Posts

Showing posts from 2015

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

TOFAUTI KUMI NA SABA (17) KATI YA YESU WA WAKRISTO NA ISA WA WAISLAM

Image
Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” .
Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”,

Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an.(Qur’an is a post Bible book).

UTAMU WA MAISHA YA NDOA

Image
(Sehemu ya Kwanza)
NDOA NI NINI?Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. Kwa kuwa si kusudi letu kutafakari sheria za nchi zinasema nini kuhusu Ndoa, tungependa kujikita zaidi katika maana ya Ndoa kwa imani ya kikristo ambayo msingi wake unajengwa katika neno la Mungu. Hata hivyo tunapenda kuweka wazi kwamba Ndoa ni suala la kisheria, na ni muhimu sana kwa wanandoa kutambua kwamba zipo taratibu za kisheria zilizowekwa na serikali zinazosimamia masuala ya Ndoa. Kwa kuwa tumefanyika wana wa Mungu, mwenendo wetu na maisha yetu ya Ndoa yanaongozwa na imani yetu kwa Mungu na si sheria za kibinadamu. Katika imani ya kikristo, Ndoa inaweza kutafsiriwa kama “AGANO KATI YA MWANAMKE NA MWANAMUME AMBAO WAMEKUSUDIA KWA HIARI KUAMBATANA NA KUISHI PAMOJA KAMA MKE NA MUME KWA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAO.” Jambo la msingi kulitambua hapa ni kwamba Ndoa ya kikristo ni AGANO. Kuna tofauti kubwa kati ya kile kinachoitwa “AGANO” na “MKATABA” kimsi…

KWANINI HAKUNA NGUVU YA UPONYAJI KATIKA UISLAM? MBONA KATIKA UKRISTO WATU WANAPONA KWA JINA LA YESU?

1. KWANINI JINA LA ALLAH HALINA UWEZO WA KUPONYA MAGONJWA? 2. ALLAH ASHINDWA KUMPONYA MUHAMMAD 3. MAOMBI YA JIBRIL YAGONGA MWAMBA 4. LAKINI JINA LA YESU LINAPONYA MAGONJWA YOTE 5. JE, UMESHA WAI ONA KUNA MKUTANO WA UPONYAJI KATIKA USILAM?
Ndugu msomaji,
Uponyaji ni nini? Ni tendo la kiimani la kupokea uzima katika roho au mwili kwa njia ya kuombewa,kuwekewa mikono au kulisikia neno sahihi la Kristo Yesu. Tendo hili la kiimani humletea mwamini uzima wa kiroho na afya ya kimwili pale ilipopunguka,kumbuka~wengi walipoponywa udhaifu wa miili yao,waliponywa pia na roho zao.
Hivyobasi, kwanini Allah alipo mtuma Jibril kwenda kumuombea uponyaji Mtume wake Muhammad kwa ugonjwa uliosababishwa na kula sumu, maombi yao hayakufanya kazi?
Hivyo basi, uponyaji haufanywi na mtu awaye yoyote yule isipokuwa Mungu. Hata madaktari bingwa wao hawaponyi bali hutoa tiba tu, mwenye kuponya ni Mungu. Watumishi wa Mungu pekee ndio hufanyika kama daraja au chombo cha kuleta uponyaji ulioachiliwa na Bwana kwa muhusika…

JINSI YA KUTOA PEPO WABAYA/CHAFU

Image
Maana ya neno pepo linamaanisha, pepo mbaya, shetani, mwovu, mharibifu na mwangamizi. Hao ni malaika waliomuasi Mungu wakatupwa duniani. “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka (Shetani), Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, Yule wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufu 12:7-9. 1. Ili kutoa pepo, kuna mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa:
Ni lazima uwe na nguvu za Roho Mtakatifu.Tunaweza kujifunza kwa Yesu alivyoweza kutoa pepo kwa uwezo na nguvu za Roho. Imeandikwa, “…..awaaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36. 2. Kutoa pepo kwa jina la Yesu. Aliye na amri na mamlaka ya kutoa pepo ni mkristo ambaye amemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pe…

ZIJUE AHADI ZA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO

Image
Mungu hutimiza ahadi zake. Imeandikwa katika 2Wakorintho 1:19-20 "Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yaani mimi na Silwano na Timotheo hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa sisi." Mungu hazirudishi ahadi zake au kuzibadilisha. Imeandikwa katika Zaburi 89:34 "Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno lililotoka mdomoni mwangu." Hakuna mojawapo ya ahadi za Mungu ambazo hazijatimika. Imeandikwa katika Yoshua 23:14 "Angalieni mimi nimekwenda njia ile waendayo watu wote wa ulimwengu...... Mungu wenu katika habari zenu yote yametimia kwenu hapana neno lo lote mlilopungukiwa." Tumeahidiwa uzima wa milele. Imeandikwa katika 1 Yohana 2:25 "Nahii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani uzima wa milele."
Mungu aweza kufanya mambo yasiyowekana. Imeandikwa katika Luka 18:27 "Akasema yasiyowezekana kwa …

