Wednesday, November 16, 2016

IBADA YA VIATU NA SHUTUMA ZA WAISLAMU KWA WAKRISTO


“IBADA YA VIATU NA SHUTUMA ZA WAISLAMU KWA WAKRISTO”
Kumekuwepo na shutuma nyingi sana kutoka kwa jirani zenu walio kushoto (Waislamu) wakitushutumu sisi Wakristo kwa kuingia kwetu Ibadani hali ya kuwa tumevaa Viatu, wakati wao wanapoenda kuswali msikitini, huingia bila viatu, kuonesha kwamba wao ndiyo wenye kufanya Ibada sahihi kuliko watu wa imani zingine zote Ulimwenguni, shutuma hizo huambatanishwa na baadhi ya maandiko ndani ya Biblia, ambayo kwa sehemu kubwa sana yametumika kuwasilimisha Wakristo (Kuwaingiza kwenye uislamu) wakidhani kwamba, kuingia kwao huko wataenda kufanya Ibada sahihi inayodhaniwa na jamaa zetu waislamu, ibada ya kuvua Viatu, maandiko ambayo huyatumia ni haya:
Kutoka 3:4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Yoshua 5:15 Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.
Mandiko haya ndiyo ambayo huwafanya waislamu wavue viatu vyao msikitini, hata wengine kuzifunga YEBO YEBO, au Kandambili zao kwa kutumia kamba, au Kufuri, ili tu kuzuia wezi wasiwezi kuiba yebo yebo zao, hata kama zimetoboka, na maandiko hayo pia yametumika kuwasilimisha Wakristo wengi bila wao kujua kuwa walipotoshwa, sasa fuatana nami katika somo hili ili uweze kujifunza juu ya Ibada hii ya kusali na Viatu, au kusali bila viatu:
1. MUSA NA KUVUA VIATU KATIKA NCHI TAKATIFU
Musu huyu yeye mwanzo alilelewa katika ngome ya Farao, baada ya kunusurika kuuawa akiwa mdogo,wenzie Waebarania ambao walikuwa wanatumikishwa, alijisikia vibaya kuona wakiteswa wakati yeye anaishi vizuri, siku moja baada ya kumona Mmisri mmoja anampiga nduguye Mwebrania, ikabidi Musa amuue Yule Mmisri
Kutoka 2:11 Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake.
12 Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga.
Baada ya kumuua huyo Mmisri, habari zile zikawafikia Waebrania wengine bila Musa kujua kama taarifa zile zimeshaenea, siku moja walipokuwa wanagombana Waebrania wao kwa wao, Mussa akaona siyo vema, akaenda kuwaamulia, mmoja wao akadhani Mussa anataka kumuua.
Kutoka 2:13 Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako?
14 Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana.
15 Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.

