…

MBINGUNI, PEPONI, KUZIMU NA JEHANNAM NI WAPI?

Image
Mpendwa mmoja aliniuliza maswali yafuatayo ambayo nimeona ni muhimu niyajibu kama Makala fupi kwa ajili hata ya faida ya watu wengine wenye maswali kama haya: Swali la 1: Hivi watu wakifa, roho zao zinakuwa wapi hasa?
Swali la 2: Roho hizo zinakuwa katika hali gani hasa? WATU WAKIFA, ROHO ZAO ZINAKUWA WAPI? Biblia inasema kuhusu Bwana Yesu kuwa: Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; (Wafilipi 2:9-10). Kulingana na mstari huu, tunagundua kuwa kuna sehemu kuu tatu:
Mbinguni
Duniani
Chini ya nchi Mbinguni ni mahali aliko Mungu; duniani ni mahali tuliko sisi wanadamu tulio hai; na chini ya nchi ni mahali aliko ibilisi. Tangu nyakati za Adamu kulikuwapo wanadamu wema na waovu. Wanadamu wema walikufa na waovu nao walikufa. Swali ni kuwa, je, walipokufa walienda wapi? Mwinjilisti Luka anatupatia picha nzuri kutokana na kisa alichosimulia Bwana Yesu juu …

ALLAH NA MUHAMMAD WASEMA KUWA JUA LINAZAMA KWENYE TOPE

Image
1. Je, ni kweli kuwa Allah aliumba kila kitu?
2. Je, kuna ushahidi wowote ule wa kisayansi kuwa Jua linazama kwenye tope?
3. Je, Muhammad ni kweli aliliona Jua likizama kwenye tope? Ndugu msomaji, Huu ni Msiba kwa Waislam wote wanao sema kuwa Allah aliumba kila kitu na Muhammad ni Mtume wake. Zul-Qarnain na Kutua kwa Jua katika Sura 18:85-86 Je, ni kweli kuwa jua linazama katika chemichemi za maji zenye tope au giza, au Koran ina makosa, au kuna maelezo mengine? Kwanza tutaangalia maana ya wazi Sura ya 18:85-86, na kisha tutaangalia maelezo na majibu ya baadhi ya Waislam kuhusu jambo hili. UNAJIMU KIDOGO
Inawezekana kuwa haijulikani kwa mapana kwamba watawala wa kislam wa Abbasid, Waarabu na Waajemi waliendelea sana katika unajimu, wakizipa majina nyota nyingi, hata walinukuru na kusahihisha baadhi ya orodha za hesabu za watawala wa Misri (Ptolemy’s tables). Hata hivyo jua ni kubwa mara nyingi zaidi ya dunia nzima, na dunia husafiri ikilizunguka jua. Jua halizami katika chemichemi za maj…

UTAFUTENI UFALME WA MUNGU NA HAYO YOTE MTAONGEZEWA

Image
Ufalme wa Mungu (au Ufalme wa mbinguni unavyoitwa hasa katika Injili ya Mathayo) ni mojawapo kati ya mada kuu za ujumbe wa Yesu Kristo katika Injili . Neno "ufalme" (kwa Kigiriki βασιλεία, Basileia) linapatikana mara 162 katika Agano Jipya, kawaida kwa maana ya Basileia tou Theou (βασιλεία τοῦ θεοῦ), Ufalme wa Mungu, au Basileia tōn Ouranōn, (Βασιλεία τῶν Ουρανῶν), Ufalme wa Mbinguni. Kwa uwazi, ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu wa milele, Mwenye nguvu juu ya ulimwengu wote. Vifungu vingi vya Maandiko vinaonyesha bila kupinga kuwa Mungu ndiye Mfalme wa viumbe vyote: "Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote" (Zaburi 103: 19). Na, kama Mfalme Nebukadineza alivyosema, "Ufalme wake ni ufalme wa milele" (Danieli 4: 3). Kila mamlaka iliyopo imeanzishwa na Mungu (Warumi 13: 1). Kwa hiyo, kwa maana moja, ufalme wa Mungu unahusisha kila kitu ambacho kilichoko. "Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hay…

NINAWEZAJE KUWA MWANA WA MUNGU?

Image
1 Yohana 5:11-12 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Mkutadha huu watwambia ya kwamba Mungu ametupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe, Yesu Kristo. Katika maneno mengine, njia ya kuumiliki uzima wa milele ni kumkubali Mwana wa Mungu. Swahili ni, mtu anawezaje kuwa na Mwana wa Mungu? Isaya 59:2 Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso Wake msiuone, hata hataki kusikia maombi yenu. Warumi 5:8 Bali Mungu aonyesha pendo Lake Yeye Mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Kulingana na Warumi 5:8, Mungu alionyesha pendo Lake kwetu sisi kwa njia ya mauti ya Mwanawe. Kwa nini ilimpasa Kristo kutufia? Kwa sababu Andiko la tangaza watu wote kuwa wafanya dhambi. Kufanya "dhambi" kuna maanisha kukosa alama. Biblia inatangaza "wote wa…

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA

Image
Tangu mapema kabisa Mungu wetu anatufundisha kwamba, mbingu na nchi za sasa zitachakaa na kuharibika, na kama mavazi, Mungu atazibadilisha Zaburi 102:25 Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako. 26 Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu Naam, hizi zitachakaa kama nguo; Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika. Nchi ya sasa yaani dunia hii au ulimwengu, umechosha na kuchakaa mno Baaya ya kukaliwa na mamilioni ya wenye dhambi wanaofanya machukizo mbele za Mungu. Dunia hii imechakazwa kwa gharika wakati wa Nuhu na vita vya kila namna mpaka vita ile ya mwisho “GOGU NA MAGOGU”. Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena. Watu wengi wako na dhana potovu juu ya mbinguni itakuwa kama nini. Ufunuo mlango wa 21-22 yatupa kiupana picha kamili ya mbingu mpya na nchi mpya. Baada ya matukio ya nyakati za mwisho, mbingu ya sasa na nchi ya sasa zitatolewa na zibad…

LA IILAHA 'IILAA YASUE ALMASIH

Image
LA IILAHA 'IILAA YASUE ALMASIH 

Kama wewe ni Muislam na umesoma "LA IILAHA 'IILAA YASUE ALMASIH" basi teyari wewe umesha MKANA ALLAH NA MUHAMMAD WAKE. Wewe sasa ni Mkristo na sio Mfuasi wa Allah.

Karibu sana kwenye Ukristo kwenye upendo na amani na uhakikisho wa uzima wa milele kupitia Yesu Kristo.

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

AMINI KWA KURATARAJIA YASIYOWEZA KUTARAJIWA

Image
Katika maisha ya kawaida mwanadamu yeyote anataka awe na usalama wa maisha, kwa mfano awe na nyumba nzuri na mali za kutosha na labda biasha kubwa inayo muingizia kipato kizuri; Lakini, matakwa haya ya binadamu si mara zote yanakuwa kama tupendavyo na wakati mwingini maisha yanaweza kuwa magumu kiasi cha kujiuliza, hivi Mwenyezi Mungu yupo wapi?
Mambo yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.” (Luka 18:27)
Yesu anatuambia katika Luka 18 aya ya 27 kwamba, yote yasiyo wezekana kwa Mwanadamu, yanawezakana kwa Mungu. Je, ni jambo gani basi tufanye ili tuweze kupokea baraka za Mungu?
Hebu tumsome Abraham na tujifunze yeye alifanya nini mpaka akawa na Isaka ambaye alimpata uzeeni.
Warumi 4: 18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya…