Tuesday, August 1, 2017

DHAMBI ZILIZOSABABISHA KIFO CHA MOHAMMAD (SEHEMU YA 5 NA YA MWISHO)

No automatic alt text available.


Huu ni muendelezo wa sehemu ya 1, 2, 3 na 4 unaohitimisha makala hii. Inahusu maswali yenye maantiki yatokanayo na tukio nzima linalozunguka kusumiwa, kuugua na kufa kwa Mohammad.
1. Ikiwa Mohammad alikuwa mtume wa kweli wa Mungu, kwanini hakutambua ile sumu kabla ya kuila?
2. Kama unaamini kuwa ilikuwa mapenzi ya Mungu Mohammad kula ile sumu, pamoja na Bishir, kwanini basi Mohammad alijaribu kujiponya? Hata malaika Jibril alimwombea apone, lakini Allah hakujibu yale maombi vilevile.
3. Kwanini Jibril hakujua mapenzi ya Allah? Kulikuwa na maana gani ya Jibril kumswalia Mohammad apone wakati Allah alishaamua afe?
4. Kwanini muda mchache kabla ya kifo chake, Mohammad alitamka laana juu ya Wayahudi na Wakristo? Je, haingekuwa bora kwa yeye kuwaombea mwongozo na msamaha kwa Allah? Hii pia inaashiria wivu, maombi ya uchungu kwa kutoponywa na Allah. Mohammad aliwaombea watu laana badala ya kuwaombea msamaha kwa Allah.
TATHMINI:
Mohammad hakuwa mtume wa kweli, alikuwa mtume wa uongo. Alikufa kwasababu ya kula sumu ambayo hakuwa na taarifa kuihusu. Nyama ya mbuzi iliyotiwa sumu ‘ilichelewa kuongea naye’ wakati akiwa ameshaila. Ni wakati tu alipogundua anakufa ndipo alitabiri kifo chake.
Musa wa Biblia alijua kuhusu kifo chake (Kumbukumbu La Torati 34:1-5). Yesu Kristo vilevile alitabiri kifo chake (Marko 8:32, 32). Ilhali, Mohammad aliachwa gizani kuhusu kifo chake hadi alipogundua dakika za mwisho kuwa alikuwa anakufa.
Mtume Paulo aliumwa na nyoka (Matendo 28:1-6), lakini hakuugua au kudhurika na hiyo sumu. Mkono wa Mungu ulimlinda mtume Paulo hadi alipomaliza kazi aliyoitiwa kuikamilisha. Mohammad alikufa ghafla kama kwamba kulikuwa na machafuko na mgogoro kuhusu nani atachukuwa nafasi ya Mohammad kama kiongozi wa Waislamu. Hadi leo, sehemu ya huo mgogoro umesalia. Dunia ya Waislamu imegawanyika (Shia na Sunni) kwasababu ya hili. Iweje Allah anayechukia mgawanyiko kwenye Ummah asingemnusuru Mohammad asife ilmuradi tu kuwe na umoja na amani huku mrithi wa Mohammad akiandaliwa?
Yesu Kristo alitabiri kuwa manabii wa uongo watakuja duniani na kuwapoteza wengi (Mathayo 24:24). Mohammad ni mojawapo ya hao manabii wa uongo. Yesu na Musa walimfahamu Mungu/Yahweh uso kwa uso, Mohammad alisikia tu ‘roho’ au ‘malaika’ aitwaye ‘Jibril’ akiongea naye. Hatimaye, hata haya maombi ya Jibril hayakujibiwa na Allah. Je, yawezekana kuwa huyu ‘Jibril’ alikuwa akihubiri dini ya uongo (Wagalatia 1:8) kwa Mohammad? Je, yawezekana Jibril alikuwa Shetani au Ibilisi akijifanya kuwa malaika?
***ALIYE NA MACHO NA AONE; ALIYE NA MASIKIO NA ASIKIE; ALIYE NA HEKIMA NA ABAINI HAYA***

No comments:

MSIBAA HUU, SANAMU YA NDAMA "NG'OMBE" WA DHAHABU KWENYE QURAN ALIKOROMA MOOOO MOOOO KAMA NG'OMBE ALIE HAI

Katika Kurani, tunapata mchwa wanaozungumza kwenye Sura 27:18-19, tazama mazungumzo ya Suleiman na ndege wa Hoopoe kwenye Sura 27:20-28 na h...

TRENDING NOW