Kitendo kile cha Musa kumuua Mmisri, kilipomfikia Farao, akaazimia kumuua Musa, ikabidi Mussa akimbie kwenda Midiani, ambako huko alikaa miaka 40, yaani alipokimbilia kule alikuwa na miaka 40, alipotokewa na Mungu alikuwa na miaka 80, sasa Ile dhambi ya kuua, ikawa bado imo ndani yake hajaitubu, Mungu alikuwa na mpango na Mussa kwa ajili ya kumtumia kuwatoa Wana wa Israel kutoka Mikononi mwa Farao, kwa hivyo akaamua kumtokea Musa wakati ambao alikuwa anachunga Mifugo ya Yethro Mkwewe,
Kutoka 3: 1 Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
*HAPO MUSA AMESEMA NITAGEUKA SASA NIYAONE MAONO HAYA, KUNA KITU CHA KUTAFAKARI, YEYE ALIONA KIJITI KINAWAKA NA HAKITEKETEI, SASA IWEJE ASEME TENA KUWA ATAGEUKA AYAONE MAONO HAYO, WAKATI AMEONA KIJITI KINAWAKA MOTO? HAPO MUSA ANAIONDOA AKILI YAKE YA KAWAIDA, NA KUINGIA ROHONI ILI AWEZE KUJUA NINI KUSUDI HILO LA KIJITI KUWAKA MOTO BILA KUTEKEKEA*
4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Hapo Tafisri ya kiroho kwa habari ya Musa kuambiwa avue Viatu, ni kutubu dhambi ambayo aliifanya ya kumuua mtu na kisha kukimbia, kwani dhambi haikimbiwi, bali dhambi, inatubiwa, ili kudhihirisha kuwa, viatu vile siyo halisi kama ambavyo waislamu hudhani, Mungu anamwambia Musa avue viatu vyake miguuni, maana Nchi hiyo aliyosimama ni Nchi Takatifu, unapozzungumza habari ya Nchi, maana YAKE ni aridhi kwa tafsiri ya kawaida, sasa aridhi yote takatifu, hakuambiwa sehemu uliyosimama, la bali Nchi, sasa kama ni viatu vya kawaida, Musa alivivua na kuviweka wapi ambako si patakatifu? Maana Nchi yote ni Takatifu, Na pia kama Nchi ile ilikusudiwa aridhi, kama ambavyo waislamu hudhani, Je Ile mifugo ambayo Musa alikuwa akiichunga, haikuwa ikinya katika Nchi hiyo Takatifu? Mavi yale ya wanayama yakiwekwa Mskitini, waislamu wanaweza kusali juu yake? Hawatayaondoa sehemu yao ya kufanyia ibada wanayo dhani kuwa takatifu? Je Mungu angependa Mussa afanye Ibada katika Nchi Takatifu ambayo imejaa mavi ya wanyama? Ni sehemu gani Mungu alimwamuru Musa ayakazoe mavi ya wale wanyama aliokuwa akiwachunga kwa sababu ni Nchi Takatifu? Au ni sehemu gani ambako kunaonesha kuwa Musa alivua viatu vyake mara baada ya kuambiwa? Kwa hivyo ni lazima ulitafakari andiko hilo kiroho, Musa aliambiwa ajitakase, ajisafishe dhambi zake, Ili Mungu apate kusema nae, Mungu aweze kumtumia katika kazi zake, na si kufanya Ibada ya kuvua viatu, ndiyo maana Musa hakufanya Ibada yo yote baada ya kuambiwa avue viatu.
2. YOSHUA NA KUAMBIWA KUVUA VIATU
Yoshua nae kadhalika alipoambiwa na Malaika avue viatu vyake, haikuwa na maana halisi kama ambavyo waislamu wanachukulia, Kibiblia siyo kila neno vua lina maana hiyo, bali kuna kuwa na maana nyingine kabisa tofauti, mfano mzuri huu hapa.
Yoshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?
Kama Ikiwa kila neno vua lina maana hiyo ya kutoa kitu halisi, sasa Yoshua alipovua macho yake, Alitumia Bisibisi kuyang’oa? Alipoyavua alitazama kwa kutumia nini meno au?
Ayubu 2:11 Basi ikawa hao rafikize Ayubu watatu walipopata habari ya mabaya hayo yote yaliyomfikilia, wakaja kila mtu kutoka mahali pake; nao ni Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi; wakapatana pamoja ili waende kumlilia Ayubu na kumtuliza moyo.
12 Basi walipovua macho yao, nao wakali mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho yake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni.
Hapo rafikize Ayubu wameyavua macho yao, kwa tafsiri ya kimwili tuseme waliyang’oa? Maana Waislamu hupenda kuyafasiri sana maandiko kimwili.
Yeremia 4:4 Jitahirini kwa Bwana, mkaziondoe govi za mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
MUNGU anasema, tuzitahiri govi za mioyo yetu, sasa swali la kujiuliza, ikiwa tunajua kuwa kutahiri ni kuondoa nyama ya uume, sasa iliposemwa kutahiri Govi ya mioyo, Je tuchukue Mkasi na nyembe, tuweze kupunguza mioyo yetu?
Hili linatakiwa liwe ni jambo la kutafakariwa na jamaa zeu waislamu, kwani Wao katika imani yao, wameruhusiwa kusali na viatau, sasa kabla sijaenda kuwaangalia kina Musa katika Ibada zao Waliruhusiwa kufanya Ibada na Viatu halisi? Je sisi Wakristo kusali na Viatu tunakosea? Kwanza nirejee kwenye Uislamu, tuangalie Je wao wana ruhusiwa kusalia na Viatu?
MUHAMMAD ASALI NA VIATU
Ukisoma kitabu cha Al-u-lu wal-marjan Uk. 179
14. Mlango:
Ruhusa ya kusali na Viatu.
325. Hadithi ya Anas Bin Malik (R.a) kutoka kwa Said Bin Yazid Al-Azid (r.a) amesema, Nilimuuliza Anas Bin Malik (r.a) “Hivi Mtume (s.a.w) alisali huku amevaa viatu vyake?” Akanijibu, “Ndiyo” (Bukhari, Hadithi N. 383, Juzuu ya 1)
Hapo tunamuona Muhammad akisali na Viatu, na mlango hapo umesema, Ruhusa ya kusali na Viatu, maana yake waislamu hapo wameruhusiwa kusali na Viatu, pia haikuishia hapo, Muhammad akasema tena kuwaambia Waislamu.
