Posts

Showing posts from September, 2017

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

Salafist cleric says fathers can marry off their newborn daughters

Image
Last week, Egyptian Salafist preacher Muftah Mohammad Maarouf, also known as "Abu Yahya," stated that it's absolutely okay for a newborn girl to be married off by her father - even at such a young age.  Yes, you heard that right.  The statement was made during a live TV interview on a show that was discussing a controversial draft law aimed at lowering marital age in Egypt to 16.  According to the preacher, if no harm will be done to a female, then nothing should prevent her from getting married, regardless of her age.  "I am not the one saying this, in Islamic Sharia there is no set age for marriage when it comes to females," Maarouf said.  When the show's presenter pressed on with: "If this is true, then any age would be fine for marriage, 2 months, 1 year," the preacher shockingly responded:  "Even if she's just 1-day-old."  People on social media were just not having it A video of the interview that saw "Abu Yahya" drop his…

JE, UNAYO NEEMA YA YESU KRISTO, MUNGU MKUU?

Image
Nini basi maana ya neema? Watu wengi wamekuwa wakiimba ,”Neema, neema imefunuliwa” na kukariri na kuisema Neema ya Bwana (2 WAKORINTHO 13:14) kama Kasuku huku hawajui wayasemayo. Nini basi maana ya neema? Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa, bila kustahili kutokana na matendo yoyote aliyoyafanya mtu au sifa aliyonayo mtu.
Neema pia, ni uwezo wa kushinda katika tabia na utumishi wa Mungu sawasawa na mapenzi yake, tunaopewa na Mungu bila gharama yoyote au nguvuzetu au kufanyia kazi yoyote. 1. Upendeleo wa kuchaguliwa bila kustahili- Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki mbele za Mungu (WARUMI 3:20). Tangu kabisa amekuwa akimhuzunisha Mungu (MWANZO 6:5-7). Wakati wa Nuhu, watu waliangamizwa kwa Gharika. Wakati wa Musa, Mungu alitaka pia kufuta kabisa kizazi cha Wausraeli na kubaki na Musa tu kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Wakati wote, wanadamu wote wamepotoka na kuoza (WARUMI 3:12). Ni Yesu peke yake tu ambaye siku zote alifanya yanayompendeza Mungu (Y…

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA SABA)

Image
Madhara ya Kiroho unapo angalia ponografia: Ponografia husababisha madhara mabaya ya kiroho. Inaweza kuwa kizuizi kikubwa kwa mtu anayetaka kuwa na uhusiano na Mungu.* Biblia huhusianisha hamu ya ngono na tamaa na ibada ya sanamu. (Wakolosai 3:5) Mtu anayetamani kitu huwa na hamu kubwa sana ya kukipata hivi kwamba kinakuwa jambo kuu maishani mwake kuliko vitu vingine vyote. Kwa kweli, wale ambao wamezoea ponografia hutanguliza tamaa zao za ngono badala ya Mungu. Kwa hiyo wanazifanya kuwa sanamu yao. Amri ya Mungu inasema: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.”—Kutoka 20:3. Ponografia huharibu mahusiano yenye upendo. Mtume Petro, ambaye alikuwa amefunga ndoa, aliwahimiza waume Wakristo wawaheshimu wake zao. Mungu hatasikiliza sala za mume anayekosa kufanya hivyo. (1 Petro 3:7) Je, mtu anayetazama picha chafu za wanawake faraghani anamheshimu mke wake? Mke angehisije akigundua? Na Mungu ambaye “ataleta hukumuni kila kazi” na ambaye “huzipima roho” angeonaje? (Mhubiri 12:14; Mithali 16:2) …

NINI MAANA YA KUUMBWA KWA MFANO WA MUNGU?

