Posts

Showing posts from April, 2014

SUPPORT MAX SHIMBA MINISTRIES

Ni Nani Walikuwa Waandishi Wa Qur,aan Tukufu Wakati Wa Mtume Saw?

KORAN HAIKUTEREMSHWA KUTOKA KWA ALLAH Je, ungependa kuwafahamu waandishi wa Koran? Katika somo letu la leo, tutajifunza kuhusu waandishi wa Koran. Je, ni kweli Koran ilishushwa? Je, kuna ushaidi wa kutosha wa kusaidia madai ya kuteremshwa kwa Koran? Unaposema kuwa Allah ndie mwandishi wa Qur'ani, ni uongo mkubwa sana  na wengi wameukubali huu uongo na udanganyifu kwamba eti Koran ilishushwa wakatia inafahamika kuwa iliandikwa miaka 1400AD. Mtu mwenye fikra anaweza kusema bila ya wasiwasi kuwa Qur'ani iliandikwa na watu kadhaa ambao wanajulikana kimajina. Waandishi Mashuhuri zaidi miongoni mwao ni hawa hapa: Imrul Qays-mshairi: wa kale wa Arabia ambaye alifariki miaka michache kabla ya kuzaliwa Muhammad Zayd b. Amr b. Naufal:-'lililopotoka' wa wakati wake ambaye alihubiri na kupandwa Hanifism Labid:-mshairi mwingine Hasan b. Thabit:-mshairi rasmi wa Muhammad Salman: – Mshauri wa Kiajemi wa Muhammad Bahira:-Nestoraian Mkristo mtawa wa Kanisa huko Syria Jabr:-Jirani wa Kikristo wa…

UTATA WA ALLAH KATIKA KUSAMEHE WATU DHAMBI

Je, Allah anao uwezo wa Kusamehe watu dhambi? Ndugu zanguni, Leo ningependa tumuangalie Allah wa dini ya Uislam ambaye wanasema ndie Mungu wao. Je, huyu Allah anayo mamlaka ya kusamehe dhambi zote? Ungana nami katika some letu la leo na tuone utata mkubwa sana uliopo ndani ya dini ya Uislam. Tuanze na Surat Azzumar aya 53 na 54 ambazo zinadai na kusema kuwa, Allah anasamehe dhambi zote, hebu tusome kwanza: Surat Azzumar 53. Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 54. Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya kukujieni adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa. Katika aya hizo hapo juu, tumesoma kuwa Allah anasamehe dhambi zote na labda tukubaliane naye kwasasa kwa ajili ya kujifunza Utata na Mashaka yalio ndani ya kitaa'b cha Allah. SASA TUANAGALIE VIFUNGU VINGINE AMBAVYO ALLAH ANASEMA KUWA, HANA UWEZO WA KUSAMEHE DHAMBI Sasa re…

JAMANI EEEE ALLAH AMEFIRISIKA SASA ANANUNUA WATU?

KUMBE ALLAH NI MFANYA BIASHARA..............
Suratut Tawba 111. Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa
UKIONA ALLAH ANANUNUA WATU, BASI ELEWA KUWA YESU ANABATIZA KWA MALUNDO.
Hakika hakuna Mbingu wataingia watu walio nunuliwa na Allah.

MUHAMMAD SIO MTUME KWASABABU HAKUWAI ONGEA NA MUNGU

Leo ningependa tujikumbushe mambo machache ambayo labda hatukuyatilia maanani. Mitume wote na manabii wote wa Biblia waliwai ongea na Mungu. Lakini, Mtume wa Allah "Muhammad" hakuwai ongea na Mungu HATA MARA MOJA. Je, utume wake tutauamini vipi maana hakuwai ongea na aliye mtuma?
Lakini Mitume wote wa Biblia waliongea na Mungu.
1. Musa anoangea na Mungu: Kutoka 3:1-21
2. Elia anaongea na Mungu: 1 Wafalme 19- Soma yote
3. Paulo anaongea na Mungu: Matendo ya Mitume 18:9
Hiyo ni mifano michache kutoka Biblia.

Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu?

KUMBE ALLAH ANAYE MSAIDIZI

UTATA NDANI YA KURAN KUHUSU UTAMBULISHO WA ALLAH!!
KUMBE ALLAH ANAYE MSAIDIZI


Je, Allah anaye Msaidizi, mbona anatumia wingi katika kujieleza?
Hebu rejea kwenye Kuran kwanza:

Suratul Anbiyaa 91. Na mwanamke aliye linda uke wake, na TUKAmpulizia katika roho YETU, na TUKAmfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu
.
Ndugu zanguni, Allah ameanza vituko vyake hapa. Katika Koran Allah anadai kuwa hana msaidizi Suratul Baqarah: aya 106 ― 107 Lakini katika aya tuliyo isoma hapo mwanzoni - Suratul Anbiyaa 91 tumeona kuwa Allah anatumia wingi alipo kuwa akielezea jinsi alivyo mpa ujauzito Maryam. 

