Tuesday, May 24, 2016

SITAKI KUWA MUISLAM KWASABABU ALLAH ATAINGIA JEHANNAM KAMA VIUMBE VYENYE DHAMBI

Katika ulimwengu wa leo kuna njia nyingi za kutumaini. Furaha ya milele na Mbinguni vina hubiriwa kila mahali. Hata hivyo kuna dini nyingi tofauti, filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo (furaha ya milele) vinatofautiana. Na kila mmoja katika tofauti hizo za dini na filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo; anaamini ya kuwa amesimama katika ukweli.
Katika Surat Maryam, Kuruan inasema kuwa (19) 71.72. Inasema, wala hapana yoyote ila mwenye kuifikia jehanamu, maana ni wajibu wa Mola wako umekwisha kuhukumiwa, nasi tutawaokoa wale wamchao na kuwaacha madharimu hali wamepiga magoti.
ALLAH KATEREMSHA AYA NA KUSEMA =>WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM
Kuruan inakiri kuwan kila bin-adam amekwisha hukumiwa kuingia Jehannam kwa maana huo ndio wajibu wa Allah kuwaingiza watu Jihannam. Allah anaendelea kusema kuwa, yeye atawaokoa Waislam baada kuingia Jehanam. Je, haya madai ni kweli?
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.
Katika Surat Ghaafir inakiri kuwa Allah anaendelea kusema kuwa Waislam wote wataingia Jehannam. Mimi kama Mkristo siwezi kuipenda dini hii ambayo teyari mungu wake amesha toa hukumu ya kwenda Jehannam kwa wote wanao ufuata Uislam.
ALLAH KASEMA MGUU WAKE UTAISHI JEHANNAM MILELE YOTE

Zaidi ya hapo, katika Surat Maryam, Allah ameshindwa kutueleza ni kivipi atawatoa watu Jehannam, bali ameweka madai tu kuwa atakuja huko na kuwatoa Waislam.
Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 371
Imeletwa kwenu na Anas:
Nabii wa Allah alisema: Watu watatupwa katika Jihannam, na Jihannam itasema. "Je, hakuna watu zaidi wa kuingia huku Jehannam?" (50.30) Mpaka Allah atakapo weka Mguu wake Jehannam, na Jihannam itasema, Inatosha, inatosha (qat! qat!)
Katika Sahihi hadith hapo juu, tumesoma kuwa, naye Allah atauweka mguu wake Jihannam, kwasababu Jehannam bado ilikuwa inaita watu waingie huko na au labda ilikuwa bado haija jaa. Je, wapi tumesoma kuwa Allah aliutoa Mguu wake Jehannan? Wapi aya ambayo inatuambia kuwa Allah aliingia huko ili awatoe waislam ambao teyari walisha hukumia kwenda Jehannam kutokana na Surat Maryam?
Ndugu wasomaji, Njia ya kwenda Mbinguni haipitii Jehannam kama ambavyo Allah anadai kwenye surat tulizozisoma hapo juu. Jehannam haipo pembezoni mwa Mbinguni kama Allah anavyo wafundisha Waislam.
Biblia ina jibu swali hilo ikisema kamwe waliotumia njia ya motoni kutaka kutokea peponi kamwe hawataiona.
Luka 16:24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Hii aya ya Biblia inatuhakikishia kuwa, kuna sehemu mbili ambazo zitakuwa na au Walio mwabudu Mungu au wali mwabudu Shetani. Biblia haisemi kuwa wote wataingia Jehannam alafu Mungu atakuja huko Jehannam na kuchukua watu wake, la hasha.
Neno la Mungu linaendelea kusema kuwa: Mithali 16:25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Ndugu msomaji. Biblia imesha tufundisha kuwa mwisho wa njia ya Allah (Surat Maryam 72-73) ni Motoni ambako kumesemwa katika Mithali 16:25.
Ndugu zanguni, hii ni moja sababu nyingi zinazo nifanye niukatae Uislam, maana teyari umesha hukumu wafuasi wake na kuwasweka Jehannam.
Sasa, mimi kama Mkristo kwanini niupende Uislam ambayo unapeleka watu Jehannam?
Karibu kwa Yesu ambako kuna uzima wa Milele. Yohana 14: 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Na Kwa Mujibu Wa Neno La Mungu, Yesu Kristo Ndiye NJIA, Mtu Hawezi Kuja Kwa BABA Pasipo Kupitia Kwake (Yohana 14:6).
Kuna Wengi Hawajui Kuwa Yesu Ndiye Hii Njia Nyembamba Iendayo Uzimani… Hawa Akili Zao Zimetiwa GIZA Na Ibilisi (mungu wa dunia hii) Ili Isiwazukie Nuru Ya Wokovu, Wakamwamini Yesu Aliye Utukufu Wa Mungu Na Sura Ya Mungu (2 Wakorintho 4:3-4).
Hatua Ya Pili Mara Baada Ya Kujua Kuwa Yesu Ni Njia Kweli Na Uzima Na Ya Kuwa Alikufa Msalabani Kuchukua DHAMBI Na Uovu Wako, Lazima Sasa UKUBALI Ukweli Huu Moyoni Mwako, UAMINI Moyoni Na Kukiri Waziwazi Kwa Kinywa Chako Ili Uweze Kupata Wokovu Na Pia Kuhesabiwa Haki (Warumi 10:9-10).
Tunapomwamini Yesu Na Kazi Ya Msalaba, Tunachukua SHARE YETU Ya UKOMBOZI Toka Msalabani, Na Kuimilki Kisheria.
Wako Watu Wengi Wanaijua Njia [Wametimiza Hatua Ya Kwanza] Lakini Kwa Kweli Hawaja Chukua Hatua Ya KUYATOA Maisha Yao Kwa Yesu, Yaani Kuingia Kwenye Njia, Yaani KUOKOKA!
Watu Wengi Tuliomo Nao Kwenye Madhehebu Na Dini Zetu Ni Watu Ambao Wako Hatua Ya Kwanza. Lakini Lazima Uchukue Hatua Ya Pili, Uingie Kwenye Njia
“Yeye atakayenikiri mbele za watu nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye Mbinguni, bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye Mbinguni,” Mat. 10:32-33.
Yesu Kristo Mwana wa Mungu hakika ndiye, “Njia na Kweli na Uzima.” Hakuna atakaye okoka isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo. Kama ukimwamini Yesu leo na kumtii ujue ya kuwa furaha na amani na uzima vita kuwa vyako; sio katika ulimwengu huu tu, bali na katika ulimwengu ule ujao.
Hizi ndizo sababu chache kwanini nakataa kuwa Muislam.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Max Shimba Ministries Org
1633 Broadway, 30th Floor, New York, NY 10019
(C) 05/09/14 Max Shimba Ministries

No comments:

Does Allah Need Help?

  In the Qur’an, the same Allah asks for help… 47:7 O you who believe ! if you help (the cause of) Allah, He will help you and make firm you...

TRENDING NOW