Posts

Showing posts from November, 2015

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

NAMNA YA KUMWITA,KWENDA NA KUMUOMBA MUNGU ILI AKUSIKILIZE.

Yeremia 29:12 “Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza”.
Utangulizi 

Watu wengi wamekuwa wakitamani maombi wanayoyapeleka mbele za Mungukusikilizwa.Watu wanaomba kila aina ya maombi inayowezakana maadam Mungu asikie na kuwaokoa kutoka kwenye shida waliyonayo au kuwapa haja za mioyo sawasawa na uhitaji wao.

Wapo wanaoomba na wanaona majibu yao yanajibiwa lakini pia lipo kundi jingine kubwa ambalo wanaona kama vile Mungu amenyamaza, amewaacha, hawasikii, au wanajiona kama vile Mungu amewakataa na kuziona ahadi za Mungu kwamba si za kweli na mbaya zaidi wengine wamefika mahali pa kumwacha Mungu kwa sababu ya kushindwa kuvumilia majibu kutoka kwa Mungu na hivyo kutafuta njia mbadala za kutatua matatizo yao. 

Wapo walioomba kuhusu watoto, ndoa zao, afya zao,ajira,biashara,Elimu zao nk. Walipoona katika fahamu zao Mungu hajibu basi wakaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji,wachawi na kwa miungu mingine kutafuta msaada huko.

Sasa ili Mungu aweze kusikiliza au kujibu maombi yako hue…

JIFUNZE KUMILIKI MAJIBU YA MAOMBI YAKO

Image
Yoshua 13:1-7 Utangulizi, Katika dunia ya leo watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao mwingi ikiwa ni pamoja na kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuomba Mungu awabariki, awaponye, awalinde kwa kifupi awajibu mahitaji yao waliyonayo mbele zake siku zote. Wapo waliokuwa hawazai wamezaa, vipofu wameona, wasioajiliwa wameajiliwa, biashara za wengi zimefanikiwa, ndoa nyingi Mungu ameziponya, wapo waliotaka kuolewa au kuoa na Mungu amewapa waume na wake wazuri. Sasa hao hao watu ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika kuomba Mungu awatendee miujiza katika maisha yao, imefika mahali wanaona yale ambayo yalikuwa ni majibu ya Moambi yao shetani ameyavamia na kuleta balaa zaidi na limekuwa pigo kubwa sana kwa wana wa Mungu. Na kwa sababu hiyo wamejikuta wakimlalamikia Mungu kama vile wana wa Israeli na imefika mahali pa wengine kuona kama Mungu hawezi na hivyo kumuacha. Tatizo la haya yote ni kwamba wakristo wengi hawana tabia ya au mazoea ya kumiliki mujibu ya maombi yao toka k…

NINI NI MAPENZI YA MUNGU KWA MWANADAMU?

Image
Mathayo 7:21 inasema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Naamini kabisa kama kweli wewe unahamu ya kuingia katika ufalme wa Mungu basi ni lazima utataka kujifunza yapi ni mapenzi ya Mungu kwako ili uyatende na uweze kuurithi uzima wa milele. Yesu anasema si kila mtu, sio watu, bali mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa Baba.…………kwa lugha nyepesi maana yake wapo wengi wenye kusema Bwana Bwana lakini hawataurithi ufalme wa milele kwa sababu ya kutotenda mapenzi ya Mungu. Hivyo basi kwa sababu si kila mtu, aniambiaye………….., maana yake kwa kila mtu chini ya jua kuna mapenzi ya Mungu ya kutekeleza, na mapenzi ya Mungu maana yake ni yale ambayo Mungu anataka watu wake wayatende . Sasa lengo au shabaha ya ujumbe huu ni kujibu swali letu kwamba nini ni mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu na hivyo kukupa maarifa yatakayokusaidia kuyajua mapenzi ya Mungu katika maisha yako . Baa…

KWA NINI MUNGU ANATAKA TUENENDE KWA ROHO?

