Friday, May 13, 2016

KUMBE TWALHA ALITAMANI KUMUOA AYSHA MKE WA MUHAMMAD?

Leo katika chambuachambua yangu ya vitabu nimeamua kupitia surah nzima ya 33 katika Qurani kama ilivyofasiriwa na Wanachuoni wa Kiislamu wa awali; fuatana nami; tuanze na aya hii Qu33:53 Enyi mlioamini! msiingie nyumba za Nabii ila kama mpewe ruhusa kwenda kula, pasipo (kwenda kaa) kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni; na mnapokwisha kula, tawanyikeni. Wala msishughulike kuzungumza, maana jambo hili humwudhi Mtume, naye huwaoneeni haya; lakini Mwenyezi Mungu Haoni haya kusema haki. Nanyi mnapowaomba (wakeze) kitu, basi waombeni nyuma ya pazia. Hayo ni safi kabisa kwa mioyo yenu na kwa mioyo yao. Wala haiwapasini kumwudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala msiwaoe wake zake baada yake abadan. Hakika hilo ni (dhambi) kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu."...............................................Maneno haya tunaambiwa tuamini ni ya MUNGU tena yapo kwenye Ubao uliohifadhiwa tangu kabla ya ulimwengu kuwepo, ni maneno ya MUNGu ya milele yasiokuwa kiumbe, ila unaposoma ni wazi tu hapa ni matayarisho ya kiongozi ambaye bila shaka alifahamu siku sio chache ataaga dunia baada ya kuteseka kwa muda kwa sumu aliyolishwa na mwanamke wa Kiyahudi ambaye alikuwa na machungu ya kuuwawa kwa jamii yake kule Khaibar; zaidi sana ni yale tunayojifundisha au kugundua kuwa kama sababu ya kuteremshwa kwa aya hii; naomba kunukuu: ....... Twalha bin Ubaydullah alikuwa akimtamani Aisha (mkewe Mtume) akisema:
“Akifa Mtume nitamuoa Aisha” pale pale Mwenyeezi Mungu (s.w) akateremsha Aya ya 53 sura 33
Taz: Addurrul Manthur J.5 Uk. 404 Tafsir ibn Kathir J.3 Uk. 513
Kwa kuwa ni haramu kumwoa, mtu mama yako hata Babako akifa, basi mtume akatangaza wake zake wote ni mama zetu. Sasa leo kumwita Aysha kale katoto kalioolewa na miaka 6 kuwa ni mama ya waumini inakuwa rahisi wala watu hawashangai;
Ajabu kiongozi huyu
Alipomwoa aliyekuwa Mke wa mwanawe wa kulea Zaid ,waarabu wakaanza kumsema , ooh Mtume gani kaoa Mke wa mwanawe , maana walimwita Zaidi bin Muhammad licha ya kuwa hakuwa baba mzazi ila baba mlezi tu; kujitetea Allah akateremsha wahyi; aya inasemaje: Qu 33: 40. Muhammad si baba ya ye yote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mungu na Muhuri wa Manabii. Na Mwenyezi Mungu ndiye Ajuaye kila kitu."..........

