Friday, February 5, 2016

Kwanini Mkristo anauhakika wa kwenda Paradiso zaidi ya Muislamu?

1. Je, Kurani inatoa uhakika kwa Waislamu?
Kurani inatengeneza tu mazingira ya mashaka kuhusiana na kuingia Paradiso au hapana. Muislamu hanauhakika wa kuiepuka jehanamu ya moto:
“Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo” (Kurani 17:57).
Waislamu hufikiria kwamba hawawezi kuwa na uhakika kuhusiana na kwenda Paradiso, kwa sababu Kurani inasema Mola huamua na mwanadamu hawezi kujua kwamba ameokoka:
"Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? Ni Moto mkali!" (Kurani 101:6-11).
Muislamu hana uhakika ni upande gani anaohusika nao. Mola alimuumba mwanadamu kufanya wema au uovu:
"Hujui ya kwamba Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humuadhibu amtakaye, na humsamehe amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." (Kurani 5:40).
Muislamu hajui ni nani atakuwa pamoja na Mola Paradiso. Kwa hiyo Kurani haiwezi kutoa uhakika kwa Muislamu kuhusiana na kwenda Paradiso.
2. Je, Muhammad anatoa uhakika kwa Waislamu?Kurani iko wazi kwamba Muhammad hawezi kumsaidia Muislamu kuingia Paradiso:
"Wala nasaha yangu haikufaini kitu nikitaka kukunasihini, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kukuachieni mpotee. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi; na kwake mtarejeshwa" (Kurani 11:34).
"Hata ukiwa na pupa ya kutaka kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anaye shikilia kupotea. Wala hawatapata wa kuwanusuru" (Kurani 16:37).
"Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake." (Kurani 39:44).
Kwa hiyo Kurani inakataa kwamba Muhammad aweza kuwa muwezeshaji kwa Muislamu kuingia Paradiso. Angalia pia Kurani 7:188, 4:123 na 9:80. Hivyo ni nini faida yake, ikiwa kila mwanadamu atateseka jehanamu, kabla ya wenye haki kuchaguliwa kutoka hao waendao jehanamu?
Je ni nini basi kwa habari ya Muhammad kuwa mfano kwa Waislamu kuingia Paradiso? Pia hili nalo halina mbadala kwa Muislamu, kwa sababu Muhammad aliona shaka kuhusu kuingia Paradiso:
“Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi." (Kurani 46:9).
Pia nyaraka zingine katika uislamu zinasema kwamba Muhammad hakuwa na uhakika wa kwenda Paradiso [1].
3. Are Christians sure about going to Paradise?Wakati Waislamu wanajaribu kutii sheria za Mola, wanabaki kutokuwa na uhakika wa wokovu, Mkristo anauhakika wa kwenda Paradiso. Mkristo atamjibu Muislamu juu ya swali “Bwana zangu, nifanye nini ili nipate kuokoka?” kwa [2]:
“Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka” (Matendo ya Mitume 16:31).
Ni lazima Muislamu afahamu kuokoka kwa upendo na neema ya Mungu. Uislamu hauna Mwokozi. Mwamini ndani ya Mwokozi Mkuu Yesu Kristo wakati wote anakuwa na uhakika wa kwenda Paradiso. Wokovu wa pekee kwa mwanadamu umetolewa kupitia Yesu Kristo, Neno la Mungu. Kwa sadaka ya mwenye haki Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi, mwamini ana uhakika wa kuingia Paradiso. Kuna mistari kadhaa kwenye Maandiko Matakatifu yanayothibitisha kuingia Paradiso kwa waaminikwenye utukufu wa Yesu Kristo:
“Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye Mimi hata akifa atakuwa anaishi” (Yohana 11:25).
"Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Nakwenda kuwaandalia makao. Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.Thomasi akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?" Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia Kwangu" (Yohana 14:2-6).
4. HitimishoMkristo ana uhakika wa kwenda Paradiso. Muislamu huishi na kufa, hana uhakika wa wokovu. Mkristo, kwa upande mwingine, amemkubali Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zake na ana uhakika. Hii ni habari njema kuhusu upendo na neema ya Mungu ni kitu ambacho Mkristo anataka kuwashirikisha rafiki zake wailslamu.
Rejea:
1. Sahih al-Bukhari, Volume 4, Book 51 and Volume 5, Book 58, Number 266.
2. E.M. Hicham, How Shall They Hear? Sharing your Christian faith with Muslims, Ambassador Publications, Belfast, 2009, 88.

No comments:

KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25?

  TEREHE 25 DISEMBA IMETAJWA KWENYE BIBLIA KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25? Tuanze na kumsikiliza Yesu akiitumia aya inayo husisha tarehe 25 n...

TRENDING NOW