Image
Ukisoma katika warumi 8:14 Biblia inasema “kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” na pia Paulo kwa wagalatia anasema” Basi nasema Enendeni kwa Roho,wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili Wagalatia 5:16. Hapa tunaona jinsi Paulo anavyosisitiza kwa makanisa ya Rumi na korinto kuhusu suala zima la kuongozwa na Roho Mtakatifu. Anawaambia warumi kwa kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu maana yake haijalishi ana umri gani, ni wa dhehebu gani, jinsia gani maadamu anaongozwa na Roho wa Mungu huyo ni mwana wa Mungu na bado anawaagiza wagalatia akisema Basi nasema enendeni kwa Roho………….. anaposema enendeni maana yake mkiongozwa na Roho, au mkimfuata Roho katika yale anayowaagiza. Maneno haya yanaonyesha zipo sababu za msingi kwa nini tunatakiwa kuongozwa na Roho sasa hapa sizungumzii kazi za Roho mtakatifu najua zipo kazi nyingi anazozifanya Roho Mtakatifu lakini mimi nazumgumzia sababu za kuongozwa na Roho Mtakatifu, ambaye ndio agano ji…

MAMBO SITA YANAYO SABABISHA MAELFU YA WATU WA AINA MBALIMBALI KUINGIA KWENYE VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA

1. Wapo waliopata watoto kwa njia za ushirikina
2. Kukubari huduma za kishirikina
3. Kuzindika nyumba
4. Matumizi ya hirizi na baadhi ya vifaa vya ushirikina
5. kuhuzuria au kuishi maeneo yenye utawala wa kipepo
6. Wengine majina yao yamewaingiza kwenye vifungo

Kwa kurithi watoto wengi wanao zaliwa kwenye familia ambazo kuna mambo ya uchawi au wanaabudu mizimu na kufanya mambo ya matambiko huwa wanatolewa kwa pepo au mizimu wangali bado wadogo kadri wanavyoendelea kukua ndivyo wanavyoendelea kuona kama mambo yanayo fanyika ni sahemu halali kwa maisha yao. Nakumbuka safari moja tukiwa kilimanjaro tulifanya huduma na kijana mmoja wa kidato cha pili aliyekuwa amefungwa na nguvu za giza , na tukiwa tunafanya nae maombi alitapika vitu fulani vyeupe vya kushangaza sana. Baada ya kufunguliwa na Bwana Yesu na yale mapepo kumuachia tukapata nafasi ya kukaa nae na kuzungumza nae, alitueleza kuwa yeye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kwenye familia yao na kuwa amekuwa akipelekwa kwenye makaburi na kufanya …

MASHAMBULIZI KUTOKA ROHO WAOVU

Image
Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, nao hawakushinda, wala mahala pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na shetani, audanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye… kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari. Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu (Ufunuo 12:7 – 12). Shetani hayuko hapa duniani kucheza. Yuko kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kwa hali na mali wewe usiingie mbinguni. Yeye anayo kazi moja tu, ya kupigana na wewe na akushinde. Yeye halali. Akikushindwa leo kesho anatafuta mbinu nyingine. Hivyo yako mashambulizi makali ya shetani, roho waovu mapepo na majini. Mtu wa Mungu huwezi kuyashinda mashambulizi ya shetani bila kujifunza mbinu zake anazozitumia na huwezi kumshinda bila ya wewe kujifunza upiga…

JE NGUVU ZA GIZA ZIPO?

Image
Wapo watu wachache ambao huwa hawaamini habari za utendaji wa nguvu za giza,. na wengine huamini kuwa wakisha okoka hawahusiki tena, na mambo yanayohusu nguvu za giza kitu ambacho si kweli, Je umeshawahi kujiuliza kwa nini Bwana Yesu kabla hajaondoka alituombea maombi haya Yoh 17 : 15 ‘Mimi siombi kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu’ ikiwa Bwana Yesu aliomba tulindwe na yule mwovu, hii inamaana kuwa alijua fika utendaji wa ibilisi na jinsi amabavyo maisha yetu yalihitaji ulinzi wa Mungu usiku na mchana. Na ndio sababu ukisoma ule mstari wa 12 ‘a’ anasema ‘nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa nikawatunza,,,,,’ unaweza ukaona jinsi ambavyo Bwana Yesu aliona umuhimu wa sisi kutunzwa, au kulindwa na ndio sababu alipokuwa akiondoka akaomba kwamba tulindwe na yule mwovu, hii ina maana kuwa alikuwa akitambua fika vifungo na manyanyaso ya Adui ambayo yalikuwepo ulimwenguni na ukiendelea kusoma ule mstari wa ‘20’ utakuta akiwaombea na wengine wata…

JE MTU ALIYEOKOKA ANAWEZA AKAVAMIWA NA ROHO ZA GIZA ?