HAPA YATUPASHA WENYE AKILI TUZITUMIE KUJIULIZA MASWALI KADHAA KABLA YA KUAMINI TU KICHWA KICHWA; YAANI kiimani Muhammad sio Baba yetu; licha ya kuwa ndiye katufundisha Dini na Ibada na ndiye kiumbe bora kwa MUNGU; Ila WAKE ZAKE ni MAMA zetu Kiimani!!!!! Are you seeing kile ninachokiona mie!!!! yaani waswahili wanasema ukiwa mwongo usiwe msaulifu...... REJEA TENA AYA ...... MUHAMMAD SIO BABA WA YEYOTE KATIKA WANAUME WENU.....hapa wanaume inakusudia kumukana Zaid ambaye kutokana na kulelewa pale nyumbani ; hata majirani na Maqureishi walimwona kuwa mmoja wa ile jamii na kumwita Zaid bin Muhammad ila babake mzazi alikuwa anaitwa Harith: sasa ili kufunika aibu ; Allah mara nyingine akateremsha aya; kumhusu Zaid, inasemaje?
Qu33:5
Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye sema kweli, naye ndiye anaye ongoa Njia.
Yaani hapa baba mtu anajitetea jamani ee; Huyu Zaid sio mwanangu haswa kama vile Qassim na Ibrahim, hivyo nikijitwalia Mke wake msiche mkanisema sana;
Allah hakufikia hapo; Aya ikateremshwa tena; inasemaje?!
Qu 33:6
Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa hamwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na rafiki zenu. Wala si lawama juu yenu kwa mlivyo kosea. Lakini ipo lawama katika yale ziliyo fanya nyoyo zenu kwa makusudi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
yaani jamni hapa wahyi unasema mwiteni Zaid bin Harith wala sio Zaid Bin Muhammad;
kumbuka WAKE ZAKE YAANI KINA ZAINABU, AYSHA, HAFSA, SAUDA, ni mama zetu kiimani!!!
Yaanio kwa Zaid, jana Zainabu alikuwa MKE WANGU; MUHAMMAD alikuwa babangu, leo MUHAMMAD SIO BABANGU TENA NA MKE WANGU SASA NI MAMA YANGU KIIMANI!!! Wacha ninikuu;
"Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni."
Sio hayo tu ila kwa kuwa jamaa kagundua wapo waume wenye nia kwa wakeze baada ya kifo chake; akaamua kuzidi kuwapa masharii mazito wakeze; naomba kunukuu;
" Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema.
wacha kuregeza sauti ;; mnatakuwa mdumu majumbani.............. " Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara" HAPA WENYE AKILI TUNATAKIWA KUJIULIZA HUU UCHAFU AMBAO Allah anawataza na kuwaondoea watu wa Nyumba ya MTUme ni uchafu upi? badala ya kujiuliza ili leo Sunni na Shia wanang'ang'ania kijua haswa NANI WANAQUALIFY kuitwa WATU WA NYUMBA YA MTUME; ila huu uchafu ndio mie naona la muhumu kujiuliza.
Sasa kwa kuwa Muhammad alijua wazi watu wanamsema kuhusiana na ili tukio la kumwoa first cousin wake ambaye alikuwa mke wa mwanae wa kulea; mara tena Allah akateremsha wahyi; unasemaje "
Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi."........ yaani hapa tunazibwa koo, tusiolize maswaliiiiii
Allah tunazidi kuambiwa eti kateremsha aya nyingine; " Na ulipo mwambia yule Mwenyezi Mungu aliye mneemesha, nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu. Na ukaficha nafsini mwako aliyo taka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea. Basi Zaid alipo kwisha haja naye tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shuruti za t'alaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.
YAANI AYA HBADO HIKO PALE PALE KWA ZAID; alipokwisha haja naye ZAINABU TULIKUOZA WEWE; YAANI Mungu ndiye kumuoza mwenyewe; baada ya kuwa Zaid kamaliza HAJA NAYEEEE; sijui hapa tunapata elimu gani, maliza haja na mwanamke yaani mkeo , mpe talaka!!! mtumie maliza haja zako, MTUME atamwoa!!!! duuu;
anazidi kujitetea mtume kwa aya nyingine; "
Hapana ubaya kwa Nabii kufanya aliyo mhalalishia Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa walio pita zamani. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyo kwisha kadiriwa. " yaani msiche mkanilaumu; hata mimi kumwoa Zainabu ni predestination , yaani jambo ambalo nilipangikwa na MUNGU zamani, yaani kudura; ........
Na Mwalimu Chaka wa Musa
Max Shimba Ministries Org.

No comments:

Does Allah Need Help?

  In the Qur’an, the same Allah asks for help… 47:7 O you who believe ! if you help (the cause of) Allah, He will help you and make firm you...

TRENDING NOW