Saturday, July 2, 2016

SINAGOGI SIO MSIKITI (SEHEMU YA KWANZA)
Tunazidi kuchambua HOJA ZA MIHADHARA ya Kiislamu
LEO TUANGALIE SINAGOGI!!
Kwa miaka mingi Afrika Mashariki na Kati kunakosemwa Kiswahili kumetokea mafundisho ambayo ni mapotofu sana ya kukejeli, na lengo lao hasa ni kuangusha mwili wa Yesu Kristo (Kanisa) na mafundisho yake. Na kupitia mafundisho hayo wengi wameacha imani iliyo ya kweli nakufuata imani zingine ambazo mwisho wao ni mauti. Na hawa siyo wengine bali ni wahadhiri wakiislamu. Wao hudai kuwa wanafuata mafundisho ya Bwana Yesu. Unukuu aya hii Mathayo 11:29-30 pale Yesu alisema jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapa raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Pia wanasema Yesu aliingia kwenye sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake siku ya Sabato Luka 4:16 kupitia kwa tendo hili la Yesu kwingia kwenye Sinagogi , wahadhiri hawa wanadhai jambo ili linamfanya Yesu kuitwa muislamu.
Tafadhali ndugu yangu ukitaka kujua ukweli fuatilia somo hili hadi tamati.. hii ni Sehemu ya Kwanza. Biblia ya Kiswahili katika maneno magumu imetaja kuwa Sinagogi ni msikiti wa Kiyahudu, hapa majamaa wanakesha!!
Historia ya Sinagogi:
Ukitaka kujua mtu Fulani ni lazima uangazie mambo kadha wakadha ikiwemo historia yake, pasina historia ni vigumu watu kufahamu mambo yaliyofichika. Hivyo nimeonelea kuwa ni bora sana kuangazia historia ya Sinagogi na chanzo chake.
Jambo la msingi kwanza ni kujua maana ya Sinagogi. Neno hili Sinagogi maana yake ni mahali pa watu kukutania. Sinagogi lilianzia pale wana wa Israeli walipokuwa utumwani kule Babeli kwa miaka Sabini kulinga na unabii wa Nabii Jeremia.
Jeremia 25:11-13
baadaye nitaeleza tofauti ya Sinagogi na Hekalu.
Sababu ya Wayahudi kuanzisha Sinagogi ni hizi.
• kule utumwani hawengeweza kurudi kule Yerusalemu ambapo palikuwa na Hekalu kwa minajili ya mambo ya ibaada. Kwa hivyo Wayahudi walitafuta jinzi ya kuendelesha ibaada na miandamo ya sikukuu zao.
• Kuendelesha utamaduni wao kama vile kutahiri mtoto wa kiume akiwa na siku nane kulingana na amri ya Mungu Mwanzo 17:9-12
• Ili kuzingatia sheria za Mungu kufundishana habari za torati na manabii.
Uongozi
Sinagogi lilikuwa likianzishwa na wazee wapatao saba au kumu wa kiyahudi, kila Sinagogi lilikuwa na viongozi wapatao wawili au zaidi. Na vyongozi hao huchaguliwa na wazee wa Sinagogi.
Katika karne ya Agano Jipya kulikuwepo Masinagogi mengi sana yapatao 480 ambazo zilikuwa zikiingiwa na watu wa wamataifa mbalimbali ambao walikubali kufuata taratibu zote za dini ya Kiyahudi.
Kazi ya Sinagogi:
Malengo makubwa ya sinagogi yalikuwa kujikumbusha sheria na pia kuangalia utamaduni wao. Tusomapo Biblia na kuichunguza tunaona mambo yafuatayo;
Malaki 4:4
Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliomwamuru huko Horebu kwa ajili ya watu wangu Israeli wote naam, amri ya hukumu.
Mathayo 5:17
Yesu alifundisha hivi:- Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au manabii la sikuja kutangua, bali kutimiliza
Hivyo basi kwa habari za Torati na manabii Wayahudi walikuwa wakifundisha watoto wao kwenye Sinagogi.
Matendo 15:21.
kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila Sabato katika Masinagogi.
Hapa tunaona Mtume Paulo naye anamkumbusha Timotheo habari ya mafundisho dhabiti alioyapata kutoka utotoni.
2 Timotheo 3:14-15
Baki wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; naya kuwa tangu utoto umeajua mandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Kulikuwa na masinagogi mengine yalikuwa na vyongozi zaidi ya wawili na mmoja wao alikuwa na cheo cha (Heb gr archi synagogue) au kasisi mkuu.
Kasisi huyu ilikuwa na kazi mbalimbali kwa mfano:-
• Kujenga na kutunza mali yao
• Kuangalia namna ya ibaada vile inavyofanywa ikiwemo kutunza sheria, Luka 13:10-14 nanukuu aya (14) Basi mkuu wa Sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu alimponya mtu siku ya Sabato, akamjibu, akawambia makutano, kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si siku ya Sabato.
• Kuchagua mtu mwenye kusoma na kuomba.
• Kualika wageni kutoka Masinagogi mengine ili aje awahutubie watu na kutilia nguvu mambo yanayohusu jamii na dini yao.
Matendo 13:13-15 na nukuu aya (15) kasha baada ya kusomwa Torati na Chuo cha Manabii, wakuu wa Sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwambia, Ndugu kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.
Kwenye Sinagogi kuna mtu mmoja ambaye kazi yake ni kutunza kile Chuo cha Torati Manabii na pia huangalia usafi wa Sinagogi kwa ujumla, nayeye hulipwa kwa kazi hiyo anayoifanya. Na kwa Kiebrania mtu huyu huitwa (Hazzan).
Luka 4:20
akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi na watu wote waliokuwamo katika Sinagogi wakamkazia macho.
Mtumishi huyo kazi yake nyingine ilkuwa ni kutangaza mwanzo wa Sabato na mwisho wake. Husimamia ujenzi wa Sinagogi au kurekebishwa kwake, kwa hivyo inambidi aishi kwenye Sinagogi.
Fuatilia hapo kesho majaliwa tuangazie hoja za wahendesha mihadhara kuhusu Sinagogi
Edited by Max Shimba
Amended by Max Shimba
By permission
Na Mwalimu Chaka

No comments:

THE QUR’AN CONFIRMS THE INTEGRITY OF THE BIBLE

There is a common held conviction among Muslims that the Bible has become corrupted. They believe that the Bible has been changed. Almost ev...

TRENDING NOW