Image
1. Je, anaweza kuwa chini ya vifungo, wakati Yesu alimaliza yote Msalabani? Ndugu mpendwa unayefuatilia mafundisho haya, kila mahali ambako Mungu amenipa neema ya kufundisha masomo haya ya ukombozi nimekuwa nikiulizwa hili swali.na inawezekana hata wewe unashauku ya kujua mengi kuhusiana na hili,
Mpendwa unayefuatilia mafundisho haya, ni kweli kabisa kuwa hata mtu aliyeokoka anaweza akavamiwa na roho za giza.
Na zika athiri mambo yake, kama biashara yake, uchumi wake, ndoa yake na hata maisha yake kwa ujumla na bado akawa anaenda kanisani, anaomba, anaimba, na kufanya baadhi ya mambo, Kumbuka adui mkubwa wa ibilisi ni yule aliyempokea kristo, na ndio maana wakati mwingine kuokoka kumetamkwa kama kutangaza vita, mtu aliyeokoka anafananishwa na mtu ambae yuko vitani na kuwa amezungukwa na maadui kila mahali, na kila adui anatamani kama angelimmaliza yeye maana anasababisha matatizo makubwa kwenye ufalme wa adui bila ya yeye kujua.
Watu wengi kwa sababu ya kutokuyasoma maandiko hudhani ya k…

MTUME MUHAMMAD ALISALI NA VIATU MSIKITINI

Image
Ndugu msomaji, Leo ningependa tujikumbushe na kujifunza kuhusu kusali na viatu katika nyumba za ibada. Waislam mara nyingi wamekuwa wakiwashutumu Wakristo na kuwakejeli kuwa, eti wanasali na viatu Kanisani. Je, Mtume wa Allah aitwaye Muhammad alivaa viatu alipo kuwa anaswali Msikitini? Hebu tuangalia ushahid huu hapa: Ukisoma kitabu cha Al-u-lu wal-marjan Uk. 179
14. Mlango:
Ruhusa ya kusali na Viatu.
325. Hadithi ya Anas Bin Malik (R.a) kutoka kwa Said Bin Yazid Al-Azid (r.a) amesema, Nilimuuliza Anas Bin Malik (r.a) “Hivi Mtume (s.a.w) alisali huku amevaa viatu vyake?” Akanijibu, “Ndiyo” (Bukhari, Hadithi N. 383, Juzuu ya 1)
Hapo tunamuona Muhammad akisali na Viatu, na mlango hapo umesema, Ruhusa ya kusali na Viatu, maana yake waislamu hapo wameruhusiwa kusali na Viatu, pia haikuishia hapo, Muhammad akasema tena kuwaambia Waislamu. Ukisoma kitabu kinachoitwa “TAFSIRI YA BULUGH AL-MARAM MIN JAM’I ADILLATIL AHKAM
Ukurasa wa 101 Hadithi Na. 171
Abu Said (r.a) amesimulia: Mtume (S.a.w) …

POSA SABA (7) ZA MUHAMMAD ZILIZO KATALIWA

Image
1. Kwanini baadhi ya wanawake walikataa posa za Muhammad?
2. Kwanini muhammad aliendelea kuomba/toa posa na huku zikikataliwa? Ndugu msomaji,
Leo nitakua ushahid kadhaa kuonyesha jinsi Muhammad alivyo penda wanawake lakini wengine walikataa posa zake na kuto jali utume wake alio pewa na Mkewe.
Muhammad alimwomba amuoe Ghaziyyah kwa sababu ya uzuri wake, lakini alikataliwa. Tabari anadai kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu lakini hatoi ushahidi. al-Tabari juzuu ya 9 uk.136. Hakuna ushahidi kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu na kwamba Muhammad hakuwa makini kwa kutokumwadhibu, au kwamba hakuwa mwaminifu na Muhammad alimwadhibu.
Layla aligusa bega la Muhammad tokea nyuma na kumuomba amuoe. Muhammad alikubali. Ndugu za Layla walisema, "Ni jambo baya kiasi gani ulilolifanya! Wewe u mwanamke anayejiheshimu, lakini Nabii ni mpenda wanawake. Tafuta kujitengua toka kwake." Layla alikwenda kwa Nabii na kumuomba aikane ndoa hiyo na aliafikianana na hilo [ombi]." al-Tabari juzuu ya 9 u…