Sunday, September 10, 2017

MAOMBI YA VITA YA KUTUMIA ALAMA ZA MUNGU

Image may contain: one or more people and text
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mungu. Ni lazima kujifunza neno la Mungu na kulitumia katika maisha yetu ya kila siku.
Baba neno lako katika Yer 23:29 linasema “Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? ”Nasimama sawa sawa na neno lako, na kuvunja vipande vipande kila mipango ya kishetani, miradi na kazi mbaya za adui, katika pepo nne za dunia, katika jina la Yesu.
Baba neno katika Waebrania 4:12 "linasema “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili. Nachukua mamlaka ya neno lako ambalo ni upanga na kugawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani ya kila nguvu za uchawi, kila enzi, falme, mamlaka, wakuu wa giza, mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho, mishale ya moto ya adui, maadui wa siri, maadui wanaojulikana, mapepo ya utambuzi, maadui wa ndani, na mamlaka zingine zote za adui, kwa kuwafunga na kuwatupa katika shimo milele, katika jina la Yesu, Amina.
Baba neno lako katika Yer 23:29 linasema “Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? ”. Natumia moto wa Mungu Mwenyezi, kuchoma kila kazi ya adui kama majivu. Chochote ambacho kilitumwa kwangu, kinachonifuata, kilichohamishiwa kwangu, au kwenye kitu chochote ambacho ni changu. Nazifunga, na kuzitupa katika lile ziwa la moto, sasa na hata milele, katika jina la Yesu.
Baba neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu Zaburi 119: 105. Nasimama sawa sawa na neno lako, na kutumia mwanga wako kuangaza kila mahali penye giza ambapo jua haliangazi. Naweka wazi kila matendo mabaya yanayotendeka kwenye maisha yangu, familia, watoto, fedha za nyumbani, kazi, huduma, ndoa, na yote ambayo ni yetu. Bwana nakushukuru kwa kufanya kazi za uovu wao kuwa dhaifu, zife, zifungwe na kufutwa, katika jina la Yesu.
Baba neno lako katika Yakobo 1:22-25 "linasema kwamba neno lako ni kama kioo" Natumia mamlaka ya neno lako, na kubamiza, kuangamiza vipande vipande vioo vyote vya mapepo, ambavyo adui hutumia kufuatilia maendeleo yetu, mafanikio, baraka, na yote yaliyo yetu. Naamrisha maadui, kuona shughuli zao mbaya, kushindwa, na anguko katika vioo vyao vya kipepo, katika jina la Yesu.
Baba neno lako ni kama maji ambayo yatusafisha dhambi zote na uovu. Waefeso 5:26-27. Natumia maji ya Bwana Mungu mwenyezi kuwazamisha maadui, mafarao wote, mayezebeli, goliati na maadui wengine wote wa maendeleo yetu katika bahari Shamu, sawa sawa na Kutoka sura ya 15
Baba neno lako linaniambia katika Zaburi 107:20 "Kwamba neno ni kama dawa" Nasimama sawa sawa na neno lako ambalo ni kama dawa, na kuponya mioyo yetu na machungu yote, uponyaji wa kimwili, kiakili, kihisia, na kiroho. Naomba neno lako liturejeshee mara mia moja, kila kitu tulichopoteza, katika jina la Yesu
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

2 comments:

Unknown said...

Barikiwa sana kwa kazi yako

Unknown said...

Amina. Nimebarikiwa sana na Maombi haya yamebadilisha Maisha yangu

MUHAMMAD ALITABIRI KUWA, ATAKAPO KUFA, MASWAHABA WAKE WATAUKANA UISLAM NA KURUDIA UKRISTO

  MANENO YA MTUME (SAWW) YA KUWAAMBIA MASWAHABA. Bukhari katika Juzuu ya 8 Mlango wa Kauli ya Mtume (saww) katika kitabu chake ameandika: Mt...

TRENDING NOW