Image
Mungu ni Roho. Je wewe ni nani? Katika somo hili la uumbaji wa binadamu, nitajibu hoja na maswali mbali mbali ambayo yanaulizwa zaidi na waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidini, kupitia wahadhiri wao wa Dini, Waislamu wamekuwa wakipinga kuwa Mungu hana Mfano kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Mwanzo Sura ya Kwanza na aya ya 26. Ndugu msomaji, nakusihi ufuatilie somo hili kwa makini ili ujue ukweli kuhusu kuumbwa kwa Binadamu kwa Mfano wa Mungu na nini maana yake: Katika siku ya mwisho ya uumbaji, Mungu alisema, "Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu" (Mwanzo 1:26). Mungu alimuumba Mtu kutoka vumbi na akampa uhai kwa kumpulizia pumzi yake mwenyewe (Mwanzo 2:07). Binadamu ni kiumbe cha kipekee ambacho Mungu alikiumba na baada ya kukiumba, akatumia pumzi yake kukipa uhai, zaidi ya hapo, binadamu ni kiumbe pekee chenye Mwili, Roho na Nafsi. Kuwa "mfano" wa Mungu maana yake, katika suala rahisi ni kwamba sisi hatufanani na Mungu katik…

ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO

Image
Kurudi nyuma na kuacha wokovu kunaitwa pia kufa kiroho (Ufunuo 3:1;Waefeso 2:1). Kwa kila aliyerudi nyuma na kuacha wokovu, hii ni saa ya kuamka usingizini na kuanza upya (Warumi 13:11-12). Lakini, je, inawezekana kuanza upya tena katika hali hii?
Ndiyo, kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Hii ni kazi yake nyingine. Roho Mtakatifu ndiye aliyemfufua Yesu, alipokufa
(Warumi 13:11). Kwa jinsi hiyo hiyo, Roho Mtakatifu anaweza kutufufua kiroho na kutupa uhai tena wa kiroho (Waefeso 2:1,4-6). Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kufufuliwa kiroho, naye atafanya. Shalom, Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

YESU ALIUMBA KILA KITU

Image
Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake (Yohana 1:3,14 ) “vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika. Naye Neno alifanyika mwili; nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli”. Yesu aitwa Neno la Mungu (Ufunuo 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(Yohana 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote. Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine.. Katika yeye vtu vyote viliumbwa (Wakolosai 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani. Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi. YESU NI MUNGU YESU ALIUMBA KILA KITU Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA NANE)

Image
Kuacha zoea la kutazama Ponografia Vipi ikiwa unapambana na zoea la kutazama ponografia? Je, kuna lolote unaloweza kufanya ili kuacha zoea hilo? Biblia hutoa tumaini! Kabla ya kumjua Kristo, baadhi ya Wakristo wa awali walikuwa waasherati, wazinzi, na wenye pupa. Hata hivyo, Paulo alisema, “lakini mmeoshwa mkawa safi.” Hilo liliwezekanaje? Paulo ajibu: “Mmetakaswa . . . kwa roho ya Mungu wetu.”—1 Wakorintho 6:9-11. Usipuuze kamwe nguvu za roho takatifu ya Mungu. “Mungu ni mwaminifu,” yasema Biblia, “naye hatawaacha nyinyi mshawishwe kupita vile mwezavyo kuhimili.” Kwa kweli, ataandaa njia ya kutokea. (1 Wakorintho 10:13) Kusali kwa bidii—kumwambia Mungu shida zako daima—kutakuwa na matokeo mazuri. Neno lake hutia moyo hivi: “Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza.”—Zaburi 55:22. Bila shaka, lazima utende kupatana na sala zako. Unahitaji kuazimia kutoka moyoni kukataa ponografia. Rafiki unayemtumaini au mshiriki wa familia anaweza kukusaidia sana, akikupa utegemezo na kitia-moyo …

ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU

Image
Kabla ya kufa kiroho, hutangulia kuzimia kiroho. Shetani hutupeleka hatua kwa hatua, kama upepo katika tairi unavyotolewa kidogo kidogo kutokana na pancha ndogo. Tukizimia kiroho, upendo wa kwanza unatoweka. Ingawa bado hatujafikia hali ya kufanya dhambi za uzinzi, uasherati, ulevi n.k kama mataifa, hata hivyo, mambo ya rohoni yanakuwa hayana mvuto kwetu kama mwanzo. Kuomba, kushuhudia, kuhudhuria ibada n.k, yanakuwa mzigo kwetu. Tunaanza kuvutwa zaidi na mambo ya dunia. Katika hali hii tunahitaji nguvu mpya, uzima mpya (Isaya 40:28-31). Anayefanya kazi hii pia ni Roho Mtakatifu, Roho wa uzima (Warumi 8:2). Pepo wa udhaifu wanatolewa kwa Roho wa Mungu (Mathayo12:28), na vivyo hivyo udhaifu wetu kiroho unatolewa na Roho wa Mungu. Je umezimia kiroho, Mwambie Roho Mtakatifu akuzindue, naye atafanya. Shalom, Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA TISA)

