Posts

Showing posts from April, 2015

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU, WAKUJUE WEWE ULIYE MUNGU WA PEKEE, WA KWELI NA YESU KRISTO ULIYE MTUMA

Ndugu wasomaji, Leo nitaielezea aya ya Yohana 17: 3 ambayo Waislam wamekuwa wakiitumia mara nyingi sana kudai kuwa eti, Yesu amekana kuwa yeye ni Mungu. Waislam kwa kupitia mihadhara ya kidini na kwa kutumia vijarida mbali mbali wanatishia Umma wa Wakristo kuwa, Yesu ameukana Uungu. Je, hayo madai ya Waislam ni kweli? Je, hiyo aya ina la zaidi la kujifunza? Ili uielewe Biblia vizuri, nilazima usome aya kadhaa ili upate kuelewa nini hasa Mungu anasema kupitia Neno lake. Hivyo basi, nimeweka aya ya 4 na ya 5 ili kufafanua nini hasa Yesu alikuwa anasema katika Yohana 17. Ngoja niziweke aya zote hapa: Yohana 17: 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.4 Nimekutukuza Wewe duniani kwa kuitimizaile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako. Yesu katika aya ya 5 [Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoj…

SIFA SABA ZA ROHO MTAKATIFU

Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 17Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu. Yesu Kristo ametupa zawadi ya ajabu sana: Zawadi ya Roho Mtakatifu. Katika baadhi ya maeneo, zawadi hiyo inajulikana kama Roho Mtakatifu, na sehemu nyingine ametajwa kama Msaidizi (Msaidizi na Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu ni sehemu ya tatu ya Uungu, sehemu ya tatu ya Utatu wa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Yeye ni Msaidizi katumwa na Yesu, baada ya Msaidizi wetu kuja ambaye ni Roho Mtakatifu, Yesu alipaa tena mbinguni. Roho Mtakatifu hutolewa kwa wote ambao wamempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao
Kuna mambo saba ambayo tunahitaji kuelewa kuhusu Roho Mtakatifu. Tunajua kwamba, katika Biblia, saba ni namba ya kukamilika/ kukamilisha, au ukamilifu, na sifa saba zote tofauti za Roho Mtakatifu ni kweli kamili na kamilifu. Tunaweza kuzi…

KAMA YESU ALIKUWA NI MUNGU, JE ALIKUWA ANAMWOMBA NANI?

Swali la Yesu ni Mungu na nani alikuwa anamwomba, huwa linaleta utatanishi mkubwa sana na kama usipo kuwa makini, unaweza kuanza kuuliza maswali katika imani yako ya Ukristo. Katika mijadala mbali mbali ya kidini, wanadhuoni wa Kiislam na hata Mashahidi wa Yehova huwa wanauliza:- Yesu alipo kuwa katika Bustani ya Gethemane, alikuwa anamwomba nani? Tena zaidi ya hapo, wanauliza, tokea lini Mungu akaomba msaada? Hakika maswali haya yanahitaji majibu thabit tena yenye aya za Biblia.
Ili umwuelewe Yesu kama Mungu duniani akiomba kwa Baba yake mbinguni , tunahitaji kutambua kwamba Mungu Baba na Yesu “Mwana” walikuwa na uhusiano wa milele kabla ya Yesu kuuchukua mwili wa mwanadamu. Zaidi ya hapo, itakupasa uelewe kuwa, Yesu alipo kuwa duniani alikuwa na asilia mbili, yaani Yesu alikuwa Mungu na wakati huo huo alikuwa Binadamu (Rejea katika Kijarida cha “Asilia mbili za Yesu Kristo”). Tafadhali soma Yohana 5:19-27, hasa mstari wa 23 ambapo Yesu anafundisha kwamba Baba alimtuma Mwana (pia taz…