YESU NI MUNGU AMBAYE ANAPONYA MAGONJWA YOTE

Image
Yesu alisema kwamba ishara moja itakayofuatana na waaminio ni kwamba wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapona (ona Marko 16:18). [Yesu] Akawaambia, Enendeni ulimwengu mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya (Marko 16:15-18). Mtumishi afanyaye watu kuwa wanafunzi, akiwa anaiga huduma kamilifu ya Kristo, hakika atatumia vipawa vyake kuendeleza huduma ya uponyaji wa Mungu katika eneo lake la ushawishi. Anajua kwamba uponyaji wa Mungu hukuza ufalme wa Mungu kwa njia mbili. Kwanza – miujiza ya uponyaji ni matangazo mazuri sana kwa Injili, kama mtoto yeyote anayesoma Injili au kitabu cha Matendo atakavyoelewa (ingawa watumishi wengi wenye madigirii makubwa wanaonekana hawaelewi). Pili – wanafunzi wenye afya nje…

YESU NI MUNGU NA ANATAKA KUKUOKOA

Image
Watu wengi wanaelewa kuwa Yesu alikuwa mtu ambaye aliishi Israeli miaka 2000 iliyopita. Takribani kila dhehebu ulimwenguni lamchukulia Yesu kama mwalimu mwema/nabii. Huku hayo mambo yakiwa kweli kuhusu Yesu, hayaangazii kabisa Yesu kwa ni nani, ama kuelezea jinzi au kwa nini Yesu aokoa. Yesu ni Mungu katika mwili wa binadamu (Yohana 1:1,14). Yesu ni Mungu, alikuja ulimwenguni kama mwanadamu wa kweli (1Yohana 4:2). Mungu alikuja akawa mwanadamu katika Yesu ili atuokoe. Hiyo yaleta swali lifuatalo: Ni kwa nini tunaitaji kuokolewa? Yesu anawaokoa wale wote wanaopokea tuzo lake la wokovu. Yesu anawaokoa wale wote wanaomwamini katika dhabihu yake pekee kama fidia ya dhambi (Yohana 3:16; Matendo 16:31). Huku Yesu kama dhabihu ilikuwa kamilifu na yatosha kulipia dhambi zote za binadamu, Yesu pekee ndiye aweza kuokoa wale pekee wanaoipokea zawadi yake (Yohana 1:12) Kama sasa unaelewa yamaanisha nini Yesu aokoa, na unataka kuweka imani kwake kama mwokozi wa maisha yako, akikisha kwamba unaelew…

UTHIBITISHO 12 KUWA ALLAH SIO MUNGU

Image
Leo nitawapa Sababu 12 kwanini allah sio mungu. 1. ALLAH NI MUNGU ASIYE NA JINA KAMILI
Qr. 17 au surat Bani Israil 110 (Wana wa Israil)
Sema; muombeni (Mwenyenzi Mungu) kwa (jina la) Allah au muombeni (kwa jina la) Rahman. Kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa). Kwani ana majina mazuri mazuri……… 2. ALLAH NI MUNGU MWENYE MAADUI AMBAO NI WAKRISTO NA WAYAHUDI
mungu wao ana maadui wake ambao ni wakristo na wayahudi
Qr. 4:51 na 57 (surat Al Maida)
Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika hao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. 3. ALLAH NA WAISLAM WOTE KUINGIA JEHANNAM
Wafuasi wote wa Allah wanangojea moto wa jehanam kisha waokolewe waislam baadaye kutoka motoni
Qr. 19:70-72
Tena hakika sisi tunawajuwa vyema Zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia.
Hiyo ni hukumu ya Mola wako mlezi ambayo lazima itimizwe.…

