Thursday, November 17, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA KWANZA)


Kwenye hili somo tutajifunza kuhusu Kitabu cha Daniel kwa kutumia maswali na majibu. Tutazipitia aya zote na sura zote katika Daniel. Sasa tulia na tuanze kujifunza Neno la Mungu.
SWALI:
Kwenye Danieli, kitabu hiki kiliandikwa nini?
Kitabu cha Danieli kinaelekea kuandikwa muda mfupi baada ya matukio kutokea, kwenye karne ya 6KK, kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1324. Vijana wengi wa Kiyahudi walipelekwa uhamishoni Babeli mwaka 605 KK, na wafafanuzi wengine wa vitabu vya Biblia wanakadiria kuwa Danieli alikuwa na miaka kama 16 hivi. Makadirio haya yanamfanya Danieli awe na umri wa miaka 85 wakati Waajemi walipoiteka Babeli.
Kitabu chenye kutia shaka kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.596 kinadai kuwa Danieli inaweza kuwa iliandikwa mwishoni mwa mwaka 165 KK. Hata hivyo, mwana historia wa Kiyahudi Josephus kwenye Antiquities of the Jews 11.8.5 (karibu mwaka 93-94 BK) anarekodi kuwa wakati Alexanda Mkuu alipoikaribia Yerusalemu (karibu mwaka 333 KK), Kuhani Mkuu Jaddua alikutana naye na alimwonyesha sehemu ya kitabu cha Danieli isemayo kuwa Wagiriki watawashinda Waajemi. Alexanda anaelekea kuwa alipendezwa na maneno haya, na aliachana na Wayahudi.
Origen (mwaka 225-254 BK) alisema kuwa wakati Alexanda wa Macedon alipokwenda Yerusalemu, kuhani mkuu wa Kiyahudi, alikutana naye akiwa amevaa joho lake takatifu. Alexanda aliinama mbele zake, akisema kuwa alimwona mtu mwenye joho kama hilo kwenye ndoto aliyoota, akimfahamisha kuwa anapaswa kuishinda Asia yote. Origen Against Celsus, kitabu cha 4, sura ya 50, uk.565.
SWALI:
Je Kitabu cha Danieli kiliandikwa kwenye karne ya pili (baada ya ushindi wa Alexanda), kwa sababu ya maneno ya Kigiriki yaliyopo kwenye Danieli?
Hapana. Ingawa kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.597 kinadai, "sehemu nyingine za lugha zisizoeleweka kwa urahisi zilizotumiwa zinaonyesha kipindi cha Kigiriki tofauti na kile cha uhamisho wa Babeli", kuna maneno matatu tu ya Kigiriki kwenye Kitabu cha Daniel, ambayo ni kidogo kuliko maneno saba ya Kiajemi yaliyomo. Yafuatazo ni maelezo zaidi ya mambo haya mawili.
Maneno matatu tu ya Kigiriki yapo kwenye Kitabu cha Danieli (Dan 3:5, 10, 15), na yote hayo matatu ni majina ya vifaa vya muziki. Hata hivyo, jambo hili halionyeshi kuwa kitabu hiki kiliandikwa kwenye karne ya pili (2 KK), kama maandishi ya Kiashuri yanavyosema kuwa mateka wa Kigiriki walikuwa Mesopotamia kwenye karne ya 8 KK. Isitoshe, kwenye karne ya 7 KK, mshairi wa Kigiriki, Alcaeus wa Lebos, anasema kuwa kaka yake alikuwa kwenye jeshi la Babeli. Vivyo hivyo, The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.247 pia inasema, "Hakuna shaka kuwa majina ya vifaa (vya muziki) kwenye Kitabu cha Danieli yalikuwa na sifa za Kiajemi, na yalifanya na Wagiriki kuwa sehemu ya utamaduni wao na kufanyiwa mabadiliko machache ya kitahajia (herufi). Kwa hiyo, hoja hii ni ya muhimu tena katika kutathmini uandishi wa Danieli."
Maneno sita na nusu ya Kiajemi yaliyomo kwenye Kitabu cha Danieli yanaongelea utawala (Dan 6:1-4, 6-7), na yaliacha kutumika karne moja baada ya Himaya ya Kiajemi kuchukuliwa na Alexanda Mkuu. Kama 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.193 inavyosema, ". . . Utumiaji sahihi wa Danieli wa maneno haya hauwezi kuelezwa endapo mwandishi alikuwa hafahamiki kwenye karne ya pili na hakufahamu undani wa serikali ya Kiajemi miaka mia tatu kabla ya muda alioishi." (Neno satrap [maliwali] linahesabiwa kuwa nusu, kwa sababu lilikuwa neno la Kimidiani, ambalo baadaye lilichukuliwa na Waajemi pia.
SWALI:
Je Kitabu cha Danieli kiliandikwa baada ya Kitabu cha Sirach, kwani Sirach 47-49 ina orodha ndefu kiasi ya Agano la Kale, isipokuwa Danieli, kama Asimov’s Guide to the Bible, uk.623 inavyosema?
Utawala wa Wamakabia haukuanza hadi mwaka 165 KK. Hata hivyo, kuna mambo manne yenye kutoa ushahidi unaotofautiana na nadharia hii ya karne ya pili.
1. Kwenye Apokrifa (vitabu vya kubuniwa vya dini ya Kiyahudi), 1 Maccabees 2:49-60 inawataja Danieli na vijana wengine watatu kwa namna ambayo inaashiria kuwa Kitabu cha Danieli kilikuwa tayari kimeishaandikwa. Vinginevyo, wasomaji wa 1 Maccabees wangewezaje kumwelewa Danieli na vijana wengine watatu?
2. Wataalamu wa elimukale wamekadiria muda hati ya kale yenye maandiko ya Kitabu cha Danieli ilipoandikwa kuwa ni mwaka 120 KK. Wycliffe Bible Dictionary, uk.436-438 inalitaja jambo hili, ikisema kuwa "linaibua swali kuhusu muda unaodaiwa kitabu cha Maccabean kuandikwa."
3. Uchimbuaji ulifanyika Babeli unaonyesha kuwa maelezo ya Danieli ni sahihi. M. Lenormant anasema, "Kwa kadri maandishi ya kikabari yanavyozidi kufahamika ndivyo haja ya kurekebisha shutuma zilizofanywa kwa haraka na shule ya ufafanuzi wa maandiko ya Ujerumani dhidi ya Kitabu cha Danieli inavyoongezeka" (La Magie, uk.14; nukuu ya 1001 Bible Questions Answered, uk.367).
4. Pia marejeo ya Josephus yaliyokwishatolewa kwenye swali lililotangulia.
USIKOSE SEHEMU YA PILI "Kwenye Kitabu cha Danieli, kuna vitu gani vinavyofanana na sehemu nyingine za Biblia?"
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Shalom

No comments:

Does Allah Need Help?

  In the Qur’an, the same Allah asks for help… 47:7 O you who believe ! if you help (the cause of) Allah, He will help you and make firm you...

TRENDING NOW