Tuesday, August 1, 2017

YESU ANAITWA MUNGU NA KUSUJUDIWA

Image may contain: one or more people and text


Katika Waebrania 1:8 twasoma, “Lakini kwa habari za Mwana, asema, kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele. Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili”
Ukianza mstari wa tano utaona kuwa anayeongea ni Mungu Baba. Anapofika mstari wa 8 anamtaja Mwana kuwa Mungu! Ni nani na asimame anayeweza kukanusha na kusema Yesu siyo Mungu?
Yesu ni Mungu!!! Isitoshe, tazama katika Ufunuo 19:10 ambapo malaika anamwelekeza Yohana kuwa anayestahili kusujudiwa ni Mungu lakini twaona ya kuwa Yesu alisujudiwa na hajawahi
kukataa!
Mathayo 2:11 “Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia;”
Mathayo 14:33 Nao walipokuwa ndani ya chombo Wakamsujudia”
Mathayo 28:9 “Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia, wakamshika miguu, wakamsujudia;”
Luka 24:52 “ Wakamwabudu; Kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu”
Yohana 9:38 “Akasema, Naamini, Bwana, Akamsujudia”
Yesu hajawahi kuwakemea watu waliokuwa wanamsujudia au kumwabudu!!! Kama Yesu siyo Mungu, na angejua kuwa siyo Mungu, angewaambia watu wasimsujudie/kumwabudu kama
malaika katika ufunuo alivyomwambia Yohana.
YESU NI MUNGU.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

MSIBAA HUU, SANAMU YA NDAMA "NG'OMBE" WA DHAHABU KWENYE QURAN ALIKOROMA MOOOO MOOOO KAMA NG'OMBE ALIE HAI

Katika Kurani, tunapata mchwa wanaozungumza kwenye Sura 27:18-19, tazama mazungumzo ya Suleiman na ndege wa Hoopoe kwenye Sura 27:20-28 na h...

TRENDING NOW