Saturday, July 2, 2016

MWENYEZI MUNGU HAKUANZISHA DINI YEYOTE ILE


Mungu Mtakatifu hakuwai sema watu wawe na dini katika Taurat au Zaburi au Injili. Wala Mungu hakuwia mwambia Adam na Hawa wawe na dini. Kumbe basi dini haitoki kwa Mungu bali ni jaribio la mwanadamu kuwa na uhusiano na Mungu. Swali la kujiuliza hapa, je, Mwanadamu mwenye dhambi anawezaje kumtafuta Mungu aliye mtakatifu? Jibu ni fupi sana. Dini haiwezi kukufikisha kwa Mungu wala kukusaidia uwe na Mungu.
Tukisoma katika Taurat, au Zaburi au Injir hatusomi sehemu yeyote ile ambayo Mungu anasema kuwa watu waanzishe dini, bali tunasoma kuwa Mungu anawaambia watu wamfuate yeye.
Ndio maana nasema Mungu hana dini. Adam na Hawa hawakuwa na dini na hakuna ushahid katika Taurat iliyo kuwepo miaka maelfu kuwa Adam alikuwa na dini. http://www.chabad.org/…/How-and-When-Was-the-Torah-Written.…
Musa Hakuwa na dini na hakuna ushahidi katika Taurat kuwa Musa au Abraham walikuwa na dini.
Daudi hakuwa na dini na hakuna ushahid katika Zaburi kuwa Daudi alifuata dini na au alikuwa na dini.
Hiyo hapo juu ni mifano michache tu ya kukufungua macho kuwa Mungu hana dini na wala hakuwaambia watu waanze na au waanzishe dini.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu Baba kwa maisha yetu. Yohana 14:6. Yesu ndie Njia.
Kumbe Mungu anaita dini kuwa ni mapokeo ya mababa (Wagalatia 1:14). Na kumbe, alipomwita Paulo katika huduma, hakutaka Paulo abakie tena humo ndani ya dini. Na kwa kuwa sasa Paulo alitoka nje ya dini, alijikuta akizalisha maadui wengi sana.
Watu waliokuwa wakimpinga Bwana Yesu na wale waliompinga Paulo hawakuwa wakitetea maslahi ya kisiasa, bali walikuwa wakitetea dini yao.
Yesu anaita kwa nguvu akisema: Njoni kwangu ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. (Mt. 11.28). kwa nini anasema hivyo? Anasema: Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. (Yoh. 10:10).
Tunatakiwa kukimbilia kwa Bwana Yesu mwenyewe; si kwenye dini. Je, hakuna watu wa dini wanaoingia motoni? Jibu ni kwamba wapo. Kwa nini waende motoni na huku wana dini? Ni kwa sababu unaweza kuwa na dini lakini ukawa huna Yesu. Na hiki ndicho kinachotokea kwa watu wengi. Wengi wameridhika na kuwa na dini wasijue kwamba hilo si hasa kusudi la kuishi kwetu hapa duniani.
Lakini hakuna mtu aliye na Yesu ambaye anakwenda motoni! Bwana mwenyewe anaahidi wazi kabisa: Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. (Yoh. 10:27). Haleluya!
Dini ni mzigo juu ya mabega ya watu. Ni taratibu zilizoanzishwa na wanadamu na kuendelea kurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Mojawapo ya washika dini wazuri sana walikuwa ni mafarisayo. Kwa mfano, walikuwa wakishika kwa uaminifu sana utaratibu wa kutokula bila kunawa mikono. Kwa hiyo, siku moja walimkabili Bwana Yesu na kumwambia: Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. (Mt. 15:1).
Kumbe tunaweza tukawa tunaenda kwenye nyumba za ibada, lakini tukawa tunafundishwa maagizo ya wanadamu!! Na kwa kuyafuata hayo tunaweza kuwa tunamwabudu Mungu bure! Inatisha kama nini! Ukisikia kazi ya hasara, basi ni pamoja na hii!
Rafiki, kwenye dini kumejaa maagizo ya wanadamu. Tena msisitizo mwingi umo kwenye hayo maagizo badala ya kuwa kwenye maagizo ya Mungu.
Amka leo. Njoo kwa Yesu upokee wokovu. Hatujaitwa kutumikia dini; tumeitwa kumtumikia Bwana Yesu!
Max Shimba Ministries Org

No comments:

MTUME MUHAMMAD ALIMTAMANI MKE WA MTU

  Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka macho yake na kumtamani mke wa mtu (mwanamke aliyeolewa) (Na’uzubillah). [Tafsir Fatah al-Qadir, Juzuu ya...

TRENDING NOW