Image
Vijana Huuliza . . . Ninaweza kuepukaje Ponografia? ▪ Elewa ponografia ni nini? Ni mbinu ya kishetani ya kushushia heshima kitu ambacho Yehova aliumba ili kiheshimike. Kuelewa ponografia kwa njia hiyo kutakusaidia ‘kuchukia yaliyo mabaya.’—Zaburi 97:10. ▪ Fikiria madhara yake. Ponografia huharibu ndoa. Inawashushia heshima wanawake na wanaume. Inamshushia heshima mtu anayeitazama. Kwa sababu nzuri Biblia inasema: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha.” (Methali 22:3) Andika hapa chini mfano mmoja wa msiba unaoweza kukupata ukiwa na zoea la kutazama ponografia. “Mvulana mmoja shuleni kwetu alikuwa amebandika picha ya msichana aliye uchi kwenye mlango wa kabati lake. Kabati hilo lilikuwa karibu na langu.”—Robert.* “Nilikuwa nikifanya utafiti kwenye Intaneti kwa ajili ya ripoti ya shule nilipopata kituo cha ponografia.”—Annette. WAZAZI wako walipokuwa na umri kama wako, mtu aliyetaka kutazama ponografia alihitaji kuitafuta sana. Siku hizi ni kana kwamba ponografia inakutaf…

ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO

Image
Baada ya kuokolewa, tunahitaji pia kutakaswa. Bila utakaso, tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi za ndani katika mawazo, na moyoni, ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda. Dhambi za ndani , ni kama hasira, wivu ,chuki, masengenyo, kugombania ukubwa, kiburi, majivuno, kutokusamehe, kinyongo, kupenda udunia n.k. Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa: Mawazo yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23), kugombania ukubwa (Luka 22:24-26; Mathayo 20:20-22,25-28; Marko 9:30-37), hasira (Mathayo 20:24) wivu, fitina, ugomvi (Marko 9:38-39; Luka 9:49-50; 1Wakorintho 3:3-5), faraka na matengano (1Wakorintho1:10-13), umimi (Mathayo 28:6-13), kutokusamehe (Mathayo 18:21-35), chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani (Luka 9:51-56; 1Wakorintho 6:1-8); Warumi 7:15 n.k . Mambo haya huondolewa kwa utakaso. Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka (Yohana 17:14-19). Roho mtakatifu ndiye atupaye U…

ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO

Image
Katika Wagalatia 5:22-23, tunajifunza juu ya tunda la Roho. Katika lugha ya asili, yote katika mistari hii yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu, Upendo. Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu katika tabia na matendo kama furaha, amani, uvumilivu, utu wema,f adhili, imani, upole, na kiasi. Ni pale tu tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo, ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Pasipo upendo, tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao, tunakuwa si kitu. Lolote jingine tunalolifanya linakuwa halina faida (1Wakorintho 13:3). Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8) Sasa basi , ni muhimu kufahamu kwamba upendo ni tunda la Roho, tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Tukilipokea tunda hili, na kukua kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12), Kama matunda yanavyokua, ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli. Tukiwa na tunda la Roho la upendo, tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa l…

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA KWANZA)

Image
Hili ni somo linalo tatanisha na kuwewesesha watu wengi, na labda naweza hata kuhukumiwa kuwa natumia lugha chafu, la hasha. Nilazima tujifunze kila kitu, maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu. KUJICHUA NI NINI HASA? Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘masturbation’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake. Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha! Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha Unapoanza kubalehe, tamaa za ngono zinaweza kuwa zenye nguvu sana. Kwa sababu hiyo, huenda ukaangukia mazoea ya kupiga puny…

ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA.

