Posts

Showing posts from August, 2015

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

YESU NI UPENDO (SEHEMU YA KWANZA)

Image
Shetani anataka tuamini nini kuhusu jinsi Yesu anavyotuona, lakini Yesu anatuhakikishia nini? Hata hivyo, swali muhimu linazuka: Je, Mungu anampenda kila mmoja wetu? Baadhi ya watu wanakubali kwamba Mungu anawapenda wanadamu kwa ujumla kama andiko la Yohana 3:16 linavyosema. Lakini wanahisi hivi: ‘Mungu hawezi kamwe kunipenda mimi.’ Shetani Ibilisi anataka sana tuamini kwamba Yesu hatupendi wala hatuthamini. Kwa upande mwingine, Yesu anatuhakikishia kuwa anamthamini kila mmoja wa watumishi wake waaminifu hata kama tunafikiri hatupendwi au hatuthaminiwi.
Kwa mfano, fikiria maneno ya Yesu kwenye Mathayo 10:29-31. Yesu alitoa mfano huu ili kuonyesha kwamba wanafunzi wake wana thamani: “Je, shore wawili hawauzwi kwa sarafu ya thamani ndogo? Na bado hakuna hata mmoja wao atakayeanguka kwenye ardhi bila Baba yenu kujua. Lakini nywele zenyewe za kichwa chenu zimehesabiwa zote. Kwa hiyo msiwe na hofu: nyinyi ni bora zaidi kuliko shore wengi.” Hebu fikiria jinsi wasikilizaji wa Yesu katika karne …

YESU NI UPENDO (SEHEMU YA PILI)

Image
Huruma ni sehemu nyingine ya upendo wa Yesu.
Huruma ni nini? Katika Biblia, huruma na rehema zinahusiana sana. Maneno kadhaa ya Kiebrania na Kigiriki yanadokeza sifa ya huruma yenye upendo. Kwa mfano, mara nyingi kitenzi cha Kiebrania ra·chamʹ hutafsiriwa “onyesha rehema” au “sikitikia.” Neno hilo la Kiebrania, ambalo Yesu anatumia kujihusu, linahusiana na neno linalomaanisha “tumbo la uzazi” linaloweza kufasiriwa kuwa “huruma ya mama.”
Biblia inatumia hisia ambazo mama huwa nazo kwa mtoto wake mchanga kutufundisha kuhusu huruma ya Yesu. Andiko la Isaya 49:15 linasema: “Je! mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie [ra·chamʹ] mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.” Ni vigumu kuwazia kwamba mama anaweza kusahau kumnyonyesha na kumtunza mtoto wake mchanga. Kwa kweli, mtoto mchanga ni dhaifu; anahitaji kupendwa na kutunzwa na mama yake usiku na mchana. Ingawa hivyo, inasikitisha kupata habari kuhusu akina mama wanaowatupa watoto w…

YESU NI UPENDO (SEHEMU YA TATU)

Image
Yesu ni Mungu Aliye “Tayari Kukusamehe Dhambi” Tunapofanya dhambi tunakuwa na hisia gani zenye kulemea, lakini tunaweza kunufaikaje na msamaha wa Yesu?
Tunapofanya dhambi, sisi huona aibu, hukata tamaa, na kuhisi hatia na huenda hali hiyo ikafanya tufikiri kwamba hatustahili kabisa kumtumikia Mungu. Hata hivyo, kumbuka kwamba Mungu ‘amekuwa tayari kusamehe.’ (Zaburi 86:5) Naam, Yesu anaweza kutusamehe dhambi zetu tunapotubu na kujitahidi kabisa kutozirudia. Ona jinsi Biblia inavyofafanua sehemu hiyo yenye kuvutia ya upendo wa Yehova.
Yesu Kristo anayo amri na mamlaka ya kusamehe dhambi
Kuna jambo lililowahi kutokea hadi likawashangaza watu; hebu fatilia kisa hiki. Biblia Takatifu inasema kwamba:
“Wakaja watu wakimleta mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia (Yesu) kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwen…

YESU NI UPENDO (SEHEMU YA NNE)

Ndugu yangu, wajua yakwamba Yesu Kristo anakupenda ? Wajuwa yakwamba alisulubiwa kwa ajili ya watu wote: Wanaume na Wanawake, Watoto, Vijana na Wazee?  Yesu Kristo alikufa kwa ajili yako.

