SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

UNAWAJUWA MALAIKA MASERAFI?

Image may contain: text

Kuna maserafi na wana mabawa sita (angalia Isaya 6:2,6). Wana nguvu uwezo wa kuondoa makosa yaletayo dhambi na kuwandaa manabii kwa kuwatakasa (Isaya 6:7).Kuwa na mabawa sita inadhihirisha ukuu na uwezo wao katika katika utendaji wao wa kazi mbalimbali.
Neno maserafi ni neno la wingi wa neno saraph (SHD 8314) likiwa na maana ya mwenye kuchoma kwa moto. Kwa sababu ya nyoka katika Hesabu 21:6,8 walikuwa na sumu inayochoma kama moto wakati wanapouma, kwa hiyo wakaitwa maserafi. Kwa hiyo hawa maserafi ni “kama moto wa mbinguni” (linganisha pia Kum. 8:15; Isaya 14:29; 30:6). Mungu aliwatuma ili waweze kuwadhibu watu waliotenda dhambi. Maumbile yao walionekana kuwa kama wandamu kwa vile walikuwa na nyuso, mikono na miguu juu ya umbile lao la kuwa na mabawa. Wanawakilishwa kama wenye “kusimama wakati wote” juu ya wote. Mfalme anaposimamisha enzi yake, tayari kwa kumhudumia.
Hawa ndiyo Malaika Wakuu na wana nafasi muhimu sana katika Jeshi la mbinguni. Ni Malaika wakuu ndiyo mara nyingi hutumwa katika nchi kuleta ujumbe wa Mungu na maonyo kwa wanadamu na kwa manabii.
Katika kitabu cha Henoko kinataja majina ya Malaika wakuu sita:
Mikaeli (Mkuu wa sehemu mhimu sana ya wanadamu) Gabriel (Mkuu, Bustani na wa Makerubi), Urieli Malaika Mkuu wa dunia na watu wakali) na Raphaeli (Malaika Mkuu wa Roho za wanadamu), Ragueli (ambaye analipiza kisasi juu ya dunia na mwangaza) na Saragaeli (Malaika Mkuu wa watoto wa wanadamu, ambao Roho zao wametenda dhambi).
Kitabu cha Henoko, sura ya 20, R.H Charles, 2002).
Malaika hawa pia wanaitwa Malaika Walinzi.

Comments

TRENDING NOW

OMBA MAOMBI HAYA KILA SIKU ASUBUHI, MCHANA NA USIKU

MAOMBI YA KUMTEKETEZA SHETANI "NGUVU ZA GIZA"

MAOMBI YA VITA YA KUTUMIA ALAMA ZA MUNGU

NANI KAMPA UTUME NA UNABII MTUME MUHAMMAD?