Image
Kila Mkristo au mtu aliyeokoka, hana budi kuwa na lengo la kufikia kimo na cheo cha utimilifu wa Kristo katika tabia na Utumishi wa Mungu (Waefeso 4:11-15 ). Kufikia kiwango cha Yesu Kristo katika tabia ni jambo linalowezekana, Kama siyo, tusingetakiwa kuwa wakamilifu na watakatifu kama Baba wa mbinguni alivyo Mtakatifu (Mathayo 5:48;1`Petro 1:15-16) Neno la Mungu pia, linatufundisha uwezekano wa kuwa na viwango vya utumishi vya Yesu alipokuwa duniani, na hata kuzidi (Yohana 14:12). Hata hivyo haya yote hayawezekani kama sisi siyo waombaji kama Yesu alikuwa mwombaji namba moja. Alifanya maombi alfajiri na mapema (Marko 1:35). Alijitenga na shughuli mchana na kufanya maombi (Luka 5:15-16) Aliomba jioni (Mathayo 14:23) Wakati mwingine alifanya maombi usiku kucha (Luka 6:12). Je,sisi tunaweza kuwa waombaji kiasi hiki? Kwa nguvu na jitihada zetu hatuwezi. Tunaweza tu, tukisaidiwa na Roho Mtakatifu. Ndiyo maana tunajifunza somo hili muhimu leo katika mfululizo wa masomo haya ya Roho Mtaka…

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA PILI)

Image
CHANZO NI NINI HASA? Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii mbaya hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta ayari! Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana. Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo
mwanzo wa kutopea huko. Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.
Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo. Kama ilivyotajwa mapema, wale w…

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Image
Ili tuweze kuwa mashahidi wa Mungu,tunahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya kuokoka na kutakaswa. Ili tumtendee Mungu kazi kikamilifu, ni lazima tupokee nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 1:8;Luka 24:49). Kwa sababu hili, somo hili, ni la muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mtendakazi mzuri wa Mungu. Tutaligawa somo hili katika vipengere vinne:- A. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU B. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU C. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPA UFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU D. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU E. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA F. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU A. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU Baada ya mtu kuokolewa,inambidi kubatizwa kwa maji kwa jina la baba,Mwana na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19). Hata hivyo,huo siyo ubatizo wa mwisho.Baada ya mtu kutakaswa,anahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:11) Uba…

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA TATU)

Image
Chunguza burudani yako. Je, wewe hutazama sinema au programu za televisheni au hutembelea vituo vya Intaneti vyenye kusisimua kingono? Kwa hekima, mtunga-zaburi alisali kwa Mungu: “Uyafanye macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa.”*—Zaburi 119:37. Sali kuhusu jambo hilo. Mtunga-zaburi alisali hivi kwa Yehova: “Uyafanye macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa.” (Zaburi 119:37) Yehova Mungu anataka ufaulu, naye anaweza kukupa nguvu za kufanya yaliyo sawa!—Wafilipi 4:13. Zungumza na mtu. Mara nyingi kuchagua mtu unayeweza kumfunulia moyo wako husaidia sana kushinda zoea hilo. (Methali 17:17) Andika hapa chini jina la mtu mkomavu ambaye unaona ni rahisi kumweleza jambo hilo. ATHARI ZA KUJICHUA "PUNYETO" Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu. Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mc…

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA NNE)

Image
Mpendwa: Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke wakiwa na uvutano wenye nguvu kati yao, na hakuna ubaya wa kutosheleza tamaa za ngono katika mpango wa ndoa. Kabla ya kufunga ndoa, huenda ukawa na tamaa kali za ngono. Hilo likitokea, usidhani kwamba wewe ni mtu mwovu au kwamba huwezi kuishi maisha safi. Unaweza kudumisha usafi wa kiadili ukiamua kufanya hivyo! Lakini ili ufanikiwe, utahitaji kudhibiti mawazo yako kuhusu watu wa jinsi tofauti. Unaweza kufanya hivyo jinsi gani? Epuka kujifurahisha kwa mambo machafu. Bila shaka, haimaanishi kwamba sinema zote, au miziki yote ni mibaya. Hata hivyo, katika ulimwengu wa leo burudani nyingi zimekusudiwa kuamsha tamaa zisizofaa za ngono. Biblia inatoa shauri gani? “Acheni tujisafishe wenyewe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.” (2 Wakorintho 7:1) Epuka kabisa burudani zote zinazoweza kuchochea tamaa zisizofaa za ngono. UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo hu…