Saturday, March 5, 2016

QURAN, ALLAH, MUHAMMAD, NA JIBRIL WANAKIRI KUWA YESU NI MUNGU KWASABABU "YESU NI NENO"

Ndugu msomaji,
Naanza kwa kunukuu Biblia:
Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!
SASA BASI, BIBLIA ILIYO KUJA KABLA YA QURAN INASEMA KUWA, YESU NI NENO, NA NENO NI MUNGU KAMA ILIVYO THIBITISHWA HAPO JUU.
JE KWEYE QURAN, ALLAH ANASEMA NINI KUHUSU ISA WA QURAN?
Qur-an Tukufu inasemaje!
Qur-anSurat al-Imran 3:45 aliposema malaika ewe Mariam Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za “neno” litokalo kwake “jina lake” ni Masihi Isa Ibn Mariam, mwenye heshma katika Dunia na akhera ………….
Andiko hilo la Qur-an linaonyesha na kufunua kwa wazi juu ya kauli ya Malaika kwa Mariam iliyomtaka kujua juu ya mamlaka inayotakiwa kukaa ndani ya tumbo lake na hapa Qur-an huitaja mamlaka hiyo kuwa ni Mwana aitwaye Isa Ibn Mariam. Lakini Qur-an hutaja mwana huyo (Isa) kama “Neno” litokalo kwake (Mungu ).
Katika maneno ya Kiarabu ni:“Kalimatu minhu” - Neno litokalo kwake (Mungu)
Katika upana wa lugha neno “kalimatu” limetumika kama kisifa kinacho mwelezea “Mtu” maana imetumika kauli ya umoja, “Kalimatu” - Neno, kwa Waarabu huita “Mufrada” yaani umoja hivyo aya haikusudii “Maneno” ya kutamkika ila ni sifa na cheo cha mtu (Isa Ibn Mariam) kama Neno katika umoja na siyo wingi (Jami-u) hivyo Isa katika Qur-an hutambuliwa kuwa na cheo au sifa iitwayo Neno kabla ya zile za kibinadamu, katika Uislam manabii mbalimbali wamepewa vyeo na sifa mfano:-
Musa huitwa - Takalama llahu………aliyeongea na Mungu
Ibrahimu - Habiba llahu ……… kipenzi cha Mungu
Lakini nabii Isa huonekana kuwa na sifa mbili ya kwanza ni ile ya kuitwa
Kalimatu llahu - Neno la Mungu
Ruh” llahu - Roho itokayo kwa Mungu
Hivyo baada ya kufahamu hilo ni vyema sasa tukaangalia na kuchunguza kwa upana juu ya sifa hii ya “Neno” Je inatueleza nini juu ya asili na mamlaka haswaa ya (Isa) kabla ya kuja hapa duniani.
Surat Al Imran 45. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).
Quran inakiri kuwa Maryam alipata MWANA KWA KUPITIA NENO LITOKALO KWA MUNGU. Hivyo basi Isa asili yane ni NENO na sio binadamu. Rejea Surat Al Imran aya 45.
JE, BIBLIA INASEMA NINI?
Baada ya kuona wazo hilo la Qur-an hebu tuone Biblia nayo inasema nini juu ya hilo?
Yohana.1: 1-3 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Katika sura na Aya hizo Biblia nayoinaeleza juu ya habari ya “Neno” (logos) pia inatupeleka mbele zaidi maana inasema kuwa huyo “Neno” (kalimatu) ni Mungu (rejea …….Yohana 1: 1-2 naye neno alikuwa Mungu) Je hii inamaana kuwa huyo Neno ni Yesu!
Na je inamaana Yesu ni Mungu kiasili?
Ndugu yangu mpendwa msomaji ukiwa ni Muislam au Mkristo yawezekana hilo likawa ndiyo swali lako. Ninakuomba kuwa makini zaidi tunapoingia sehemu hii ngumu na inayosumbua watu wengi.
Hebu kwanza tumfuatilie huyu Neno Je Biblia inasemaje juu ya Neno?
Zaburi 33:6 kwa “Neno” la Bwana Mbingu zilifanyika na Jeshi lake lote kwa Pumzi ya kinywa chake.
