SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

UNAJUA KWANINI ALLAH ALIUMBA UGONJWA WA HOMA?

Image may contain: 1 person, closeup


SOMA MAAJABU MAKUBWA YA ALLAH KUHUSU HOMA YA SIKU MOJA.
Katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu kilichoandikwa na Sheikh Said Moosa Mohammed al-Kindy wa Muscat Oman. Juzuu 3-4 uk 74 hadith na 924 inasema 
“Homa ni bahati ya kila Muislamu kwa (adhabu ya) moto. Na homa ya siku moja inafuta (madhambi ya) mwaka (mmoja) kamili.
Nikisema hii dini ni ya kutengeneza mnabisha, lakini leo mtaelewa kuwa hakuna dini hapa bali ni usanii mtupu.
Mimi nawauliza Waislam, kama homa ya Siku moja inakufutia madhambi ya mwaka mzima Je, homa ya wiki moja mnafutiwa dhambi za miaka mingapi?
Mwiba Huondoa Dhambi:
Katika Sahih Bukhari na Muslim juzuu ya 7 Hadith 544
“ Hadith ya Aisha (r.a), mke wa mtume (SAW) alisema mtume wa Allah amesema “Hakuna tatizo litakalompata Muislamu isipokuwa Allah atafuta madhambi kwa tatizo hilo kwake, hata kama ni mwiba utakaomtoboa” (al lu’lu war-marjan vol.3 H.1663 UK.969)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Comments

TRENDING NOW

OMBA MAOMBI HAYA KILA SIKU ASUBUHI, MCHANA NA USIKU

MAOMBI YA KUMTEKETEZA SHETANI "NGUVU ZA GIZA"

MAOMBI YA VITA YA KUTUMIA ALAMA ZA MUNGU

NANI KAMPA UTUME NA UNABII MTUME MUHAMMAD?