Yesu anakupenda sana, inawezekana kuna mtu anakupenda sana ila Yesu anakupenda zaidi ya wote duniani hivyo nakushauri ukate shauri umfuate yeye maana atakupa kustarehe milele na kuurithi ufalme wa mbinguni pamoja naye.

TAFAKARI: “Yesu anakupenda upeo, amepoteza kila kitu, na kufa kifo cha aibu ili asikupoteze.”


JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mnyanganyi, mwizi, mwongo, muuaji, usiye kuwa na ukweli? Yesu anakupenda na anataka kukuponya.


JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mlozi mkubwa mwenye kutumikia Shetani, tangu ujana wako unazuru wanadamu wengine, unaua watoto, wanawake hata wanaume, unaharibu mavuno, unatawanya magonjwa toka jamaa kwa ingine, unaua hapa na pale.Unapopita ni woga mtupu na kukimbia mbali sababu ya mapepo mabaya yako. Mara na mara unajiuliza nini ulikuja kufanya hapa dunian…

Ubatizo Wa Roho Mtakatifu

Mtu anaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, utendaji wa Roho Mtakatifu katika kanisa la kwanza ni dhahiri kwenye kila ukurasa. Ukiondoa kazi ya Roho Mtakatifu katika kitabu cha Matendo, huna kitu kilichobaki. Kweli, aliwatia nguvu wanafunzi wa kwanza ili “kuupindua ulimwengu” (tazama Matendo 17:6).
Siku hizi katika dunia yetu, mahali ambapo kanisa linakua kwa haraka ni pale ambapo wafuasi wa Yesu wmejitoa kwa Roho Mtakatifu kabisa na kuwezeshwa Naye. Hili lisitushangaze. Roho Mtakatifu anaweza kufanikisha mambo mengi kwa muda wa nukta kumi kuliko tunayoweza kufanikisha sisi kwa muda wa miaka elfu kumi, kwa juhudi zetu. Kwa hiyo, ni kitu muhimu sana kwamba mtumishi anayefanya watu kuwa wanafunzi aelewe Maandiko yanafundisha nini juu ya kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha na huduma za waamini.
Mara kwa mara katika kitabu cha Matendo ya Mitume tunapata mifano ya waamini wakibatizwa kwa Roho Mtakatifu na kuwezeshwa kufanya huduma. Tuwe na busara kujifunza somo hili ili ikiwezekana, hata si…

KAMA YESU ALIKUWA NI MUNGU, JE ALIKUWA ANAMWOMBA NANI?

Image
Swali la Yesu ni Mungu na nani alikuwa anamwomba, huwa linaleta utatanishi mkubwa sana na kama usipo kuwa makini, unaweza kuanza kuuliza maswali katika imani yako ya Ukristo. Katika mijadala mbali mbali ya kidini, wanadhuoni wa Kiislam na hata Mashahidi wa Yehova huwa wanauliza:- Yesu alipo kuwa katika Bustani ya Gethemane, alikuwa anamwomba nani? Tena zaidi ya hapo, wanauliza, tokea lini Mungu akaomba msaada? Hakika maswali haya yanahitaji majibu thabit tena yenye aya za Biblia.
Ili umwuelewe Yesu kama Mungu duniani akiomba kwa Baba yake mbinguni , tunahitaji kutambua kwamba Mungu Baba na Yesu “Mwana” walikuwa na uhusiano wa milele kabla ya Yesu kuuchukua mwili wa mwanadamu. Zaidi ya hapo, itakupasa uelewe kuwa, Yesu alipo kuwa duniani alikuwa na asilia mbili, yaani Yesu alikuwa Mungu na wakati huo huo alikuwa Binadamu (Rejea katika Kijarida cha “Asilia mbili za Yesu Kristo”). Tafadhali soma Yohana 5:19-27, hasa mstari wa 23 ambapo Yesu anafundisha kwamba Baba alimtuma Mwana (pia taza…