USIKUBALI KUWA MPUMBAVU KWA KUKATAA KUWA HAKUNA MUNGU NA KUWA YESU NI MUNGU

Image
Kuna imani nyingi sana hapa duniani, zingine zinadai kuwa "Hakuna Mungu" eti, kwasababu wameshindwa kuongea nae na au kumwona; Imani zingine zinadai kuwa "Hakuna Mungu" eti kwasababu Sayansi inashindwa kuhakikisha uwepo wake scientifically; Imani zingine zinadai kuwa, kivipi Yesu awe Mungu na biandamu kwa wakati mmoja, zinadai eti, Mungu halali, wala hali chakula, lakini wakati huo huo wanakiri kuwa Mungu anaweza kufanya jambo lolote lile atakalo; Haya yote ni madai ambayo hawawezi kuyathibitisha. Hebu tusome Biblia: 2 Samweli 2:31-34 na Zaburi 14:1 ‘Mpumbavu amesema moyoni, mwake hakuna Mungu…..’ Mpenzi msomaji naamini unaendelea vema kwa ujumla kimwili na kiroho. Katika mwezi huu nataka niseme nawe juu ya kifo cha kipumbavu. Mpumbavu ni nani? Kibiblia ni mtu yoyote aliyekataa kuwa na ufahamu au elimu ya Mungu ndani yake. Mtu aliyekataa uwepo wa Mungu au kuwa na Mungu maishani mwake. Hivyo basi mpumbavu ni mtu ambaye moyoni mwake amesema hakuna Mungu. Mauti inayom…

UTHIBITISHO 10 KUWA YESU NI MUNGU

Image
“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno! Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.” Kwa madai haya hata kwenye Qurana hawawezi thibitisha kuwa Allah Allah ni mungu, zaidi ya hapo, hata Utume wa Muhammad unakuwa kwenye njia panda, maana hakuna aya kwenye Quran Muhammad anasema mimi Muhammad ni mtume wa Mungu. Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21). Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.
1. YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUZALIWA
Ufua…

UPONYAJI KATIKA JINA LA YESU

Image
Leo ninaweka aya kadhaa zinazo tupa mamlaka ya kuombea wagonjwa. Mungu akubari mpendwa na pokea uponyaji wako leo katika Jina la Yesu aliye hai. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote. - [Zaburi 34:19] Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. - [Yakobo 5:14-16] Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. - [Zaburi 107:20] Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana. - [2 Wafalme 20:5b] Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa…

MAOMBI YA USHINDI KWA MAISHA YAKO

Image
Baba katika Jina la Yesu. Laana zote nilizo tupiwa na wabaya wangu zimeshindwa kwa jina la Yesu na nazivunja na kuzisambaratisha kwa Damu ya Yesu. Mshindwe wote mnao tuma laana kwangu katika Jina la La Yesu. Nawavunja na kuwaharibu na kuwakatakata Wachawi wote kwa damu ya Yesu. Nasambaratisha kila neno la uovu lililosemwa juu yangu na familayangu katika jina la Yesu. Naharibu na kuisambaratisha madhabahu yenu mliyo fanyia kafara kwa damu ya Yesu. Navunjavunja na kubomoa kila uovu na uchawi mnaonifanyia katika jina la Yesu. Nairudisha misukule yote na majini yote yawarudie nyie na kuwalipa dhambi zote mnazo fanya katika jina la Yesu. Naharibu kila uchawi, kila urogi, kila ndumba kila aina ya uovu ambao mnaufanya ili uniumize mimi na familia yangu katika jina la Yesu. Nawateketeza kupitia damu ya Yesu Wachawi wote walio tumiwa kunitumia uchawi katika jina la Yesu. Nawateketeza na kuwaharibu majini yote yaliyo tumwa kuja kufanya kazi hiyo waliyo tumwa na Wachawi katika jina la Yesu. Nawa…

MAOMBI YA KUFUNGA MWAKA NA KUANZA MWAKA MPYA 2016 KWA BARAKA TELE KUTOKA KWA MUNGU MKUU, YESU KRISTO ALIYE HAI

Image
Ndugu msomaji na mpendwa katika Bwana. Bwana Yesu apewe sifa. Mpendwa, yawezekana umekuwa ukiishi bila kutambua uwezo wa jina la Yesu katika kukuonyesha mwelekeo wa maisha yako.Je, unahitaji mwelekeo mpya katika maisha yako? Je, unahitaji kujua njia ya kutoka katika hali uliyonayo? KAMA UMECHOKA NA MAISHA YA TABU, KAMA UMECHOKA KUISHI NA MAGONJWA, KAMA UMECHOKA KUWA MASKINI, KAMA UNAHITAJI KAZI, BIASHARA YAKO IFANIKIWE N.K. BASI HUU UJUMBE NI WAKO. Napenda kukufahamisha kuwa, tupo katika Maombi kila siku mpaka tutakapo maliza mwaka huu wa 2015. Nafahamu wengi mmepata baraka tele katika Mwaka wa 2015 na labda wengi mmlikuwa katika mashindano na vita kubwa na nguvu za giza. Kumbuka USHINDI ni wetu katika Jina la Yesu. Mpendwa , pengine hali ya maisha uliyonayo imekufanya ukate tamaa na kujiona kwamba hakuna njia ya kukufanya utimize furaha ya ndoto zako. Je, unahitaji njia ya kuishi kwa amani na furaha; njia ya kuwa na mahusiano mazuri katika ndoa yako; njia ya kuwa na mahusiano mazuri …