Friday, May 6, 2016

WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI?


(SEHEMU YA PILI)
Ndugu Waislam,
Asanteni kwa majibu yenu katika Sehemu ya Kwanza ya Huu Mjadala Mzito ambao mpka sasa bado hamjatoa majibu kuthibitisha lini Muhamamd alisimu, badala ya Waislam kutoonyesha wapi Muhammad Kawa mwislamu kwa hoja hii na hii wenzetu wanabaki tu kwenye Hali ya kujaribu kujibu Yale niliyokuwa naelezea pasina mwanzo kutupa somo kuonyesha wazi mwezetu huyu Hana hoja. Pili Waislam wanadai tu kuwa kwa mujibu wa Qurani 30:30 Muhammad atakuwa kazaliwa muislamu na hili pia linazua balaa kama tutakavyoona , na ndio maana nikaanza kwa kutuonyesha kuwa Babu yake ambaye alikuwa mshirikina tena alikufa katika hiyo Hali ya ujahiliwa aliwahi kumpeleka mjukuu wake Ndani ya alkaaba wakati huo ikiwa na miungu 360 ya kikafiri wakati wa swala ya alfajiri akamtia wakfu kwa dua ila kumwandaa kwa siku za usoni. Kupanga pia kafiri huyu mshirikina ndiye aliyemchagulia mjukuu wake jina sio kama jina la Yohana au Ishmael au Yesu yaliyoletwa na Malaika. Jina ili ndilo alilotumia hata baada ya kujibashiria utume.
Lakini pia tunapo soma kwenye sura ya 93: kuna maneno haya; "Naapa kwa mchana! 2. Na kwa usiku unapo tanda! 3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. 4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. 5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. 6 Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? 7. Na akakukuta umepotea akakuongoa? 8 Akakukuta mhitaji akakutosheleza? 9. Basi yatima usimwonee! ZINGATIA MANENO HAYA :::::: NA AKAKUKUTA UMEPOTEA AKAKUONGOA!!!
Hapa kwa mwenye kutaka kufahamu Kuna mazingatio. Neno ambalo mabingwa wa tafsiri ya Qurani wamelifasiri kupotea njia ni neno "Dhaallan" kwenye Aya ya saba. Tazama the noble Quran pia hivi ndivyo walifasiri kina Ibn Kathir, Jalalayneen
Pili katika Surah ya 42:52 tunasoma "Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka."
Zingatia kauli hii ULIKUWA HUJUI KITABU WALA IMANI na ndio maana allah akasema akimwambia muhammad ulikuwa umepotea njia!!!!
MASWALI:

