Posts

Showing posts from August, 2016

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

Je, Kanisa ni Kiti cha Enzi cha Shetani?

Image
Biblia inasema: “Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani…” (Ufunuo 2:13)

Waislamu “WAHUBIRI WA BIBLIA”, kama kawaida ya “injili” yao potofu hawaachi kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka; lakini kama hawataki kutubu, hukumu yao inakimbia mbio kuwajilia. Wahubiri hawa hutumia andiko hilo hapo juu kuonyesha eti Kanisani ni mahali akaapo shetani, wakimaanisha kuwa Wakristo wote tunapoenda kuabudu Kanisa, basi tunakuwa kwa shetani!
Lakini andiko hili maana yake ni nini?

Maneno haya yamo kwenye ujumbe wa Bwana Yesu kwa Kanisa la Pergamo. Kwa kuwa Bwana Yesu anatoa ujumbe kwa Makanisa kadhaa, hebu tuanzie nyuma kidogo ili tuweze kuona MUKTADHA wa matumizi ya maneno haya kwa usahihi. Siku zote nasisitiza umuhimu wa kuangalia maandiko katika MUKTADHA wake kwa kuwa bila kufanya hivyo, utadanganywa, utadanganywa tu na watumishi wa shetani na roho yako itaangamia milele!!
Mstari wa nane wa sura ya pili ya Ufunuo unasema: “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo anen…

Urithi wa Uislamu kutoka kwenye dini za kipagani za Uarabuni – Sehemu ya 2

Image
Ka’aba
Katika sehemu ya 1 ya makala haya tuliangalia kuhusu asili ya Allah. Katika sehemu hii ya 2 tutaongelea kuhusiana na mji wa Makka na ka'aba, ambayo ni madhabahu kuu ya Uislamu.

Mji wa Makka ndio kitovu cha Uislamu duniani. Kwenye mji huu ndiko iliko Ka’aba, au kama wanavyoamini na kuiita Waislamu Bait – ul- Haram; au Bait – ul- Allah, yaani ‘nyumba ya Allah’ au ‘nyumba ya Mungu’. Na kila Mwislamu kokote duniani anatakiwa kuswali swala 5 kila siku huku akielekeza uso wake Makka iliko hiyo nyumba ya Mungu wao. Vilevile, kila mmoja wao anatakiwa kwenda Makka kuhiji walau mara moja katika maisha yake, maana hija ni moja ya nguzo kuu katika Uislamu. Kwa maana nyingine, Ka’aba ndiyo madhabahu kuu katika Uislamu.


Ka’aba ni nyumba ya umbo la takriban mchemraba ambayo, pamoja na vitu vingine vichache iliyo navyo, kuna kipande cheusi cha jiwe ambacho kimejengewa ukutani kwenye kona mojawapo. Hivyo, Waislamu wanapoenda Makka kuhiji huzunguka Ka’aba na pia kulibusu  jiwe hilo, au kuligusa…

Je, Nafsi tatu zaweza kuwa Mungu mmoja?

Hili ni swali nyeti sana na huenda ndilo msingi wa sababu hasa za baadhi ya watu katika ulimwengu wa dini kupinga fundisho hili la kweli la Kibiblia juu ya Utatu Mtakatifu na Uuungu wa Bwana Yesu. Hoja kubwa katika sehemu hii inaonekana kuwa ni ya kimahesabu zaidi ambapo jamii ya wale wanaopinga utatu mtakatifu hudai kuwa haiwezekeni Baba, Mwana na Roho mtakatifu yaani mamlaka tatu kuwa Mungu mmoja. Yaani hiyo ni sawa na kusema 1 + 1 + 1 = 3 na siyo 1’ kwa hiyo Baba + Mwana + Roho Mtakatifu = Miungu watatu. 
Kwa mtazamo huu ninalazimika katika sehemu hii kushughulika na dhana ya kimahesabu zaidi ili kuona kama madai hayo ni sahihi na kama yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa kifarsafa katika maandiko. Katika kulipatia swala hili ufumbuzi ni vyema tukaongozwa na mtazamo wa kimaandiko kupitia fungu la kitabu cha ISaya… 
Isaya 55:8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana Hiyo ni tahadhari ya msingi sana katika kushughulika na mada hii, Mungu mwenyewe katika ki…