ALLAH ANAMUUMBA ISA BIN MARYAM KWA KUTIMIA WINGI
Kuran imejaa utata, hebu soma hapa Suratul Attahriim 12. Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na TUKAmpulizia humo kutoka ROHO YETU, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu. 

HAPA: Allaha anasema kwa undani zaidi TUKAmpulizia ROHO YETU. Hivi huyu Allah ni kweli ali…

Eti Biblia inataja mashehe, kwa hiyo inaunga mkono Uislamu!

Image
Wahubiri wa ‘injili’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha quran kupitia Biblia. Nasema ‘kuhaha’ kwa sababu hakika kabisa wana juhudi kubwa mno lakini inasikitisha kwa sababu hakuna hata siku moja waliyowahi kusema jambo lenye ukweli kibiblia linalounga mkono quran kama wasemavyo wao – Mungu ni shahidi yangu. Mara waseme Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia; mara waseme Yesu aliposema kuwa ataletwa Msaidizi basi alimaanisha Muhammad, n.k. Ni kituko kimoja baada ya kingine. Na wanayemdanganya ni wao wenyewe pamoja na Wakristo wachache wasiojua Biblia.

Kwa msingi huohuo, wanasema eti Biblia imewataja mashehe; na kwa hiyo kwao huo ni ushahidi kuwa uislamu ulikuwapo tangu zamani.
Acha ninukuu hoja ya mmoja wao kama ilivyo, kuhusiana na suala hili, kisha kama kawaida, utaona jinsi hoja hiyo inavyosambaratika mbele za nuru ya Kristo, yaani neno lake.

YESU ALIISHI KABLA YA DUNIA KUUMBWA

Yohana 17:5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. 
Katika aya hapo juu tunasoma kuwa Yesu aliishi kabla ya kuumbwa ulimwengu. 
Kumbe basi Yesu si Nabii tuu, kama wanavyo dai Waislam kuwa eti, Yesu ni Nabii tu na si zaidi ya hapo. Kumbe Yesu ni zaidi ya Nabii, maana aliishi kabla ya kuzaliwa. 

Ndugu zanguni, nani aliye ishi kabla ya Uumbaji? Hata Koran inakiri kuwa, kabla ya kuumbwa kwa vitu vyote, alikuwepo Mungu. YESU ANASEMA KUWA, ALIISHI KABLA YA UUMBAJI. (Yohana 17:5).

Kumbe basi, Yesu ni Mungu maana alikuwepo wakati wa uumbaji. Wakolosai 1: 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 

Tumesoma katika Wakolosai kuwa katika Yesu kila k…

JINA LA YESU LINAMAMLAKA YA KURUDISHA MALI ZAKO ZOTE

Ndugu Msomaji: Leo ningependa tujikumbushe jambo Fulani kuhusu maisha yetu ya kila siku.

Hebu kwanza tusome neno la Mungu kama lilivyo andikwa katika Isaya:

Isaya 42:22‘Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.’

Inawezekana kabisa labda huelewi kuwa, shida zako zote zimesemwa katika hii aya hapo juu. Labda hufahamu kuwa wewe ni tajiri na Shetani amekuwa akikuibia mali zako. Labda hufahamu kuwa wewe ni Msomi na ulitakiwa uwe na Madigirii kadhaa. Labda hufahamu kuwa wewe ni Kiongozi Fulani ambae ameibiwa uongozi wake, “nyota yako”.

Leo ningependa ufahamu kuwa Shetani ni Mwizi na anaweza kukuibia wewe unae soma huu ujumbe. Ningependa ujiulize, hivi, Je, huyu Shetani alikuibiaje wakati wewe ni mtoto wa Mungu na umeokoka?

Katika Injili kutokana na Yohana 10:10 inasema kuwa: Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi na…

PASAKA NI NINI NA MAANA YAKE

Pasaka ni sikuku iliyoamriwa na Mungu tangu siku za kale kwa wayahudi kuifanya katika mwezi wa Abibu au Nisani katika “kalenda ya kiebrania” yaani mwezi wa 3 au 4 katika kalenda ya kirumi, kwa lengo la kumbuka njisi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani Misri; Twasoma: “Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako. Nawe umchinjie pasaka BWANA, Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.” (Kumbukumbu 16:1-2) Soma pia: (Kutoka 12:14) Kama tulivyoona katika pasaka wayahudi waliamriwa kuchinja mnyama mmoja katika kundi, lakini tunapoendela kusoma tunaona jinsia Mungu alivyoamuru mnyama huyo aokwe na kuliwa; Twasoma:
“Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoa nchi ya Misri, siku zot…