Kweli 100 Kuhusu Yesu

1. Yesu alidai kuwa Mungu, (Yohana 8:24, 8: 56-59 (angalia Kutoka 3:14), Yohana 10: 30-33) 2. Yesu anaitwa Mungu, (Yohana 1: 1, 14; 20:28; Kol 2: 9, Tito 2:13; Ebr 1: 8.) 3. Yesu ni mfano wa Mungu asiyeonekana, (Ebr 1: 3.) 4. Yesu anaishi milele, (Ebr. 7:24) 5. Yesu aliumba vitu vyote, (Yohana 1: 1-3; Kol 1: 15-17) 6. Yesu kabla ya vitu vyote, (Yohana 1: 1-3; Kol 1:17) 7. Yesu ni wa milele, (Yohana 1: 1, 14; 8:58; Mika 5: 1-2) 8. Yesu anaheshimiwa sawa na Baba, (Yohana 5:23) 9. Yesu ana abudiwa (Mathayo 2:. 2, 11; 14:33, Yohana 9: 35-38; Waebrania 1: 6). 10. Yesu ni yupo kila mahali "omnipresent" (Mathayo 18:20;. 28:20) 11. Yesu yu pamoja na sisi siku zote, (Math. 28:20) 12. Yesu ni mpatanishi wetu pekee kati ya Mungu na sisi wenyewe, (1 Tim 2: 5.) 13. Yesu ni mdhamini wa agano bora, (Ebr 7:22; 8: 6). 14. Yesu alisema, "Mimi ndimi mkate wa uzima" (Yohana 6:35, 41, 48, 51) 15. Yesu alisema, "Mimi Mlango", (Yohana 10: 7, 9) 16. Yesu alisema, "Mimi ni …

ASILIA MBILI YA YESU KRISTO “MUNGU NA BINADAMU”

Tokea Dunia ianze, hapajawai toke Mtu yeyote alieishi kama Yesu Kristo. Yesu ni mtu wa maana sana ambaye ni Mwokozi, Mungu katika Mwili “Emanueli” (Isaya 9:6). Yesu sio Nusu Mungu na Nusu Binadamu kama watu na au imani nyingi zinavyo sema. Yesu yeye ni Mungu na ni Binadamu kwa wakati mmoja. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa na asilia Mbili tofauti ambazo ni Mungu na Binadamu kwa wakati mmoja.
Biblia inasema kuwa, Yesu ni “Neno” ambaye ni Mungu na alikuwa kwa Mungu na akafanywa kuwa Mwili na kuishi nasi, soma Yohana 1:1 na 14. Hii inamaanisha kuwa, mtu huyu mmoja ambaye ni Yesu alikuwa ana asilia mbili za Mungu na Binadamu.
Hii asilia ya Mungu haikubadirika pale ambapo “NENO” lilipo kuwa Mwili (Yohana 1:1, 14). Badala yake, Neno liliunga ubinadamu (Wakolosai 2:9). Hivyo basi, Umungu wa Yesu Kristo haukuharibika na au badirika. Zaidi ya hapo, Yesu hakuwa mtu tu ambaye alikuwa na Mungu ndani yake au Mtu aliye fanya kazi ya Mungu pekee, la hasha, Yesu ni Mungu katika Mwili na ni sehemu ya P…

Similarities between Non-theism and Islam

Similarities between  Non-theism and Islam
EXHIBIT 1
Both Non-theists and Muhammadans deny the existence of God.
Islam:
1. Allah: There is NO God but Allah, ……
Non theists:
2. Darwinites: God does not exist,……As you can see, both non-theists and Muslims deny the existence of God.

EXHIBIT 2
Both Non-theists and Muhammadans support evolutions:
Islam: 
1. Allah will change all Jews into Apes and Pigs…….
Non theists:
2. Man evolved from Monkeys, …..As you can see, both non-theists and Muhammadans dogma fallacies say humans are related to Primates.

UTHIBITISHO WA UTATU WA MUNGU

Hatuna budi kila mmoja wetu kutambua kuwa tunaishi katika nyakati za hatari. Nyakati tulizonazo zinaitwa nyakati za hatari kutokana na watu wengi watakaojitenga na imani wakisikiliza mafundisho ya mashetani na roho zidanganyazo- 1TIMOTHEO 4:1;

2TIMOTHEO 3:1; 2TIMOTHEO 4:3-5.
Moja kati ya mafundisho yaliyo kinyume na imani ni kukana utatu wa Mungu. Kwa mfano kusikiliza mafundisho ya mashahidi wa Yeheva na mahubiri mbalimbali ya akina William Brauham yanayodai kuwa hakuna UTATUwa Mungu bali Yesu ndiye Baba, Mwana na Roho mtakatifu. Pamoja na kwamba alianza vema huduma hii lakini hatimaye akakengeuka. Kwa hiyo somo hili ni la msingi mno kwa kila mkristo ili kuishindania imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu-YUDA 1:3.

Somo hili limegawanywa katika vipengele sita ( 6 ) vifuatavyo:-
1. MAFUNDISHO NA ROHO ZIDANGANYAZO KUHUSU UTATU WA MUNGU2. NAFSI TATU ZA MUNGU KATIKA BIBLIA3. UTHIBITISHO KUWA YESU SIYO BABA4. USIBITISHO KUWA YESU SIYO ROHO MTAKATIFU5. UTHIBITISHO KUWA ROHO MTAKATIFU SIY…