Friday, February 19, 2016

JE, WAKRISTO WANASTAHILI KUITUNZA SIKU YA SABATO? (SEHEMU YA KWANZA)

Ndugu msomaji,
Leo tutajikumbusha kwa mara nyingine tena kama tunatakiwa kuitunza Sabato.
Sabato ilipeanwa kwa Waisraeli, si kanisa. Sabato bado ingali siku ya Jumamosi si Jumapili na haijawai badilishwa. Bali sabato ni sehemu ya sheria ya Agano La Kale na Wakristo wako huru kutoka kwa mkono wa sheria (Wagalatia 4:1-26; Warumi 6:14). Wakristo hawitakiwi kuitunza sabato hata kama iko siku ya Jumamosi au Jumapili. Siku ya kwanza ya juma, siku ya Bwana (Ufunuo 1:10) za sherekea kiumbe kipya Kristo aliyefufuka akiwa kiongozi wetu. Hatujaamrishwa kiufuata sheria ya Musa ya sabato ya kustarehe, bali tuko huru kumfuata Kristo aliyefufuka. Mtume Paulo alisema kwamba kila mkristo amue mweneyewe kama ataifuata sabato, “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe” (Warumi 14:5). Twastahili kumwabudu Mungu kila siku, si Jumamosi pekee or Jumapili pekee.
Lengo la Mungu kupeana sabato kwa Waisraeli haikuwa kukumbuka uumbaji, bali waukumbuke utumwa wa Wamisri na kule kuokolewa na Bwana. Kumbuka yanayohitajika kwa kuitunza sabato: mtu aliyewekwa chini ya hiyo sheria hangeweza kutoka kwa boma yake (Kutoka 16:29), hangewakisha moto (Kutoka 35:3), angeruhusu mtu yeyote kufanya kazi (Kumbukumbu La Torati 5:14). Mtu mwenye angivunja shreria ya sabato angeuwawa (Kutoka 31:15; Hesabu 15:32-35).
Uchunganusi wa ukurasa wa Agano Jipya watuonyesha mambo mane muimu: 1) Popote Kristo alionekena baada ya kufufuka kwake na siku zimetajwa, kila wakati ni siku ya kwanza ya Juma (Mathayo 28:1,9, 10; Mariko 16:9; Luka 24:1,13,15; Yohana 20:19, 26). 2) Wakati pekee sabato imetajwa kutoka kwa kitabu cha Matendo ya Mitume hadi ufunuo ni kwa sababu ya lengo la uinjilisti kwa Wayahudi kwenye Masinagogi (Matendo Ya Mitume 13-18). Paulo aliandika, “Nilikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi” (1 Wakorintho 9:20). Paulo hakuenda kaitka Masinagogi kuwa na ushirika na kuwajenga waumini, bali alienda ili awathibitishie injili na kuwaokoa walikuwa wamepotea. 3) Mara moja Paulo anasema, “tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa” (Matendo Ya Mitume 18:6), sabato tena haitajwi kamwe. Na 4) Badala ya kupendekeza kuwa waitunze siku ya sabato, sehemu nyingine ya Agano Jipya iliyobaki yasema kinyume ( ikijumulisha sehemu ya tatu ilioachwa nche hapo juu, inapatika katika Wakolosai 2:16).
Kwa kuingalia hoja ya nne kwa makini, tutafumbua kwamba, hakuna jukumu lolote la kuitunza sabato kwa waumini wa Agano Jipya. Pia tutaonyesha kuwa dhana ya Jumapili “Sabato ya Wakristo” si ya kibibilia. Vile imejadiliwa hapo juu, hakuna wakati sabato imetajwa baada ya Paulo kuanza kuangazia Mataifa, “Basi mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Wakolosai 2:16-17). Sabato ya Kiyahudi ilifutiliwa msalabani hamali ambapo Kristo “Akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki” (Wakolosai 2:14).
Wazo hili limerudiwa zaidi ya mara moja katika Agano Jipya: “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwinginie aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku huiadhimisha kwa Bwana” (Warumi 14:5-6a). “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika siku, na miezi, na nyaktati, na miaka” (Wagalatia 4:9-10).
Ni siku gani ya sabato, Jumamosi au Jumapili? Wakristo wastahili kuitunza hii siku?
Twastahili kumwabudu Mungu kila siku, si Jumamosi pekee or Jumapili pekee.
Mungu awabariki sana,

No comments:

KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25?

  TEREHE 25 DISEMBA IMETAJWA KWENYE BIBLIA KWANINI KRISMAS NI DISEMBA 25? Tuanze na kumsikiliza Yesu akiitumia aya inayo husisha tarehe 25 n...

TRENDING NOW