ETI BIBLIA INATAJA MASHEHE KWAHIYO INAUNGA MKONO UISLAM, THUBUTU

Image
Wahubiri wa ‘injili potofu’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha Quran kupitia Biblia. Nasema ‘kuhaha’ kwa sababu hakika kabisa wana juhudi kubwa mno lakini inasikitisha kwa sababu hakuna hata siku moja waliyowahi kusema jambo lenye ukweli kibiblia linalounga mkono quran kama wasemavyo wao – Mungu ni shahidi yangu. Mara waseme Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia; mara waseme Yesu aliposema kuwa ataletwa Msaidizi basi alimaanisha Muhammad, n.k. Ni kituko kimoja baada ya kingine. Na wanayemdanganya ni wao wenyewe pamoja na Wakristo wachache wasiojua Biblia. Kwa msingi huohuo, wanasema eti Biblia imewataja Mashehe; na kwa hiyo kwao huo ni ushahidi kuwa uislamu ulikuwapo tangu zamani. Acha ninukuu hoja ya mmoja wao kama ilivyo, kuhusiana na suala hili, kisha kama kawaida, utaona jinsi hoja hiyo inavyosambaratika mbele za nuru ya Kristo, yaani neno lake. Mtu huyu anasema:
"Swali kwenu nyinyi ambao hamjabahatika kuwa waislam, yaani Wakristo. Kama uislam uliletwa na muhammad s.a.w,…

QURAN SIO MANENO YA ALLAH WALA MWENYEZI MUNGU

Image
Ndugu msomaji, Huu ni MSIBA mkubwa sana kwa Waislam wote duniani. Waislam wamekuwa na tabia ya kusema kuwa, eti Quran yote ni maneno ya Allah. Unapo wauliza, huyo Allah aliwezaje ongea na Muhammad, wanabakia kimya na kuanza kukutukana. Zaidi ya hapo, leo nitawawekea ushahid tosha kuwa Quran sio maneno ya Allah. Haya ungana nani kwa ushahidi: SHETANI ANASEMA KWENYE QURAN
Surah Al Hijr 39. Shetani akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote, Kwenye Surat Al Hijr, tumesoma kuwa Shetani ndie anazungumza katika hiyo aya ya 39. Kumbe basi, Shetani ni msemaji ndani ya Qurani. HAPA TUNASOMA KUWA ZAKARIA NA YEYE NI MZUNGUMZAJI KATIKA QURAN
Surat Maryam: Zakaria Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe. Waislam, hivi Quran ni maneno ya nani? Endelea kupata darasa hapa: MARYAM NA YEYE NI MSEMAJI KATIKA QURAN
S…

JINA LA ISA BIN MARYAM HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA AU KUPONYA MAGONJWA

Image
SHALOM TENA, Kwa mara nyingine twamshukuru Yehova Mungu kwa kutupa neema hii tena ili tuweze kukufikishia ujumbe huu wa Biblia na kweli zake. Kwa muda wa miaka mingi sana pia duniani pote imekuwa ni kawaida kuwasikia waislamu wakifundisha watu wao na kuwadanganya bila ya wao kujuwa ao wengine wakiwa wanakijuwa wanachokifanya kuwa ISA bin Maryam’ Kama Qurani inavyofundisha ndiye “YESU KRISTO”. Mafundisho haya hivi sasa yanaendeshwa kwa kulinganisha aya za Biblia na Qurani. Ma sheihk, ma Imam na wahubiri wengi wa dini ya kiislamu wanaendesha mihadhara kwa uwingi duniani. Wahadhiri hao pia hutumia mbinu zingine mbali-mbali kama majarida na kurekodi kanda za audio na video, ambazo zimesababisha baadhi ya wakristo nusu au wakristo wajinga waamini kuwa Isa Bin Maryamu ndiye Yesu Kristo. Swali la msingi kwa wakristo wote;Je, ni kweli Isa bin Maryam ndiye Yesu Kristo? Katika hadithi Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu namba 1, Hadithi namba 104 ukurasa 64 “Hadithi ya Ibn Abbas kutoka kwa Mtume (s.a.…

KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS? (SEHEMU YA PILI)

Image
Mwalimu Chaka KUHITILAFIANA NA INJILI TAKATIFU
Kuna ushahidi mwingi kwamba Mwandishi wa Injili ya Barnaba alikuwa hana uhusiano wowote na Mitume wa Kristo, au wanafunzi wake ambao waliandika vitabu vyao wakiongozwa na Roho Mtakatifu. 1.Ushahidi wa kwanza ni kutokufahamu kwa mwandishi JIOGRAFIA ya Palestina ambayo ndiyo nchi na kitovu cha masimulizi ya kidini. Anasema, “Yesu akaenda kando ya ziwa Galilaya na akapanda mashua kusafiri hadi Nazareti, mji wake mwenyewe. Kukawa na dhoruba kubwa na mashua ilikuwa karibu kuzama” (Sura ya 20:1-2). Ni vizuri kujua kwamba Nazareti iko juu ya mlima wa Galilaya, wala sio mji wa pwani, kama mwandishi anavyosema. 2. Mahali pengine anasema, “Kumbuka kwamba Mungu aliamua kuharibu Ninawi kwa sababu hapakuwa na mmoja katika mji huo ambaye alikuwa mcha Mungu. Yeye (Yona) alijaribu kutoroka Tarso, kwa kuwa na hofu ya watu, lakini Mungu akamtupa baharini na samaki akammeza na kumtupa nje karibu Ninawi” (BARNABA Sura 63:4-7). Ni jambo lanalojulikana kwamba …

KWANINI ALLAH ALITEREMSHA SURATUL HIJR AYA 6 NAKUSEMA KUWA NABII WA WAISLAM NI MWENDAWAZIMU?

Ndugu zanguni, Biblia inasema kuwa, mtawafahamu kwa matunda yao, hayo yalikuwa maneno kutoka Injili ya [Mathayo 7:16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya]. Mtume Muhammad alishindwa kuonyesha uadilifu katika kazi yake. Kazi aliyo dai katumwa na Mungu, ilijaa maswali mengi ambayo yaliwafanya watu wamuite yeye, Muhammad, “Mwendawazimu”. Kitendo cha Mtume kuoa Mtoto wa miaka 6, kulileta kizungumkuti, kwasabau kitendo hicho si cha kibinadamu na hakikufanywa na Mitume walio kuja kabla yake. Hapa chini ni aya kutoka Koran iliyo teremshwa na mungu wa Islam kupitia msaada wa Gibril. Quran 15: 6. Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu. http://www.quranitukufu.net/015.html Muhammad anaitwa mwendawazimu mbele ya kadamnasi. Hayo madai ya uwendawazimu hayakukataliwa na mtume wa Allah. Alicho fanya Muhammad ni kukaa kimya, jam…

USHUHUDA WA MUISLAMU ALIYEOKOKA ALIKUWA NA MAJINI YA CHUMA ULETE SASA NI MWINJILISTI, COSMAS JUMA HAMIS

Image
Mimi Mwinjilisti Cosmas Juma Hamis nimezaliwa mwaka 1975 Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora nikiwa ni mtoto wa kwanza wa mama Mwamini Said Ntembela na Baba Shekh Juma Hamis Mdaki, Baba akiwa msumbwa na mkazi wa Wilaya mpya ya Kaliua na Mama mwenyeji wa tarafa ya Usoke wilaya Urambo akiwa ni wa kabila la watusi wazawa wa mkoa Tabora. Mwaka 1985 nikiwa na umri wa miaka 10 nilianza elimu ya msingi katika shule ya msingi mapinduzi iliyoko tarafa ya Usoke wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora pamoja na kuanza elimu ya msingi pia nilijiunga na shule ya kiislamu (yaani nilijiunga na shule ya kiislamu (madrasat) kusoma elimu ya kiislamu na hii ilitokana na Baba yangu na Mama yangu kuwa ni waislamu hivyo nilipelekwa katika madrtasa hiyo ili nisome uislam ambao ndio dini ya wazazi wangu na ndugu zangu wote. Nikiwa ni mzaliwa wa kwanza kati ya watoto 12 katika tumbo la mama yangu Mwamini Said Ntembela ambapo mimi kwa Baba tumezaliwa watoto 2 mimi na dada yangu Johari Juma Hamis na mimi nikiitwa wakati ul…

KWANINI JINA LA ALLAH HALINA UWEZO WA KUPONYA MAGONJWA?