Biblia hapo inaonyesha kutaja tena habari ya “Neno” na huyu Neno hapo anaonekana kuwa na sifa ya kuumba, lakini ninayo imani kuwa Biblia inapotaja habari ya “Neno” bado ingali inazungumzia juu ya Mungu mmoja tu katika upana wa utendaji (Nafsi) hivyo Neno ndiye Mungu huyo.
Je Neno la Mungu ndiye Mungu huyo?
Ndiyo ni kweli ndugu msomaji wangu hebu nikupe mfano:-
Kwa kutumia kielelezo cha Neno lakawaida tunajifunza juu ya neno kama nafsi fikiri huenda ulimuudhi mtu Fulani naye kwa kughadhibika akaamua kukushitaki kwa kosa la kumtamkia “Neno” baya Swali! Je polisi watakapo kuja kukukamata watakamata “Neno” lako lililosema vibaya au utakamatwa wewe mwenyewe?
Jibu:- Niwazi kuwa utakamatwa wewe mwenyewe na hiyo ni kwasababu! Neno na mwenye Neno ni kitu kimoja.
Kielelezo hicho kinawiana fika na mamlaka ya Yesu kama Neno la Mungu huwezi kumtenganisha kiasili na mamlaka ya Uungu, yeye (Yesu) ni Neno kama nafsi (logos) ya utendaji wa Mungu, alikuwako kabla ya vyote.
Pamoja na hayo ninaamini bado unajiuliza maswali haya.
Je! Huyu Yesu ninani haswa na je vitabu vyote vya dini vina uwazi gani kuhusu Yesu kama ni Mungu, na je kweli zipo dalili na sifa za Uungu wake?
Maswali hayo ni mazuri ikiwa yapo katika fikra zako ndugu msomaji wangu mpendwa.
Kumbuka:
Mungu ufahamika kwa vigezo na sifa maalumu zinazomfanya aitwa Mungu vigezo na tabia hizo kamwe havipaswi kumhusu mwanadamu. Vinginevyo ikiwa yuko anayeonekana kuwa mwanadamu lakini vitabu halali vya Kidini yaani Qur-an na Biblia vikampa sifa za kimungu hiyo anapaswa kutazamwa upya na kwa umakini, asije akawa ni Mungu pamoja nasi (Emmanuel).
Kumbuka:
Mungu alijifunua kwenye kijiti na kusema na mtumishi wake nabii Musa (Qur-an 20:911)
Kulingana na ukuu na uweza wa Mungu huenda hilo lilikuwa ni jambo duni na lakushangaza ila Musa alipaswa tu kutambua kuwa alikutana na kuzungumza na Mungu na ndiyo sababu leo hii Musa huitwa katika Uislam.
Takalama llahu - aliyeongea na Mungu
Kubuka Musa alipoona ule moto alifikiri hata kuutumia kwa mambo binafsi lakini laajabu kumbe moto ule ulisitiri mamlaka ya Mungu aliye hitaji kuzungumza naye.
Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.
Allah anamwambia Muhammad katia Suratul Yunus aya 94 kuwa, kama Muhammad anashaka na ukweli kuwa Yesu ni Neno na Neno ni Mungu. Basi Muhammad atuulize Wakristo kuwa, Je, hayo madai ya Allah ni ya kweli? Hakika Biblia imekamilika na kusema bila ya shaka yeyote ile kuwa Yesu ni Neno na Neno alikuwa na Mungu kabla ya Mwanzo kuwepo. Allah na yeye amekiri hayo kuwa Yesu ni Neno ambalo lilikuwa na Mungu hata kabla ya Mwanzo kuwepo.
Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Yesu ni Mungu kwasababu "YESU NI NENO NA NENO NI MUNGU"
Katika huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
Copyright © Max Shimba Ministries 2016

No comments:

KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25?

  TEREHE 25 DISEMBA IMETAJWA KWENYE BIBLIA KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25? Tuanze na kumsikiliza Yesu akiitumia aya inayo husisha tarehe 25 n...

TRENDING NOW