Sunday, September 10, 2017

OMBA KWA JINA LA YESU KRISTO SEHEMU YA KWANZA

https://www.facebook.com/MaxShimbaMinistry/videos/843400799142857/
Kila Mkristo anapenda awe na maisha ya maombi yaliyo na mafanikio – anapenda akiomba kitu kwa Mungu ajibiwe. Lakini mara nyingi nimewasikia wakristo kadhaa wakisema wameomba jambo Fulani kwa Mungu lakini hawajajibiwa. Wengine wanapofikia hali ya namna hii, hukata tama – hata wokovu unaanza kupoa utamu wake.
Kuna sababu nyingi ambazo zimeandikwa ndani ya Biblia zinazoeleza chanzo cha kutijibiwa maombi ya watu. Sababu mojawapo ni kutokuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu – au kwa tafsiri nyingine kuomba kinyume na maagizo ya Mungu (Yohana 5:14-15)
Yesu Kristo alituachia maagizo mbalimbali juu ya maombi katika kulitumia Jina lake – mojawapo ni hili;
Tumuombe Baba kwa jina la Yesu Kristo.
Katika kitabu cha Yohana 16:23-24; Yesu Kristo alisema; “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.”
Wazo la kwanza tunalopata katika agizo hili ni kuelekeza mawazo na maombi yetu kwa baba Yetu aliye mbinguni wala si kwa malaika wala kwa wanadamu. Ndiyo maana imeandikwa; “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (Waebrania 11:6)
Yesu Kristo alipokuwa anawafundisha kuomba alisema; “basi ninyi saline hivi; Baba yetu uliye mbinguni….” Jambo kubwa alilotaka wanafunzi waone ni umuhimu wa kujua na kuelekeza mawazo na maombi yao kwa BABA MUNGU. Watu wengi wamekwama kwenye maombi kwa kuwa katika mawazo yao wamewategemea sana watu katika kupata majibu ya maombi yao badala ya kumtegemea Baba Mungu.
Sisemi ni vibaya kushirikiana na watu wengine katika maombi – hapana. Bali nataka ujue kuwa hata ukiwashirikisha watu wakusaidie kuomba – wewe elekeza mawazo yako kwa Baba Mungu na kumtegemea Yeye kukujibu.
Wazo la pili tunalolipata katika maagizo ya Yesu Kristo juu ya maombi yaliyoandikwa katika (Yohana 16:23-24) ni tuombe kwa Jina lake. Hakusema tuombe kwa ajili yake au kwa niaba yake, bali alisema tuombe kwa jina lake.
“Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.” (Yohana 16:23-24)
Mara kwa mara utawasikia watu wakimaliza maombi yao kwa kusema “kwa ajili ya Yesu Kristo, amina”. Lakini sioni mahali ambapo Yesu Kristo alisema tuombe kwa ajili yake. Hebu fikiri mtu anaomba uponyaji wa tumbo halafu aombe akisema “Naomba tumbo langu lipone kwa ajili ya Yesu Kristo”. Je! Ni Yesu Kristo anayehitaji uponyaji au ni wewe?
Yesu Kristo alisema tuombe kwa Jina lake na siyo tuombe kwa ajili yake wala kwa niaba yake – kumbuka hilo kila wakati unapolitumia jina la Yesu Kristo katika maombi. Lakini kama unataka mtu apone kwa ajili ya Yesu Kristo, basi omba kwa jina la Yesu Kristo – ili Jina hili litukuzwe.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

ASILI YA UISLAM

IJUE DINI YA UISLAMU NA ASILI YAKE Na Mwalimu Eleutary H. Kobelo. Utangulizi Kwa miaka mingi waislamu duniani, wanatuhimiza sana sisi Wakris...

TRENDING NOW