KWANINI HAKUNA NGUVU YA UPONYAJI KATIKA UISLAM? MBONA KATIKA UKRISTO WATU WANAPONA KWA JINA LA YESU? 1. KWANINI JINA LA ALLAH HALINA UWEZO WA KUPONYA MAGONJWA? 2. ALLAH ASHINDWA KUMPONYA MUHAMMAD 3. MAOMBI YA JIBRIL YAGONGA MWAMBA 4. LAKINI JINA LA YESU LINAPONYA MAGONJWA YOTE 5. JE, UMESHA WAI ONA KUNA MKUTANO WA UPONYAJI KATIKA USILAM? Ndugu msomaji, Uponyaji ni nini? Ni tendo la kiimani la kupokea uzima katika roho au mwili kwa njia ya kuombewa,kuwekewa mikono au kulisikia neno sahihi la Kristo Yesu. Tendo hili la kiimani humletea mwamini uzima wa kiroho na afya ya kimwili pale ilipopunguka,kumbuka~wengi walipoponywa udhaifu wa miili yao,waliponywa pia na roho zao. Hivyobasi, kwanini Allah alipo mtuma Jibril kwenda kumuombea uponyaji Mtume wake Muhammad kwa ugonjwa uliosababishwa na kula sumu, maombi yao hayakufanya kazi? Hivyo basi, uponyaji haufanywi na mtu awaye yoyote yule isipokuwa Mungu. Hata madaktari bingwa wao hawaponyi bali hutoa tiba tu, mwenye kuponya ni Mungu. Watumis…

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUKIRI KUWA MUHAMMAD ALIKUWA HAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA

HUU NI MSIBA MKUBWA SANA Je, kuna uhashihidi wowote ule wa aya kusaidia madai ya kuto kujua kusoma kwa Muhammad katika Quran? Wanadhuoni wa Kiislam, hupenda kusema kuwa, Nabii wa Allah wao, aitwaye Muhammad alikuwa ameelimika, lakini unapo wauliza maswali na kuomba ushahidi wa madai yao, huwa wanaanza kukutishia na kusema kuwa, Muhammad ndie nabii wa mwisho, na kukwepa swali, la msingi. Je, Muhammad alikuwa anajua kusoma na kuandika? Hebu tuanze moja kwa moja na aya ambazo ziliteremshwa na Allah kwa kupitia msaidizi wake Malaika Jibril kama Quran inavyo dai. Ushahidi wa Kwanza:
Koran Surat Al A'raaf [7:157]
Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii Muhammad, asiye soma wala kuandika, Ndugu wasomaji, aya tuliyo isoma katika Surat Al A'raaf 157 inatuambia kuwa Nabii pekee wa Allah, Muhammad, alikuwa ngumbaru; hakufahamu kusoma wala kuandika.
Najua waislam, wataanza kubisha na kutupa maneno ya hapa na pale. Ili kuwanyamazisha tusoma ushihidi mwingine kutoka Quran yao. Ushahidi wa P…

UPO WAPI UTHIBITISHO WA AYA KUWA MUHAMMAD ALITAIRIWA?

KUMBE MTUME MUHAMMAD HAKUTAIRIWA. Ndugu msomaji, KATIKA sehemu nyingi za ulimwengu, watoto wa kiume wanatahiriwa kwa sababu za kiafya. Watu fulani katika nyakati za zamani, kama vile Wamisri, walitahiriwa, yaani, walikatwa magovi ya kiungo chao cha kiume. Yesu alitahiriwa. Kwa mujibu wa Agano la Kale, mapokeo haya yalianzia na Mtume Ibrahimu, Katika Mwanzo 17:10-13, imeandikwa, “Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na nyinyi. Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako. Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa na fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele. Katika Injili kwa mujibu wa Luka 2:21: “Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama …

POSA SABA (7) ZA MUHAMMAD ZILIZO KATALIWA

1. Kwanini baadhi ya wanawake walikataa posa za Muhammad?
2. Kwanini muhammad aliendelea kuomba/toa posa na huku zikikataliwa?
Ndugu msomaji, Leo nitakua ushahid kadhaa kuonyesha jinsi Muhammad alivyo penda wanawake lakini wengine walikataa posa zake na kuto jali utume wake alio pewa na Mkewe. Muhammad alimwomba amuoe Ghaziyyah kwa sababu ya uzuri wake, lakini alikataliwa. Tabari anadai kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu lakini hatoi ushahidi. al-Tabari juzuu ya 9 uk.136. Hakuna ushahidi kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu na kwamba Muhammad hakuwa makini kwa kutokumwadhibu, au kwamba hakuwa mwaminifu na Muhammad alimwadhibu. Layla aligusa bega la Muhammad tokea nyuma na kumuomba amuoe. Muhammad alikubali. Ndugu za Layla walisema, "Ni jambo baya kiasi gani ulilolifanya! Wewe u mwanamke anayejiheshimu, lakini Nabii ni mpenda wanawake. Tafuta kujitengua toka kwake." Layla alikwenda kwa Nabii na kumuomba aikane ndoa hiyo na aliafikianana na hilo [ombi]." al-Tabari juzuu ya 9 u…

MUHAMMAD ALIFANYA MAZINGAOMBWE NA KUPIGA RAMLI

Image
1. Mtume Muhammad alitumia Ndumba
2. Mtume Muhammad adai eti Nywele zake zinatibu jicho ovu.
3. Wapi katika Biblia tunasoma kuwa Manabii na Mitume wa Biblia walitumia Ndumba? Ndugu Msomaji,
Leo ningependa tusome kuhusu Muhammad na Utumiaji wa NDUMBA katika Uislam, MTUME MUHAMMAD ANATUMIA NDUMBA Muhammad alitumia ndumba [nguvu za kimazingaombwe] dhidi ya jicho ovu na wanyama jamii ya mjusi wenye sumu Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3525 uk.48. Hivi wapi tunasoma katika Taurat au Zaburi au Injir kuwa Mitume na Manabii wa kwenye Biblia walitumia NDUMBA? Hivi Allah hana uwezo wa kutibu jicho ovu au Sumu mpaka atumie NDUMBA? MUHAMMAD SASA AMPA MKE WAKE AISHA NDUMBA Muhammad alimpa ‘Aisha ndumba ili kutibu jicho ovu. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na. 5445,5447-5450 uk.1196. Hivi Ndumba ina tofauti gani na UCHAWI? Sasa hapo juu tumesoma kuwa Muhammad ametoa NDUMBA kwa mke wake kipenzi. Wapi tunasoma kuwa Manabii wa Biblia walitumia NDUMBA?
Muhammad aliamini katika jicho ovu, na kulikuwa na hi…

JE, UNAFAHAMU KWANINI AISHA MKE WA MUHAMMAD ALIZINI NA SAFWAN IBN AL MUATTAL?

Image
ZAIDI YA HAPO, KWANINI AISHA ALIKATAA KUZAA WATOTO NA MUHAMMAD? Utasikia Waislam wakijgamba, Aisha ni mama wa waaminio, ikimaanisha ni Mama wa Waislam. Swahaba wa Muhammad Amr bin Al-Aas alimuuliza Nabii wa Allah (PBUH): O, Nabii wa Allah, ni Mke yupi unampenda zaidi kuliko wake zako wat? Nabii Muhammad akamjibu "Aisha" Kama tulivyo soma hapo juu, Muhammad alimpenda Aisha zaidi ya wake zake wote. LAKINI: AISHA MWANA WA ABU BAKAR ALIFUMANIWA AKIFANYA NGONO NA SAFWAN BIN AL MUATTAL: Imesimuliwa na Ibn Hisham, na kusimuliwa na Ibn Ishaq, kuwa Aisha alifumaniwa akifanya ZINAA "ngono" na Safwan Ibn Al Muattal, mmoja wa Maswahiba wa Muhammad "Safwan incident". Haya mambo yalifanyika huko Madina na habarii ilitapakaa Madina yote na kumfanya Nabii wa Allah amrudishe Aisha kwa Wazazi wake. Ali ambaye alikuwa binamu yake wa karibu na Mume wa binti yake Fatimah, alimsihi Muhammad ampe takala Aisha ili kuficha hii aibu kubwa ya fumanizi la KUZINI. Hii ni siri kubwa …

KWANINI MUHAMMAD ALITAKA KUJINYONGA “COMMIT SUICIDE”?

