Tuesday, May 24, 2016

KWANINI KWENYE QURAN HAKUNA JINA LA YEHOVA?Ndugu wasomaji,
Biblia ilikuwepo miaka 671 kabla ya Quran imetamka kuwa, Mwenyezi Mungu Jina lake ni Yehova [ يهوه yahuh]. Lakini cha ajabu, hakuna aya hata moja kwenye Quran inayo kiri kuwa Allah ni Yehova [ يهوه yahuh].
Zaburi 83: 18 Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.
Hebu tuanze kwa ushahidi wa aya kutoka Biblia takatifu:
Katika Biblia, Mungu anasema: “Mimi ni Yehova. Hilo ni jina langu.” (Isaya 42:8) Ingawa ana majina mengi ya cheo kama vile “Mungu Mweza-Yote,” “Bwana Mwenye Enzi Kuu,” na “Muumba,” anawaheshimu waabudu wake kwa kuwaalika wamwite kwa jina lake la kibinafsi.—Mwanzo 17:1; Matendo 4:24; 1 Petro 4:19.
Yehova ni tafsiri ya jina la Mungu katika Kiswahili ambayo imekuwa ikitumiwa kwa miaka mingi. Ingawa wasomi wengi hupendelea kuliandika “Yahweh,” Yehova ndilo jina linalojulikana na watu wengi zaidi na lipo kwa lugha ya Kiswhaili.
Biblia inamtaja Yehova kuwa Mungu wa Kweli, Muumba wa kila kitu. (Ufunuo 4:11), lakini kwenye Quran Allah anaogopa kujiita Yehova. Zaburi 83: 18 Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.
SASA NAWAULIZA WAISLAM:
1. Ipo wapi aya kutoka Quran ambayo Allah anaitwa Yehova?
2. Ipo wapi aya kutoka Quran ambayo Allah anathibitisha Isaya 41:8?
3. Kama Allah ni Mungu wa Adam, Ibrahim, Musa, nk. Kwanini amekataa kujitambulisha kwa jina lake la Yehova? Zaburi 83: 18 Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.
KAMA KUNA MUISLAM ATAKUJA NA AYA KUTOKA QURAN NA KUTHIBITISHA KUWA ALLAH NI YEHOVA. BASI LEO HII NITAUKANA UKRISTO WANGU NA KUWA MUISLAM. LEO MTANISILIMISHA HAPA HAPA.
Bila ya jazba wala nini, Waislam naombeni mnipe aya kutoka Quran. NATAKA KUSILIMU NA KUWA MUISLAM.
Max Shimba Ministries Org

No comments:

Does Allah Need Help?

  In the Qur’an, the same Allah asks for help… 47:7 O you who believe ! if you help (the cause of) Allah, He will help you and make firm you...

TRENDING NOW