Saturday, December 17, 2016

KWANINI YESU ALIKUFA MSALABANI?

Image may contain: text
i. Mungu Baba alipanga kifo cha Yesu Msalabani.
ii. Yesu alikufa ili kwa ajili ya dhambi zako.
“Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya agano la milele
alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji
Mkuu wa kondoo, awafanye ninyi wakamilifu mkiwa
mmekamilishwa katika kila jambo jeama ili mpate kutenda
mapenzi Yake, ili atende ndani yetu kile kinachompendeza
machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una Yeye
milele na milele” (Waebrania 13:20-21).
Mungu Baba alipanga kifo cha Bwana Yesu na pia alipanga
kufufuka kwake. Hii ndiyo sababu Biblia inasema kwamba
Mungu alimleta tena kutoka kwa wafu “Kwa damu ya Agano la
milele” (Waebrania 13:20-21).
“Damu ya Agano la milele” inamaanisha damu ya Yesu Kristo. Yesu alisema, “Hii ndiyo damu yangu ya agano” (Mathayo 26:28). Biblia inatufundisha kwamba ili Yesu atuokoe ilimbidi akufe na afufuke. Yesu hangefufuka, basi hatungeokolewa. Kifo cha Bwana Yesu Kristo kilileta msamaha wa dhambi, kuoshwa kwa dhambi na wokovu kwa watu wa Mungu. Kufufuka kwa Yesu Kristo lilikuwa ni dhihirisho kwamba Mungu Baba amekubali dhabihu yake ya kifo msalabani.
Wakati Yesu alikufa msalabani alijitoa kuwa sadaka kwa watu wake ili awalipie fidia ya dhambi zao. Wakati Mungu Baba alimfufua kutoka kwa wafu lilikuwa dhihirisho kwamba Mungu alifurahishwa na kifo cha Yesu. Mungu Baba alikuwa anasema kwamba kifo cha Yesu kimetosheleza fidia ya dhambi za watu wake.
Biblia inasema, “Kama Kristo hajafufuka, imani yenu ni batili, nanyi bado mko katika dhambi zenu” (1 Wakorintho 15:17). Hii inamaanisha kwamba kufufuka kwa Yesu Kristo lilikuwa hakikisho kwamba Mungu Baba alikubali kifo cha Yesu Kristo kama malipo yanayokubalika kulipia dhambi za watu wake. Yesu hangefufuka kutoka kwa wafu basi kifo chake hakingemfaidi yeyote. Ni baada tu ya kufufuka ndipo angeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwa dhambi zao.
Biblia inasema, “Kristo alifufuka kutoka wafu kwa utukufu wa Baba” (Warumi 6:4). Tukija kwa Yesu Kristo kwa imani na kumwamini yeye pekee kwa wokovu, basi dhambi zetu zitaondolewa na tutasamehewa na kupewa wokovu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

MATOLEO 20 TOFAUTI YA QURAN

MATOLEO 20 TOFAUTI YA QURAN ::::::::20 VERSIONS OF QURAN:::::::::: Je, Kati ya haya Matolea 20 (Ishirini) ya Quran, toleo lipi ni la kweli? ...

TRENDING NOW