Tuesday, January 10, 2017

ALLAH ATHIBITISHA KUWA MAIMAMU, MASHEHE NA USTAADH NI VIONGOZI BANDIA

Image may contain: one or more people, meme and text


1. ALLAH HAKUWATAJA KWENYE QURAN
2. KUMBE MAIMAMU, MASHEHE NA USTAADHI NI VIONGOZI BANDI NA FAKE.
Ndugu msomaji,
Tukisema kuwa Uislam ni bandia, ndugu zetu wanakuja na madai kuwa tunasema uongo na maneno mengi yasio na hata ushahid wa aya.
Leo ningependa kuwauliza Waislam.
1. Wapi katika Quran Allah kasema Uislam uwe na Ma-Imamu, Mashehe na Maustaadhi?
2. Tupeni sifa za Imamu kwa kutumia aya za Quran.
3. Tupeni sifa za Mashehe kwa kutumia aya za Quran.
4. Tupeni sifa za Ustaadh kwa kutumia aya za Quran.
Ningependa ndugu Waislam watupe aya moja kwa moja. Mimi leo hii sina muda wa ngonjera zisizo na aya. Watuletee aya. Mimi nataka kusilimu.
Waislam wanasema eti hii aya kwenye Surat Al Baqara inazungumzia Imam: 124. Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. Link: http://www.quranitukufu.net/002.html
Hapo kwenye hiyo aya hakuna cha Imamu wala Shehe zaidi ya Allah kudai anampa uongozi Ibrahimu.
Mkishindwa kutuletea aya kutoka Quran zinaso sema kuwa muwe na hao viongozi wenu wa dini, basi ifahamike kuwa Uislam ni dini ya bandia na kujitungia wenyewe.
Lakini tunapo soma Biblia iliyo kamilika tunapewa aya kuhusu viongozi wa Kanisa. Ngoja niweka aya chache ili kusaidia mada:
SIFA ZA WAANGALIZI WA KANISA
Bwana alikuwa wazi sana katika neno lake kuhusu jinsi Yeye anataka kanisa lake duniani kwa lipangwe na kusimamiwa. Kwanza, Kristo ni kichwa cha kanisa na mamlaka yake makuu (Waefeso 1:22; 4:15, Wakolosai 1:18). Pili, kanisa lenyewe linafaa kujitawala, liko huru kutoka mamlaka yoyote ya nje au udhibiti, na haki ya kujitawala na uhuru kutokana na kuingiliwa na uongozi wowote wa watu binafsi au mashirika (Tito 1:5). Tatu, kanisa linastahili kutawaliwa na viongozi wa kiroho likiwa na ofisi mbili kuu - wazee na mashemasi.
MA-ASKOFU NA WACHUNGAJI

1 Timotheo 3: 1 Hili ni neno kweli, kwamba mtu akitamani kazi ya askofu, atamani kazi nzuri. 2 Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi,
anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. 3 Asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha. 4 Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia. 5 (Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu?) 6 Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya Shetani. 7 Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.
MASHEMASI
Sifa Za Mashemasi
8 Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali. 9 Inawapasa kushikamana sana na ile siri ya imani kwa dhamiri safi. 10 Ni lazima wapimwe kwanza, kisha kama hakuna neno dhidi yao, basi na waruhusiwe kuhudumu kama mashemasi. 11 Vivyo hivyo wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasiozungumza maneno ya kuwadhuru wengine, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo. 12 Shemasi awe mume wa mke mmoja na inampasa aweze kusimamia watoto wake na watu wa nyumbani mwake vema. 13 Wale ambao wamehudumu vema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Kristo Yesu.
USHAHID ZAIDI: Tito (1:1-4), Tito (1:5—3:11) na Tito (2:11-15)
Ndugu msomaji, nimethibitisha kwa aya kuwa Wakristo wao hawajajitungia vitu bali kuna aya zinazo ongoza jinsi ya kupata hawa viongozi, lakini kwenye Quran na Uislam, hatuoni aya yeyote ile inasema kuwa Waislam wawe na Maimam au Shehe au Ustaadhi na wawe watu wa aina gani.
Mimi leo ningependa Waislamu watuambie, kwanini wana Imamu, Shehe Ustaadh kwenye dini yao/ Hakika Uislam ni dini iliyo jaa shaka na MSIBA mkubwa sana kwa Muhammad.
Nawakaribisha Waislam waje kwenye Ukristo na wokovu wa kweli.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

ETI, ALLAH KAUMBA MATUNDA DUME NA MATUNDA JIKE

Jenda za Matunda? Inahitaji muujiza kuamini katika hili ... Hivi majuzi, niligundua "muujiza mwingine wa kisayansi" katika Qur'...

TRENDING NOW