Friday, July 14, 2017

MPENDWA SIMAMA IMARA KATIKA KWELI NAYO KWELI ITAKUWEKA HURU

Image may contain: 1 person, textKisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno Yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.’
Yohana 8:31-32
Inawezekana umechoka na unaogopa kusema jambo fulani kwasababu unaogopa, ndugu zako au jamaa zako au waumini wa imani yako watasema nini. Hakika inatisha na kutetemesha akili unapokuwa katika njia panda ya namna hiyo.
Kukaa na hiyo siri kunaweza kukusababishia mambo mabaya zaidi na kufungua milango mibaya ya shetani maishani mwako. Basi usiogope kusema kweli, maana hata kama watakucheka na kukusimanga, wewe utakuwa huru na moyoni mwako utakuwa na imani.
Basi simama imara leo na mshirikishe jambo nduguyo au muumini mwenzako na sema yote, omba nae na amini kuwa umesha wekwa huru.
HAKIKA Yesu anataka kukuweka huru hii leo. Basi sema kweli nayo kweli itakuweka huru.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

Does Allah Need Help?

  In the Qur’an, the same Allah asks for help… 47:7 O you who believe ! if you help (the cause of) Allah, He will help you and make firm you...

TRENDING NOW