Lakini sasa inabidi tuhoji, kama halikukuwa Haji imani wala hukusoma kitabu cha Mungu kabla ya Quran, pangoni alikuwa akifanya ibada kwa mwongozo gani? Kwa msingi wa imani gani? Ibada hii ilikuwa ya dini gani kama sio ya mababu zake?
Zaidi sana tunaelezwa kisa kimoja Muhammad alipokuwa umri wake kama miaka 35 Alkaaba ilionekana kuwa na nyufa hivyo Maqureishi wakaamua kuirekebisha na jiwe jeuzi lilipokuwa liwekwe kwenye sehemu yake pakatokea sintofahamu na tunaona wazi Muhammad akishiriki katika ibada hii ya ujenzi wa alkaaba uliokuwa ukiongoza na majahili wakati huu kumbuka bado Kuna masanamu 360 ndani mle. Na tunaona Maqureishi wakikubali uamuzi wake.
Ndio maana sasa Allah anampa Muhammad amri hii katika sura ya 6:14. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina"
Ukizingatia aya hii ni amri, Muhammad anatakiwa asilimu na atoke miongoni mwa washirikina. sasa wapi kaitii ili awe amesilimu?
Na kama je ni kweli kabla ya kupewa amri hii alikuwa miongoni mwa washirikina na kama katii amri hii alibadili jina lake alopewa na mshirikina babu yake kama wanafotakiwa waislamu wapya leo hii au alibaki na jina alopewa zama za ujahiliya?
Ama kuhusu Nabii Isaya ameandika kwamba: Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi (Isaya 29:12).
Waislamu kama Ibrahimu walipoona andiko hili wakadhani kuwa tayari wameshapata ushahidi kuwa Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia kwa kuwa Muhammad alikuwa ni mtu ambaye hakuwa amesoma.
Ukifuatilia sura nzima ya 29 na mantiki iliyozaa mstari huu wa 12, unaweza kuishia kucheka tu, ingawaje hili si jambo la kucheka.
Wanachofanya Waislamu ni upotovu mkubwa ambao unaangamiza mamilioni ya watu wa Mungu milele katika jehanamu ya moto. Watu wanaaminishwa uongo na wao wanaukumbatia kana kwamba ni ukweli.
Kwa ujumla, ukisoma sura ya 29 ni sura ambayo inatamka hukumu juu ya Ariel (Yerusalemu) kutokana na uasi wao juu ya sheria na maagizo ya Mungu, Yehova. Hebu tusome sura hiyo kwa Taratibu:
1 Ole wa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi alifanya kituo chake ndani yake; ongezeni mwaka baada ya mwaka; sikukuu na zirudi wakati wake,
2 ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli.
3 Nami nitapiga kimo juu yako pande zote, nitakuhusuru kwa ngome, nami nitajenga maboma yakuzunguke.
4 Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong'ona toka mavumbini.
5 Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula.
6 Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.
7 Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, nao wamwudhio, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.
8 Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
9 Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo.
10 Kwa maana Bwana amewamwagieni roho ya usingizi, amefumba macho yenu, yaani, manabii; amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji.
Mbali na hukumu hizo hapo juu, Mungu bado akaendelea kusema kuwa, kutokana na uasi wao, hata neno lake hawatalielewa. Yaani hawataweza kusikia au kujua Mungu anasema nini hata kama watasoma au kusikia neno lake. Hii ni pamoja na wale ambao ndio wanatarajiwa kuwa wenye kuelewa neno hili – yaani manabii na waonaji – ukiachilia mbali wale wasio na maarifa juu ya neno la Mungu, yaani watu wa kawaida. Kwa hiyo, anaendelea kusema:
11 Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri;
12 kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.
Sasa basi, kama kweli Muhammad ndiye anayetajwa kwenye Isaya 29:12, kimantiki ina maana kuwa yeye ni kati ya wasioelewa lolote kwa kuwa wako chini ya hukumu ya Mungu; maana kama tulivyoona, sura hii ni tamko la hukumu ya Mungu kutokana na uasi. Si vibaya hata hivyo! Ndiyo maana nikasema kwamba unaposoma hoja hii ya Waislamu unaweza kuishia kucheka tu.
Lakini hebu tazama CHUO hiki ni WATU humpa mtu asiye na maarifa? Sasa kama chuo hiki kinakusudiwa ni Qurani? Je Watu hawa waliompa Muhammad chuo hiki ni kina nani? hivi kumbe Quran imetoka kwa WATU wakumpa Muhammad?
Hata hivyo, kwa kuwa sasa Muhammad ni nabii asiyeelewa chochote kutokana na kuwa chini ya hukumu ya Mungu kulingana na mantiki ya andiko hili, maana yake ni kuwa ujumbe alioleta kwa wanadamu hautoki kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi. Ndiyo! Labda kama, kwa makusudi tu, hutaki mantiki iliyopo. Kwa nini basi umfuate mtu wa namna hiyo?
Kumbuka kama Muhammad kweli ni Muislamu tangu tumboni ambapo nimetoa ushahidi kuwa amekuwa na shetani wake tangu tumboni wala Waislam hawajalipinga hilo , je iweje Allah ampe muislamu amri ya kusilimu na jee wapi sasa katii amri hii na kusilimu!
Fanya maamuzi; nafsi yako ni ya gharama Mpendwa.
NDIO MAANA BADO NAULIZA WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI.
IKIWA kama KUNA MTU YEYOTE MWENYE USHAHID kuwa MUHAMMAD MWANA WA AMINA NA Bwana ABDALLAH ALIKUWA NI MUISLAMU? UWE NI USHAHIDI WA SURA, AU HADITH ALETE.
na Mwalimu Chaka
For Max Shimba Ministries Org.

No comments:

Does Allah Need Help?

  In the Qur’an, the same Allah asks for help… 47:7 O you who believe ! if you help (the cause of) Allah, He will help you and make firm you...

TRENDING NOW