Image
1. MUHAMMAD ALITAKATA KUJINYONGA
2. MUHAMMAD ALIPANDA MLIMANI NA KUJARIBU KUJIRUSHA ILI AFE
3. AISHA ASEMA MUHAMMAD ALIKUWA AMEROGWA
Ndugu msomaji, Tunaposoma Biblia tunajifunza kuwa Mungu aliwapa Unabii na Utume watu wake kwa njia ya upendo. Lakini nilipo soma vitabu vya Allah nilikutana na mambo ya ajabu sana. Bila ya kupoteza muda, ngoja niweke vitabu vyake ili na wewe ujisomee mwenyewe. Maana Waislam huwa wanadai eti nawasingizia au namzulia uongo Allah. KATIKA SAHIHI BUKHARIY TUNASOMA KUWA MUHAMMAD ALIJARIBU KUJINYONGA KWA SABABU YA HUZUNI KWENYE NYOYO YAKE: Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: Wao watanifukuza? Riwaya inaendelea kwa yanayoshangaza zaidi kuliko hayo Waraqa bin Naufal alipomkuta MTUME AKIJARIBU KUJINYONGA KWASABABU YA HUZUNI yake kwa kukatika Wahyi, kama si Jibril kumtuliza mara hii baada ya kuwa Waraqa bin Naufal akifanya hivyo. Sahihi Bukhariy J:9 uk 93 kita Ta’abiyri Swali la kujiuliza hapa ni hili: Hivi wapi tunasoma kwenye Taurat au Zaburi au Injili kuwa Mitume wa …

KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS? (SEHEMU YA TATU)

Mwalimu Chaka Leo napenda tuangalie baadhi ya mafundisho na upindaji wa maandiko ya Mungu kama tunaona katika Injili hii ya Barnaba.
Utabiri wa Ujio wa Muhammad katika Injili ya Barnaba. Katika Biblia tunasoma jinsi Yohana Mbatizaji alitangaza ujio wa Bwana Yesu: "Sasa huu ulikuwa ni ushahidi wa Yohana, Wayahudi wa Yerusalemu walipowatuma makuhani Walawi, na kumwuliza yeye ni nani. naye alikiri, wala hakukana, alikiri kwamba "Mimi siye Kristo." Nao wakamwuliza, " Ni nani basi? U Eliya wewe?" Akasema, "Mimi siye." "Je, wewe u Nabii yule? "Yeye akawajibu, "La" Basi wakamwambia, "Wewe u nani? ili tuwapelekee jibu wale waliotutuma?, Wanenaje juu ya nafsi yako?" Yohana alijibu kwa maneno ya nabii Isaya, "Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Nyoosheni njia ya Bwana.’” "... siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, "Tazama Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:19-29) Kat…

ALLAH HANA UWEZO WA KUSAMEHE DHAMBI WAISLAM WALIO KUFA

Je, Allah anao uwezo wa Kusamehe watu dhambi?
Ndugu zanguni, Leo ningependa tumuangalie Allah wa dini ya Uislam ambaye wanasema ndie Mungu wao. Je, huyu Allah anayo mamlaka ya kusamehe dhambi zote? Quran inaendelea kusema kuwa wale walio kuwa katika Umauti kamwe Allah hana uwezo wa kuwasamehe dhambi, ingawa WAISLAM bado wana utamaduni wa kuombea Maiti msamaha ili Allah aipokee roho ya marehemu. Suratul Muuminum 101. Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana. ***102. Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa. ***103. Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu. ***104. Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana. ***105. Je! Hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha? ***106. Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea. ***107. Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kwel…