Ukisoma kitabu kinachoitwa “TAFSIRI YA BULUGH AL-MARAM MIN JAM’I ADILLATIL AHKAM
Ukurasa wa 101 Hadithi Na. 171
Abu Said (r.a) amesimulia: Mtume (S.a.w) amesema: “Ye yote miongoni mwenu atakapoenda msikitini kusali, basi atizame, akiona uchafu au najisi katika viatu vyake aondoe kisha aswali navyo”. Abu Dawud Ibnu Khuzaimah ameipa daraja ya Sahih.
*Murad wa kutwaharisha viatu:
Iwapo mtu amekanyaga najisi kwa kiatu, atakitwaharisha kwa kusugua chini mchangani*
Hapo kwa mtu mwenye akili zake timilifu, hawezi kukomaa na kuanza kuwalaumu Wakristo, eti kwa nini wana Sali na viatu? Wakati Muhammad mwenyewe, alisali huku amevaa viatu, na pia akawaambia waislamu wanapoenda kusali, basi watazame viatu vyao kama kuna najisi, basi wavisugue chini mchangani, labda waislamu watuambie wao kusali na viatu, ni Uviviu wa kusugua viatu mchangani? Au mazingira yao wanayoishi hayana mchanga?
Tena Muhammad akakazia zaidi kuhusu Viatu, aliponukuliwa katika Hadithi hii.
Kasema Mtume (S.a.w) “Atakaepata (ona) nge nae anasali, basi amuue kwa kiatu cha kushoto” (Mkweli Mwaminifu, Juzuu ya 1-2, Hadithi Na. 188, Uk, 88)
Muhammad anawataka Waislamu wakimuona Nge basi wamuue kwa kiatu cha kushoto, sasa jiulize, wewe umevua viatu, unaswali peku peku (kama bata) Halafu amekatiza nge, unaweza kweli kumkanyaga kwa mguu? Nachoweza kusema ni uvivu tu wa waislamu katika kusugua mchangani viatu vyao vilivyo na najisi, kwani wameshapewa ruhusa ya kusali navyo.
TUREJEE KWA KINA MUSA NA UHALISIA WA KUSALI NA VIATU:
Musa baada ya kupewa sheria na Mungu, namna gani wataweza kumfanyia Mungu Ibada, ibada ya Pasaka, Mungu aliwataka waifanye hali ya kuwa wamevaa viatu halisi Miguuni mwao.
Kutoka 12:11 Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana.
Achilia mbali, Ibada hiyo ya Pasaka, Ibada zote ambazo Wana wa Israeli walizifanya, Hawakuwahi kuvua viatu vyao kwa kuagizwa, bali walifanya Ibada viatu vyao vikiwa miguuni mwao, kwa ushahidi wa Kauli ya Mungu mwenyewe.
Kumbukumbu la Torati 29:5 Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.
Miaka 40 Viatu vyao miguuni havikuchaa, na hakuna sehemu hata moja ambayo Mungu alimwamuru Musa kuwaambia Wana wa Israeli kuvua viatu, kama kuna mwenye ushahidi huo basi ana ruhusiwa kuutoa ushahidi huo, Sisi Wakristo, hatufungwi na Sheria ya Viatu, kwamba eti ni ili Ibada zetu ziwe sawa ni lazima tuvue Viatu, laa, Sisi tunaingia na Viatu, kwa ushahidi huu.
Kwanza Yesu mwenyewe alikuwa na viatu
Luka 3:16 Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto;
Hakuna sehemu hata moja ambayo Yesu katika Ibada zake aliwahi kuvua Viatu, kama angekuwa anavua na kututaka sisi tuvue, tungevua, lakini maadam hakufanya hivyo, wala hakutuambia sisi tuvue, basi hatufungwi na sheria hiyo, Mtu yupo huru, akiwa na Viatu, ruksa kusali navyo, kama mtu hana viatu pia hazuiliwi kusali, maana dhambi haikai kwenye kiatu, bali dhambi inakaa kwa mwenye kuvaa viatu, kwa hivyo kuwa na kiatu hakikuondolei dhambi, wala kutokuwa na viatu, hakukuondolei dhambi ulizo nazo,,,
Ila pengine waislamu wanaweza kutaka aya ambayo imetuka tuingie katika Jengo la Kanisa tukiwa na viatu, maana maelezo tu hayawatoshi, acha niwape.
Muhubiri 5:1 Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
Maandiko yanasema, Jitunze Mguu wako uingiapo Nyumbani mwa MUNGU sasa hiyo nyumba ya Mungu ni ipi?
1 Timotheo 3:15 Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Kanisa ndo nyumba ya Mungu alie hai, sasa tumeambiwa tujitunze mguu wetu tunapoingia kwenye hiyo nyumba ya Mungu, sasa tuna utunzaje mguu wetu tuingiapo nyumbani mwa Mungu?
Yeremia 2:25 Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu; lakini wewe ulisema, Hapana matumaini kabisa; la, maana nimewapenda wageni, nami nitawafuata.
Kwa hivyo sisi tunavaa viatu kwa ajili ya kujizua na mambo mengi, wewe fikiria, mtu kavaa viatu vyake, akifika njeya jingo anavua, viatu vingine vinanuka hatari, unataajia nini kwa afya za watu? Kama Waislamu wameamua kushirikia msimamo wao wa kuvua viatu kuwa ndiyo njia sahihi, basi na matako yao pia nayo yawe wazi kama walivyokuwa hawa wenzao
Isaya 24:4 vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.
Kwa hivyo wao hawana tofauti na wafungwa hao, kikubwa tu na wao wanapovua Viatu, basi matako yao pia yawe wazi kama wafungwa wenzao hao,, ila sisi tupo huru, kusali na Viatu.
Somo Hili limetayarishwa na Abel Suleiman Shiriwa

No comments:

Does Allah Need Help?

  In the Qur’an, the same Allah asks for help… 47:7 O you who believe ! if you help (the cause of) Allah, He will help you and make firm you...

TRENDING NOW